Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Mama hili haliwezi,miradi ya JPM inamtesa,akizubaa atamaliza mihula miwili bila kumaliza hiyo miradi kukamilka sijui atasingizia nini
 
Unazungumzia mto Mzinga au Kizinga?
Mto mzinga upo kule Mbagala Kokoto kama unaenda Kongowe, yet unasema Mbagala ihamie mkoa wa Pwani. Kama unazungumzia mto uliopo pale Mission/mtongani (panaitwa msikitini) kwa chini, hapo upo sahihi.

Wazo lako ni zuri, lakini umeisahau wilaya ya Kisarawe. Iende wapi? Pwani au Dar hiyo unayoipropose?
 
Kwa CCM hii hii [emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umepangilia vizuri hoja yako na unaijua jiografia vizuri. Hoja ya kudhibiti ongezeko la watu hapa si mahala pake. By the way tuna mapori mengi sana hatuyafanyii chochote Tanzania haina dalili ya over population.
Nchi yetu ya Tanzania suffers from different challenges, but overpopulation is not one of them. This country has a land area larger than California, Michigan, Arizona, and Virginia combined, lakini idadi ya watu ni sawa na size of California's and Virginia's combined.

In a nutshell, data zipo pia.
 
Nilimaanisha ule mto karibu na mission,Kisarawe nayo yafaa iwe mkoa wa Dar Es salaam
 
Ukitaka kujua hii nchi ni mapori matupu panda treni ya kati kutoka dar kwenda kigoma,kuna ardhi haijawahi kuguswa mahekari kwa mahekari
 
Mkuu, katika kuliweka hili sawa, nadhani wakati mwingine estimates za population hazifanywi kwa kutazama na ukubwa wa eneo pekee. (Idadi ya watu dhidi ya ukubwa wa eneo).

Pia hufanywa kwa kuwianisha idadi ya watu na rasilimali wezeshi zilizopo katika eneo husika (huduma za msingi katika eneo husika kama vile maji, barabara, n.k).

Nimekumbusha hili ili kutoingia kwenye mtego wa kusema "Jangwani Sahara au Kalahari kuko underpopulated maana eneo ni kubwa sana lakini watu ni wachache."

Au kwa case ya NGORONGORO crater, kama inavyozungumzwa ikiwa ndivyo, then kule kuko overpopulated au kuko katika tishio la kuwa hivyo hata kama population density yake ni ndogo mno ukilinganisha na maeneo kama ILALA kwa mfano.
 
Hii nchi ina shida katika utawala, hasa decision makers. Wanagawa mikoa tu daily, kuna tija gani? Labda tujiulize, wangapi leo hii wanaenda ofisi ya mkoa? Kufata nini?
Je, hicho wanachokifata hawawezi kukipata hapo walipo?
Eti mwalimu anaenda mkoani anatoka Rufiji au Mafia mpaka Kibaha maili 1 kupeleka barua ya kuomba uhamisho kwa afisa elimu mkoa. Wakati tunaishi dunia yenye email na simu.

Hatuhitaji mikoa mingi. Tunahitaji utoaji huduma ulio bora katika mikoa michache tu. Hilo lingepangiliwa pamoja na mipango miji, serikali ingeweza kuhudumia population yote ijayo.
 
Kuna kipindi huu ushauri ungepokelewa bila tashwishwi ila zingehamishiwa Chato🐒
 
Mama hili haliwezi,miradi ya JPM inamtesa,akizubaa atamaliza mihula miwili bila kumaliza hiyo miradi kukamilka sijui atasingizia nini

Kwa hiyo Mama amalizie Chato Airport na Chato Mkoa.....
 
Miaka kidogo niliwaza hili!!
lakini natofautiana naww kidogo hapo!!…

Niliwaza kadili mji unavokua BAGAMOYO iingizwe dar es salaam
Kabisa mkuu tena bagamoyo ingechangamka sana
 
Iv mtu wa Rufiji , Kibiti , Mkuranga, Bagamoyo na Chalinze wakiwa na shida ofisi ya Mkuu wa Mkoa wanaenda wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…