Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Dar es salaam enzi hizo ikiwa kama mkoa ilijumuisha mkoa unaoitwa Pwani ukijumuisha Kisarawe na Kibaha. Huu utaratibu wa kuunda mikoa unaofuata ongezeko la watu na makazi ndio unaotugharimu na kupata mihemuko inayopelekea watu kuomba mikoa mipya iiundwe. Harakati za kutaka Chato kuwa mkoa ni mfano halisi ulio wazi kati ya mingi inayoendelea kimya kimya.

Kimsingi miundombinu inatakiwa kuwekwa kabla watu hawajaanza kugawiana viwanja kujenga na kuanza kazi muhimu ya kuzaliana. Ilitakiwa huko kwenye wizara za ardhi na makazi ambako kuna wataalamu wa mipangomiji watangulie kutoa ramani ya mpangomji kabambe kwa kila halmashauri ili kila eneo lifahamike liko kwa ajili gani iwe makazi, barabara, bustani au hata mkoa. Mambo mengi yanafanyika kwa kufuata matakwa ya wanasiasa na ndio wanaosikika zaidi na kuamua badala ya
wataalamu

Mfano mzuri ulioutoa wa safari ya kutoka kaskazini ya Dar es salaam kuelekea kusini ingeweza kufanyika kwa kupita Kisarawe bila kuzungukia Ubungo na Tazara. Kituko kingine ni upanuaji wa barabara ya Morogoro kipande cha Mbezi hadi Kibaha tena kwa njia nane!. Badala yake wangeijenga kwa njia nne, huku wakipasua barabara nyingine ya njia nne kuanzia Kibaha kwa Mathias kwenda hadi Kisarawe kuunganisha na Pugu road, Lakini pale Masaki kabla ya kufika Kazimzumbwi, barabara yake inayopita Chanika, Mvuti hadi Mbagala ingepanuliwa ili magari yanayoenda kusini yasilazimike kuingia Ubungo.

Kwa maoni yangu sioni faida ya kuendelea kugawanya nchi na kuongeza idadi ya mikoa, badala yake barabara na miundombinu ya kila mikoa ingejengwa kwa kiwango cha juu ili kusiwe na mshawasha wa kukimbilia mijini lakini muhimu zaidi kudhibiti ongezeko la watu. Watanzania naona wanafyatuana utafikiri wataadhibiwa kwa kutoijaza Dunia.
 
Kinondoni hii hasa A na Magomeni aliyekuwa mbunge wa kwanza Mr.DB(ila alikua ni mzungu mtanzania na rip)akifufuka leo na kutembelea Ile mitaa na muindo mbinu aliyoibuni na kuitekekeza vema Nina imani kabisa ataamua kurudi kaburini kuendelea kupumzika maana uchafu tulioufanya hatuwezi kuusahihisha.
 
... hiki ulichoeleza hapa ni sera ya majimbo ya Chadema.
Wewe sio msemaji wangu, ningetaka kuelezea hayo ningesema mwenyewe, sio kila mada tuijadili kisiasa, ujadili wangu ni kuhusiana na utitiri wa mikoa na services delivery kwa wananchi
 
Mitaa ya Kinondoni,magomeni,ilala ,mwananyamala na baadhi ya mitaa ya temeke ilikuwa na lami na taa za kumulika usiku mwema mpaka miaka ya mwanzoni80
 
Dah kweli kabisa mkuu,kipindi makamba mkuu wa mkoa DSM ilikuwa na watu wasiozidi mil 2 tunafyatua hasa.
Kuhu barabara ya kutoka kibaha kwenda kisarawe ni muhimu sana,
 
Mtoni kijichi pia ni Mbagala
 
Mto Mzinga hauwezi kuigawa Dar es Salaam.
Mto Kizinga unaishia pale Mtoni Msikitini na ukiufatilia unajua umetengenisha Mbagala kwa lingaya Jimbo la mbagala na Mtoni unguja huku temeke Unaenda Tena kupitia katikati ya Yombo halafu Unaenda kuitenganisha kati ya Mbagala Kilungule, Yombo Buza kwa Mpalange, inaendelea Tena kuitenganisha Chamazi saku na Kitunda Mwanagati, Unaenda Tena kuitenganisha Chamazi Dovya na Kivule , Unaenda kutokea Matembele mawili Kivule huko na Kutokea kitonga .

Mto Mzinga umepita huku Mbagala baada ya rangi tatu , nyuma nyuma umetengenisha Chamazi Mbande huku ni Jimbo la Mbagala upande wa pili mkuranga, Unaenda kuitenganisha Msongola, kitonga, Mvuti ambalo ni Jimbo la ukonga jijini Dar es Salaamupande wa pili wilaya ya mkuranga.
Hii ni ishara wewe ni wakuja Dar es Salaam na umekuja na gari la Ndizi, la Mkaa, Mbio za Mwenge au kwa shemeji.
 
