Ushauri wenu Wakuu, Wahadhiri wanaoomba rushwa ya ngono wamemfikia mtoto wangu

Ushauri wenu Wakuu, Wahadhiri wanaoomba rushwa ya ngono wamemfikia mtoto wangu

Mkuu, pole kwa matatizo.

Rushwa ya ngono ngumu sana kumkamata mtu redhanded, bora ata rushwa ya pesa.

Hapa kumuokoa mwanao ni kumuambia afanye appeal ya ilo somo lirudiwe kusahihishwa.

Appeal inafanyia kwenye department/school husika, na ilo somo litafanyiwa marking upya na walimu wengine, kwahiyo kama ameonewa atapass.

Pili, kwanini umesema semester iliyopita alitoa hela? Inamaana same mwalimu anawafundisha kila semester kama secondary au walimu tofauti tofauti wanamtaka dogo?

Tatu, omba account ya matokeo ya mwanao uingie uone. Kuna mdau kasema hapo usikute dogo amechukulia scapegoat.

Na mwisho, hakuna ushahidi wowote ambao dogo ameutunza kama vile msg, call record, etc ila kama ni wa maneno tu ngumu sana sana sana kushinda, ila kama by anymeans kuna ushaidi valia njuga nenda chuo husika kaonane na dean au HoD au ata mkuu wa taasisi ili swala mlisettle.

Pole sana, wengi humu tutajibu kwa hisia kwasababu hatuna watoto waliokutwa na iyo kitu.
Hii ya ku-appeal mkuu sina hata hamu nayo. Walimu wa department husika Huwa wanalindana ni ngumu kuchomoa hilo lilikuwa wazo langu la kwanza.
Mtoto semester ya mwaka Jana alisupp somo Moja tu. Na mwaka huu hii semester ni Moja tu na yote ni ya huyo mwalimu.
Vyuo vyetu hivi unakuta Kuna mwalimu semester ya kwanza anawafundisha somo Moja na semester nyingine kingine hii ni kawaida sana hasa vyuo vyetu hivi.
Ushaidi wa kumtia hatiani ndio tunautafta.
 
Naiona pesa nje nje,natamani huyo ndio angekuwa binti yangu yaani ningemuwekea mtego huyo bazazi domo zege,mtego ambao hajawahi kuuona kwenye hii dunia,na angelia kikwao maana pesa nitakayompiga baada ya fumanizi ili ailipe inabidi akope misharahara yake yote mpaka anastaafu na utamu asingekula angeishia kushika paja tu.Hizi bahati Kwa nini hazitukuti sisi
Mbona unapoteza muda wako na mhadhili fukara kama huyo.
Pesa ipo waziwazi, tena ndefu sana kila unapotazama muundo wa utawala wa Samia Suluhu Hassan.

Sahau maswala ya "uchawa"; hayo hayalipi tena siku hizi baada ya Samia kufanikiwa kunyakua uongozi kwa mabavu. Tazama vizuri humo ndani utapata sehemu ambayo itakupatia pesa haramu kama unayoililia wewe hapa.

Ni swala la kujuwa tu ni wapi pa kujipenyeza ili unufaike.
 
Mwambie amrekodi akiwa anaongea awapelekee pccb! Mimi nilikutana na huyo mshenzi pale saut, nilikuwa mjeuri nikacarry nikakomaa nikatoboa! Ilipotea test moja tu ndio sababu ya kurudia mtihani mwalimu anashindwa kureweka records, ukifika ofisini anakwambia we binti una shape hivi! Anaanza kukusogelea! Aisee na akijichanganya akalala naye ndio bye bye atamtumia mpaka achoke na hachomoi hiyo supp! Kuna dada alikaa miaka mi5 chuo!
Kama hayajakukuta unaweza ukadhani masikhara, mdogo wangu mpaka alihama chuo na akapoteza mwaka mzima sababu ya walimu kama hawa.

Nachukia sana haya mambo ya rushwa ya ngono!
 
Stories za aina hii nazo ni za kuzisikiliza with an open mind. Sijawahi kusikia story kama hii kutoka kwa msichana mwenye uwezo mkubwa darasani.
Mimi ninayo ya mdogo wangu, top of class UDOM, mwalimu alimbully kwamba atamfelisha na alimtorture mentally mpaka akahama chuo na kupoteza a whole year. Amemaliza degree yake ya kwanza miaka kadhaa iliyopita top of her class na moja kwa moja akapata scholarship ya postgraduate nje ya nchi.

Kuna upumbavu mkubwa sana binti akiwa hajirahisishi kwa walimu huko vyuoni!
 
Huyu mtoto wangu amepitia hii changamoto mwaka Jana mpaka mtoto akatoa pesa bila sisi kujua,

Bahati mbaya tena mwaka huu mwalimu alikuwa anawafundisha pia amempa supp na ameahidi hachomoi mpaka ampe mapenzi, na inasadikika ameungua wakuu msaada wenu
Jina la Lecturer, chuo, faculty namba yake ya simu tumtumie Waziri Gwajima
 
Mimi ninayo ya mdogo wangu, top of class UDOM, mwalimu alimbully kwamba atamfelisha na alimtorture mentally mpaka akahama chuo na kupoteza a whole year. Amemaliza degree yake ya kwanza miaka kadhaa iliyopita top of her class na moja kwa moja akapata scholarship ya postgraduate nje ya nchi.

Kuna upumbavu mkubwa sana binti akiwa hajirahisishi kwa walimu huko vyuoni!
Mkuu nakuelewa sana chuoni ukiwa na urafiki na wadada hata ue unaweza kupewa
 
Huyu mtoto wangu amepitia hii changamoto mwaka Jana mpaka mtoto akatoa pesa bila sisi kujua,

Bahati mbaya tena mwaka huu mwalimu alikuwa anawafundisha pia amempa supp na ameahidi hachomoi mpaka ampe mapenzi, na inasadikika ameungua wakuu msaada wenu
Amrekodi na kumshitaki kwa ushahidi wa kumrekodi akiomba rushwa.

Amshitaki mitandaoni mpaka TAKUKURU.

Bila ya hivyo atampitia yeye na wengine wengi tu.
 
Muache ujuaji kwa kila jambo, hivi mnadhani Chuo mmeenda pekee?, hakuna asiyejua haya mambo yapo vyuo vyote hapa nchini, mpaka hivyo top 5 vina huu upuuzi.
Wewe umejifungia ndani ya gunia, wakati mimi nikikueleza hali inavyopaswa kuwa kwenye taasisi yoyote ya huduma kama hiyo..

Unashindwa kujuwa tatizo linatoka wapi; utaweza vipi kutoa ushauri wa ufumbuzi.

Hizo top 5 unazozungumzia wewe, sijui unazipa u'top' tokana na nini; kutoa digrii za heshima hata kwa watu vihiyo?

Tatizo siyo hayo mavyuo na wahadhili wake; ni uozo ulionea katika kila sehemu ya taifa hili.

Samia mtu mwovu ataanzia wapi kuwa kielelezo cha mambo mazuri yatakayofanyika kwenye hivyo vyuo.

Unalalamikia mhadhiri, halafu unashindwa kumlalamikia anayewezesha hali hiyo kuwa mbovu.
 
Back
Top Bottom