Ushauri wenu Wakuu, Wahadhiri wanaoomba rushwa ya ngono wamemfikia mtoto wangu

Ushauri wenu Wakuu, Wahadhiri wanaoomba rushwa ya ngono wamemfikia mtoto wangu

Mwambie amrekodi akiwa anaongea awapelekee pccb! Mimi nilikutana na huyo mshenzi, nilikuwa mjeuri nikacarry nikakomaa nikatoboa! Ilipotea test moja tu ndio sababu ya kurudia mtihani mwalimu anashindwa kuweka records, ukifika ofisini anakwambia we binti una shape hivi! Anaanza kukusogelea! Aisee na akijichanganya akalala naye ndio bye bye atamtumia mpaka achoke na hachomoi hiyo supp! Kuna dada alikaa miaka mi5 chuo!
 
Sina huo ushahidi zaidi ya stori za huyo mwalimu kufahamika na wanafunzi wa chuo hicho, option iliyopo ni kukata rufaa lakini vyuo vyetu mwalimu wa department hiyo hiyo atasahihisha na atambeba mwalimu mwenzake kama kawaida yao
Aandike barua aombe rufaa asahihishiwe mtihani na mwl mwingine ila kama ana uhakika atafaulu na aweze kulipia hizo gharama!
 
Huyu mtoto wangu amepitia hii changamoto mwaka Jana mpaka mtoto akatoa pesa bila sisi kujua,

Bahati mbaya tena mwaka huu mwalimu alikuwa anawafundisha pia amempa supp na ameahidi hachomoi mpaka ampe mapenzi, na inasadikika ameungua wakuu msaada wenu
Uwe mwangalifu sana na stori za vijiweni, na habari za huyo mwanao.

Hakuna 'chuo' chenye hadhi kinachoweza kutoa 'supp' bila ya maelezo ya msingi.
Ushahidi hauwezi kujificha; kama ni 'supp' ni supp' hata uende wapi!

Mwanao atakuwa na udhaifu kwenye uwezo wake wa kumudu anachotakiwa kujuwa.
Kama inakuwa kila mara ni yeye; hilo haliwezekani' labda hivyo vyuo vya jalalani.
 
Mitego mingi ya kumtia nyavuni, huyo muhuni
 
Ni kweli unachokisema lakini sio mtoto wangu wa kwanza kulalamika ni wanafunzi wa kike wa huyo mwalimu wengi wamepitia hayo masaibu na anajinasibu kuwa anatafta wake akiwa darasani
Basi hicho ni chuo kibovu kama haya usemayo ni kweli.

Chuo kisicho linda hadi ya taaluma yake; hiyo ni takataka.
Hivi ni vyuo wanavyosoma akina Samia..
 
Huyu mtoto wangu amepitia hii changamoto mwaka Jana mpaka mtoto akatoa pesa bila sisi kujua,

Bahati mbaya tena mwaka huu mwalimu alikuwa anawafundisha pia amempa supp na ameahidi hachomoi mpaka ampe mapenzi, na inasadikika ameungua wakuu msaada wenu
Stories za aina hii nazo ni za kuzisikiliza with an open mind. Sijawahi kusikia story kama hii kutoka kwa msichana mwenye uwezo mkubwa darasani.
 
Uwe mwangalifu sana na stori za vijiweni, na habari za huyo mwanao.

Hakuna 'chuo' chenye hadhi kinachoweza kutoa 'supp' bila ya maelezo ya msingi.
Ushahidi hauwezi kujificha; kama ni 'supp' ni supp' hata uende wapi!

Mwanao atakuwa na udhaifu kwenye uwezo wake wa kumudu anachotakiwa kujuwa.
Kama inakuwa kila mara ni yeye; hilo haliwezekani' labda hivyo vyuo vya jalalani.
Muache ujuaji kwa kila jambo, hivi mnadhani Chuo mmeenda pekee?, hakuna asiyejua haya mambo yapo vyuo vyote hapa nchini, mpaka hivyo top 5 vina huu upuuzi.

Nina ushahidi wa vyuo vikubwa mkoa fulani ndio michezo ya hao wapuuzi wanaoitwa wakufunzi, yaani serikali imewapa maamuzi makubwa ktk maisha ya watu kuliko uwezo wao wa kiakili.

Fanya research yako, kaa na wanafunzi wa vyuo ongea nao utazipata hizi habari au kama umepita chuo lazima utaelewa jambo hili, kubisha hili ni ushahidi kuwa hujui lolote kuhusu ushenzi unaendelea vyuoni maana hujafika chuo.

Narudia tena, hizi kenge zinazoitwa wakufunzi(lecturers) zimepewa maamuzi makubwa kuliko uhalisia, maamuzi yanayoaffect mamia ya wanafunzi wasio na hatia hasa wanawake, kuna kesi nyingi sana vyuoni ambazo zinatia aibu mfumo wa elimu ya hii nchi.

Anayetetea huu ushenzi ni either hajasoma hajui haya mambo au ni mmoja wa wanufaika wa huu unyanyasaji wa kingono huko mavyuoni.

Kuna ulazima wa kupitia upya background na afya ya akili kwa hawa wakufunzi kabla ya kupewa majukumu yanayoharibu maisha ya watoto wa watu.

Shame on you chawa
 
Back
Top Bottom