Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Dar es salaam enzi hizo ikiwa kama mkoa ilijumuisha mkoa unaoitwa Pwani ukijumuisha Kisarawe na Kibaha. Huu utaratibu wa kuunda mikoa unaofuata ongezeko la watu na makazi ndio unaotugharimu na kupata mihemuko inayopelekea watu kuomba mikoa mipya iiundwe. Harakati za kutaka Chato kuwa mkoa ni mfano halisi ulio wazi kati ya mingi inayoendelea kimya kimya.

Kimsingi miundombinu inatakiwa kuwekwa kabla watu hawajaanza kugawiana viwanja kujenga na kuanza kazi muhimu ya kuzaliana. Ilitakiwa huko kwenye wizara za ardhi na makazi ambako kuna wataalamu wa mipangomiji watangulie kutoa ramani ya mpangomji kabambe kwa kila halmashauri ili kila eneo lifahamike liko kwa ajili gani iwe makazi, barabara, bustani au hata mkoa. Mambo mengi yanafanyika kwa kufuata matakwa ya wanasiasa na ndio wanaosikika zaidi na kuamua badala ya
wataalamu

Mfano mzuri ulioutoa wa safari ya kutoka kaskazini ya Dar es salaam kuelekea kusini ingeweza kufanyika kwa kupita Kisarawe bila kuzungukia Ubungo na Tazara. Kituko kingine ni upanuaji wa barabara ya Morogoro kipande cha Mbezi hadi Kibaha tena kwa njia nane!. Badala yake wangeijenga kwa njia nne, huku wakipasua barabara nyingine ya njia nne kuanzia Kibaha kwa Mathias kwenda hadi Kisarawe kuunganisha na Pugu road, Lakini pale Masaki kabla ya kufika Kazimzumbwi, barabara yake inayopita Chanika, Mvuti hadi Mbagala ingepanuliwa ili magari yanayoenda kusini yasilazimike kuingia Ubungo.

Kwa maoni yangu sioni faida ya kuendelea kugawanya nchi na kuongeza idadi ya mikoa, badala yake barabara na miundombinu ya kila mikoa ingejengwa kwa kiwango cha juu ili kusiwe na mshawasha wa kukimbilia mijini lakini muhimu zaidi kudhibiti ongezeko la watu. Watanzania naona wanafyatuana utafikiri wataadhibiwa kwa kutoijaza Dunia.
 
Mwingireza alikuwa na Mikoa michache,na aliweza kujenga mpaka nyumba za vigae huko pembezoni mwa nchi hii.

Tukumbuke nchi ilikuwa haina miundo mbinu kama sasa,kwa jinsi watawala wa sasa wanawaza kuongeza wilaya na mikoa?! Badala ya kuimarisha usimamizi wanafikiria maeneo kisiasa,hivyo nchi kuendelea kuwa maskini,maeneo kutopimwa na kukosa mpangilio!!!

Swali gumu ambalo viongozi wetu hawataki kufikiri,kujiuliza wala kutafuta ufumbuzi(miji kama New york,tokyo na mingine ina watu zaidi ya milioni 18,Lakini ipo kwa mpangilio).huku kwetu Viongozi kupangilia miji sio kipaumbele!!!,wanawaza kuongeza maeneo ya utawala ili kujitengenezea nafasi za kimadaraka na siasa bila kujali hali ya baadae ya jamii.
Kinondoni hii hasa A na Magomeni aliyekuwa mbunge wa kwanza Mr.DB(ila alikua ni mzungu mtanzania na rip)akifufuka leo na kutembelea Ile mitaa na muindo mbinu aliyoibuni na kuitekekeza vema Nina imani kabisa ataamua kurudi kaburini kuendelea kupumzika maana uchafu tulioufanya hatuwezi kuusahihisha.
 
Mitaa ya Kinondoni,magomeni,ilala ,mwananyamala na baadhi ya mitaa ya temeke ilikuwa na lami na taa za kumulika usiku mwema mpaka miaka ya mwanzoni80
 
Dar es salaam enzi hizo ikiwa kama mkoa ilijumuisha mkoa unaoitwa Pwani ukijumuisha Kisarawe na Kibaha. Huu utaratibu wa kuunda mikoa unaofuata ongezeko la watu na makazi ndio unaotugharimu na kupata mihemuko inayopelekea watu kuomba mikoa mipya iiundwe. Harakati za kutaka Chato kuwa mkoa ni mfano halisi ulio wazi kati ya mingi inayoendelea kimya kimya.

