Hii mambo iliwah nitokea nimetoka chuo na piga kaz na fundi mtaani.
Tuko na fundi mtaan tunapiga kaz kwenye nyumba ya mshua mmoja hv wa mambo ya ujenzi.
Asubuhi hiyo nagonga nyundo sana juu ya dari, fundi mkuu yuko chini na mama mwenye nyumba wanaongea kwa kilugha huku mimi nasikia baadhi ya maongezi yao kuwa "mwangalie fundi wako huko juu asije akaniunguzia nyumba yangu" na fundi akamjibu "haina shida ntaenda kuangalia",
Nilijisikia vibaya kwani kaz ninaijua vizur tu, pia fundi ananikubali kwenye kaz zenye utata lkn huyu mama alinidhalau sana na umbo langu dogo.
Kazi iliisha tukatimua na fundi wangu na ujira wetu mkononi, fundi mkuu alinieleza tulipo toka kuwa yule mama hakuamini kabsa kwenye kazi nikamjibu nilisikia alichoongea nikiwa juu.
Jion sasa yule mama alimwakia fundi kuwa kijana wako kaharibu kule juu anataka kumwunguzia nyumba yake, fundi mkuu akamwahidi kesho atakuja kurekebisha mwenye mama wa watu akapoa. Fundi alinipigia na kunijulisha hiyo inshu na tukakubaliana kwenda kesho.
Siku iliyofuata asb kama kawaida tukakutana fundi, ila fundi siku hiyo mtoto wake alikuwa mgonja hivyo alikuwa anafanya maandalizi ya kumpeleka hospital mtoto wake na hivyo mm kwenda eneo la tukio ila fundi aliniambia nimpe matumaini kuwa atakuja si muda kukangua kazi.
Nimefika site mama wa watu ananiangalia hovyohovyo tu, fundi yuko wapi? Yuko njian atakuja.
Nikaingia mzigoni sasa wala hata sikupanda juu ya dari yaani ni palepale kwenye main switch mchezo ukaisha , namwambia angalia vitu vyako vinafanya kazi? Akajibu ndio. Nikajua imemkaba hiyo na dhalau zke akidhani palipoharibika ni juu ya dari nipokuwa nagongagonga.
Nikawa zangu pale nje namsubili fundi aje maana hatukuwa na mawasiliano ya simu mpaka alipofika akamweleza nn kutokufika kwa wakat kwa kilugha, hao tukaendelea na shughuli zetu.
Nikamwacha anashangaa tu màana na fundi hakuangaika kukagua !