Ni jambo lililo wazi kuwa Shirikisho ni mashindano yasiyo na hadhi sawa kulingana na Champions League na hata AFL, sasa sijui huu mjadala unahusu nini hasa. Kuna mtu anapinga hilo?
Simba bado anashiriki mashindano ya Kimataifa, ikiwemo AFL ambapo mpaka dakika hii Yanga hana uhakika wa kujumuishwa wakati Simba tayari imo. Katika rank za CAF, Simba bado imeiacha Yanga. Kuna anayepinga haya?
Saido alipohamia Simba kutoka Geita, magoli yake yaliendelea kuhesabika alipokuwa anagombania ufungaji bora.
Kwenda Shirikisho ni jambo jema kwa Simba kwa sasa kama nilivyosema katika uzi ule nwingine iwapo itajipanga vizuri.