Kimsingi miundombinu inatakiwa kuwekwa kabla watu hawajaanza kugawiana viwanja kujenga na kuanza kazi muhimu ya kuzaliana. Ilitakiwa huko kwenye ya wizara za ardhi ambapo kuna wataalamu wa mipangomiji watangulie kutoa ramani ya mpangomji kabambe kwa kila halmashauri ili kila eneo lifahamike liko kwa ajili gani iwe makazi, barabara, bustani au hata mkoa. Mambo mengi yanafanyika kwa kufuata matakwa ya wanasiasa na ndio wanaosikika zaidi na kuamua badala ya
wataalamu

Mfano mzuri ulioutoa wa safari ya kutoka kaskazini ya Dar es salaam kuelekea kusini ingeweza kufanyika kwa kupita Kisarawe bila kuzungukia Ubungo na Tazara. Kituko kingine ni upanuaji wa barabara ya Morogoro kipande cha Mbezi hadi Kibaha tena kwa njia nane!. Badala yake wangeijenga kwa njia nne, huku wakipasua barabara nyingine ya njia nne kuanzia Kibaha kwa Mathias kwenda hadi Kisarawe kuunganisha na Pugu road, Lakini pale Masaki kabla ya kufika Kazimzumbwi, barabara yake inayopita Chanika, Mvuti hadi Mbagala ingepanuliwa ili magari yanayoenda kusini yasilazimike kuingia Ubungo.

Kwa maoni yangu sioni faida ya kuendelea kugawanya nchi na kuongeza idadi ya mikoa, badala yake barabara na miundombinu ya kila mikoa ingejengwa kwa kiwango cha juu ili kusiwe na mshawasha wa kukimbilia mijini lakini muhimu zaidi kudhibiti ongezeko la watu. Watanzania naona wanafyatuana utafikiri wataadhibiwa kwa kutoijaza Dunia.
Dah kweli kabisa mkuu,kipindi makamba mkuu wa mkoa DSM ilikuwa na watu wasiozidi mil 2 tunafyatua hasa.
Kuhu barabara ya kutoka kibaha kwenda kisarawe ni muhimu sana,
 
[emoji38][emoji38][emoji38] mkuu geographia yako bado haijakaa sawa

Unapoepeleka kigamboni Pwani ni makosaa
Iyo kigamboni unayoisema iende pwani ni kigambon hii hii au ipo nyingine ?

Kigamboni hihii ya ferry mpaka kibada pale kuna short cut ya kutokea Kijichi mtoni, ambako ni DSM

Suluhisho hapa ni kuanzisha mkoa mpyaaa utakaojumuisha wilaya za rufiji, mkuranga , kibiti, mafia hapo ndipo binafsi naona ni solution ila sio.kuichukua kigamboni kuipeleka pwani
Mtoni kijichi pia ni Mbagala
 
Kipindi nakua mji ulikuwa mwisho ubungo, pale lilipo jengo la Tanesco ndio ulikuwa mzani wa kupima malori ambao sasa uko mkoa wa Pwani, Dar inakuwa kuelekea kaskazini,npaka wa Dar na kibaha ubafutika, mpaka wa Dar, Bagamoyo unafutika kwa kasi sababu ya ujenzi unaokuwa kwa kasi ya ajabu.

Jiografia ya mkoa wa Pwani inashangaza sana, mtu wa Bagamoyo akitaka kwenda Rufijii au mafia lazima apitie Dar au apande chombo cha baharini. Ushauri wangu hizi wilaya mbili zije Dar, ili kubalance mapato na uchumi Kigamboni na Mbagala yote iende Pwani,waungane na Mkuranga,Kisarawe, Mafia na Rufiji

Faida zake:

Jiji la Dar eS Salaam litapumua kwa kupata ardhi ya kutosha na kukua kwa kasi ya ajabu kibaha itakuwa kama urusi kwa technology na Bagamoyo zitakuwa kama ukraine kwa utalii, pata oicha chalinze ni sehemu ya Dar es Salaam.