Mbagala ni kata tu ila inazidi Singida mjini kwa idadi ya watu na mishemishe
Halafu Mbagala sio kata ilikuwa tarafa na Sasa ni Jimbo la uchaguzi.
Kata ya Chamazi Ina wakazi wengi zaidi kuliko kata yoyote Yaa jiji la Dar es salaam
 
Ahaaaa,kiukweli kuhusu huo mto ulivyoulezea we noma.mi mjini kitambo ila mbagala naweza kata miaka kumi sijaja,mara ya mwisho nilienda chamazi kule Uvikiuta kumsalimia mzee mwenzangu jordan.w e niulize habari za magomeni tangu enzi za mwalimu
 
Halafu Mbagala sio kata ilikuwa tarafa na Sasa ni Jimbo la uchaguzi.
Kata ya Chamazi Ina wakazi wengi zaidi kuliko kata yoyote Yaa jiji la Dar es salaam
Kule kuna watu wengi sana,
 
Mawazo yangu ndugu kwa nini tusianzishe Metropolis sijui kama nimeandika sawasawa

Kwamba Dar es Salaam Metropolis sijui Metropolicies itahusisha na kuchukua maeneo yafuatayo:

Wilaya yote ya Mkuranga na bandari ndogo ya kisiju pwani.
Kwa nini tayari mkuranga inapakana na wilaya tatu za jiji la Dar es Salaam kuanzia Kigamboni, Temeke na Ila


Na ndio sehemu inayofuatia kujengwa zaidi baada ya Kigamboni na
Kuna daladala za kutoka Kisemvule mpaka Kariakoo na ukumbuke Kisenvule mpaka mkuranga mjini karibu mno hapazidi hata kilomita 10.

Wilaya ya kibaha yote, kila mtu anashuhudia maendeleo ya kibaha mjini pale

Wilaya ya Bagamoyo yote

Wilaya ya kisarawe yote ila liwe jiji lenye Mbuga ya wanyama karibu

Wilaya ya Mafia

Kuandaliwe miundombinu yote , huduma za kijamii

Idadi ya watu inazidi kuongezeka Tanzania na watu wataendelea kujenga.

Waanze plan ya kuziunganisha miji tajwa hapo juu na Usafiri wa reli za kisasa, Utanuzi wa Barabara.
Na Dar es Salaam kuwe na Mamlaka ya Metropolitan.
 
Ahaaaa,kiukweli kuhusu huo mto ulivyoulezea we noma.mi mjini kitambo ila mbagala naweza kata miaka kumi sijaja,mara ya mwisho nilienda chamazi kule Uvikiuta kumsalimia mzee mwenzangu jordan.w e niulize habari za magomeni tangu enzi za mwalimu
Upo sahihi ila ubaya wa Dar es Salaam ni Miundombinu

UVIKIUTA hata Barabara ya Kitunda Kivule Banana ingepigwa rami bado ungefika kwa sababu UVIKIUTA inaanzia Chamazi mpaka Kivule.

Wandengereko na Wazaramo hawakukosea kuita Kizinga na Mzinga
 
Uko sahihi mkuu hizi wilaya ziunganishwe kuizunguka Dar es salaam. fikiria mtu wa rufiji eti akiumwa rufaa anaambiwa aende tumbi hospitali ya mkoa,njiani anapita hospitali zenye hadhi kubwa au sawa na tumbi,maana amana,temeke na mwananyamala zina hadhi ya mkoa,unafika tumbi unakufa maiti inarudishwa tena rufiji kuzika
 
Utagundua kutoka city center Dar es salaam kwenda maeneo tajwa Karibu ni Kisarawe mjini halafu inafuatwa Mkuranga.

Kuna umuhimu wa kuanzisha Metropolis Dar es salaam kwa sababu inakwenda kufikisha idadi ya wakazi wake Milioni kumi ila miundombinu inaiangusha.
 
Hata mimi nasapoti dsm ipanuliwe.sasa ili ipanuliwe lazima sehemu ya pwani imegwe kuja Dar.Yakitokea hayo, Kuna watu watalalamika as usual.sasa kuepusha mengi PWANI YOTE iwe DAR, iletwe kama ilivyo na wilaya na majimbo yake, wakazi wa pwani hawatanung'unika coz hata kwao itakuwa ni PROMOTION..hii habari eti nipe kibaha nikuachie kigamboni ni ngumu kuelewana...Bahati mbaya; Rais wa sasa hana hulka ya kufanya shocking decisions! hili tusahau kutokea..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…