Dar es salaam enzi hizo ikiwa kama mkoa ilijumuisha mkoa unaoitwa Pwani ukijumuisha Kisarawe na Kibaha. Huu utaratibu wa kuunda mikoa unaofuata ongezeko la watu na makazi ndio unaotugharimu na kupata mihemuko inayopelekea watu kuomba mikoa mipya iiundwe. Harakati za kutaka Chato kuwa mkoa ni mfano halisi ulio wazi kati ya mingi inayoendelea kimya kimya.
Kimsingi miundombinu inatakiwa kuwekwa kabla watu hawajaanza kugawiana viwanja kujenga na kuanza kazi muhimu ya kuzaliana. Ilitakiwa huko kwenye wizara za ardhi na makazi ambako kuna wataalamu wa mipangomiji watangulie kutoa ramani ya mpangomji kabambe kwa kila halmashauri ili kila eneo lifahamike liko kwa ajili gani iwe makazi, barabara, bustani au hata mkoa. Mambo mengi yanafanyika kwa kufuata matakwa ya wanasiasa na ndio wanaosikika zaidi na kuamua badala ya
wataalamu
Mfano mzuri ulioutoa wa safari ya kutoka kaskazini ya Dar es salaam kuelekea kusini ingeweza kufanyika kwa kupita Kisarawe bila kuzungukia Ubungo na Tazara. Kituko kingine ni upanuaji wa barabara ya Morogoro kipande cha Mbezi hadi Kibaha tena kwa njia nane!. Badala yake wangeijenga kwa njia nne, huku wakipasua barabara nyingine ya njia nne kuanzia Kibaha kwa Mathias kwenda hadi Kisarawe kuunganisha na Pugu road, Lakini pale Masaki kabla ya kufika Kazimzumbwi, barabara yake inayopita Chanika, Mvuti hadi Mbagala ingepanuliwa ili magari yanayoenda kusini yasilazimike kuingia Ubungo.
Kwa maoni yangu sioni faida ya kuendelea kugawanya nchi na kuongeza idadi ya mikoa, badala yake barabara na miundombinu ya kila mikoa ingejengwa kwa kiwango cha juu ili kusiwe na mshawasha wa kukimbilia mijini lakini muhimu zaidi kudhibiti ongezeko la watu. Watanzania naona wanafyatuana utafikiri wataadhibiwa kwa kutoijaza Dunia.