Tuje Pwani sasa.

Pwani kwa kupewa Kigamboni na Mbagala itachangamka sana, tatizo la Pwani ni kikosa amsha amsha. Mbagala itakuwa Dubai mpya kwa biashara mpaka sasa Mbagala inazidi baadhi ya mikoa kwa idadi ya watu na amsha amsha ya kibiashara pata picha Mbagala iko Pwani na Kigamboni itakuwa Paris au Spain sehemu za kula bata kwenye fukwe.

Mto mzinga utenganishe dar na Pwani
Wakazi wengi wa Mbagala wana asili ya Pwani au Kusini mwa Tanzania, warudisheni nyumbani kwa style nyingine.
Chawa wa mama mfikishieni hii
Mto Mzinga hauwezi kuigawa Dar es Salaam.
Mto Kizinga unaishia pale Mtoni Msikitini na ukiufatilia unajua umetengenisha Mbagala kwa lingaya Jimbo la mbagala na Mtoni unguja huku temeke Unaenda Tena kupitia katikati ya Yombo halafu Unaenda kuitenganisha kati ya Mbagala Kilungule, Yombo Buza kwa Mpalange, inaendelea Tena kuitenganisha Chamazi saku na Kitunda Mwanagati, Unaenda Tena kuitenganisha Chamazi Dovya na Kivule , Unaenda kutokea Matembele mawili Kivule huko na Kutokea kitonga .

Mto Mzinga umepita huku Mbagala baada ya rangi tatu , nyuma nyuma umetengenisha Chamazi Mbande huku ni Jimbo la Mbagala upande wa pili mkuranga, Unaenda kuitenganisha Msongola, kitonga, Mvuti ambalo ni Jimbo la ukonga jijini Dar es Salaamupande wa pili wilaya ya mkuranga.
Hii ni ishara wewe ni wakuja Dar es Salaam na umekuja na gari la Ndizi, la Mkaa, Mbio za Mwenge au kwa shemeji.
 
Mbagala ni kata tu ila inazidi Singida mjini kwa idadi ya watu na mishemishe
Halafu Mbagala sio kata ilikuwa tarafa na Sasa ni Jimbo la uchaguzi.
Kata ya Chamazi Ina wakazi wengi zaidi kuliko kata yoyote Yaa jiji la Dar es salaam
 
Ahaaaa,kiukweli kuhusu huo mto ulivyoulezea we noma.mi mjini kitambo ila mbagala naweza kata miaka kumi sijaja,mara ya mwisho nilienda chamazi kule Uvikiuta kumsalimia mzee mwenzangu jordan.w e niulize habari za magomeni tangu enzi za mwalimu
 
Halafu Mbagala sio kata ilikuwa tarafa na Sasa ni Jimbo la uchaguzi.
Kata ya Chamazi Ina wakazi wengi zaidi kuliko kata yoyote Yaa jiji la Dar es salaam
Kule kuna watu wengi sana,
 
Mawazo yangu ndugu kwa nini tusianzishe Metropolis sijui kama nimeandika sawasawa

Kwamba Dar es Salaam Metropolis sijui Metropolicies itahusisha na kuchukua maeneo yafuatayo:

Wilaya yote ya Mkuranga na bandari ndogo ya kisiju pwani.
Kwa nini tayari mkuranga inapakana na wilaya tatu za jiji la Dar es Salaam kuanzia Kigamboni, Temeke na Ila

Na ndio sehemu inayofuatia kujengwa zaidi baada ya Kigamboni na
Kuna daladala za kutoka Kisemvule mpaka Kariakoo na ukumbuke Kisenvule mpaka mkuranga mjini karibu mno hapazidi hata kilomita 10.

Wilaya ya kibaha yote, kila mtu anashuhudia maendeleo ya kibaha mjini pale

Wilaya ya Bagamoyo yote

Wilaya ya kisarawe yote ila liwe jiji lenye Mbuga ya wanyama karibu

Wilaya ya Mafia

Kuandaliwe miundombinu yote , huduma za kijamii

Idadi ya watu inazidi kuongezeka Tanzania na watu wataendelea kujenga.

Waanze plan ya kuziunganisha miji tajwa hapo juu na Usafiri wa reli za kisasa, Utanuzi wa Barabara.
Na Dar es Salaam kuwe na Mamlaka ya Metropolitan.
 
Ahaaaa,kiukweli kuhusu huo mto ulivyoulezea we noma.mi mjini kitambo ila mbagala naweza kata miaka kumi sijaja,mara ya mwisho nilienda chamazi kule Uvikiuta kumsalimia mzee mwenzangu jordan.w e niulize habari za magomeni tangu enzi za mwalimu
Upo sahihi ila ubaya wa Dar es Salaam ni Miundombinu

UVIKIUTA hata Barabara ya Kitunda Kivule Banana ingepigwa rami bado ungefika kwa sababu UVIKIUTA inaanzia Chamazi mpaka Kivule.

Wandengereko na Wazaramo hawakukosea kuita Kizinga na Mzinga
 
Mawazo yangu ndugu kwa nini tusianzishe Metropolis sijui kama nimeandika sawasawa

Kwamba Dar es Salaam Metropolis sijui Metropolicies itahusisha na kuchukua maeneo yafuatayo:

Wilaya yote ya Mkuranga na bandari ndogo ya kisiju pwani.
Kwa nini tayari mkuranga inapakana na wilaya tatu za jiji la Dar es Salaam kuanzia Kigamboni, Temeke na Ila

Na ndio sehemu inayofuatia kujengwa zaidi baada ya Kigamboni na
Kuna daladala za kutoka Kisemvule mpaka Kariakoo na ukumbuke Kisenvule mpaka mkuranga mjini karibu mno hapazidi hata kilomita 10.

Wilaya ya kibaha yote, kila mtu anashuhudia maendeleo ya kibaha mjini pale

Wilaya ya Bagamoyo yote

Wilaya ya kisarawe yote ila liwe jiji lenye Mbuga ya wanyama karibu

Wilaya ya Mafia

Kuandaliwe miundombinu yote , huduma za kijamii

Idadi ya watu inazidi kuongezeka Tanzania na watu wataendelea kujenga.

Waanze plan ya kuziunganisha miji tajwa hapo juu na Usafiri wa reli za kisasa, Utanuzi wa Barabara.
Na Dar es Salaam kuwe na Mamlaka ya Metropolitan.
Uko sahihi mkuu hizi wilaya ziunganishwe kuizunguka Dar es salaam. fikiria mtu wa rufiji eti akiumwa rufaa anaambiwa aende tumbi hospitali ya mkoa,njiani anapita hospitali zenye hadhi kubwa au sawa na tumbi,maana amana,temeke na mwananyamala zina hadhi ya mkoa,unafika tumbi unakufa maiti inarudishwa tena rufiji kuzika
 
Utagundua kutoka city center Dar es salaam kwenda maeneo tajwa Karibu ni Kisarawe mjini halafu inafuatwa Mkuranga.

Kuna umuhimu wa kuanzisha Metropolis Dar es salaam kwa sababu inakwenda kufikisha idadi ya wakazi wake Milioni kumi ila miundombinu inaiangusha.
Screenshot_20220226-220459.jpg
Screenshot_20220226-220558.jpg
Screenshot_20220226-220528.jpg
Screenshot_20220226-220643.jpg
 
Hata mimi nasapoti dsm ipanuliwe.sasa ili ipanuliwe lazima sehemu ya pwani imegwe kuja Dar.Yakitokea hayo, Kuna watu watalalamika as usual.sasa kuepusha mengi PWANI YOTE iwe DAR, iletwe kama ilivyo na wilaya na majimbo yake, wakazi wa pwani hawatanung'unika coz hata kwao itakuwa ni PROMOTION..hii habari eti nipe kibaha nikuachie kigamboni ni ngumu kuelewana...Bahati mbaya; Rais wa sasa hana hulka ya kufanya shocking decisions! hili tusahau kutokea..
 
Back
Top Bottom