Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Jamani Mimi Nina mwili mdogo halafu ni mfupi dharau ninazopitia duniani hapa huwa naishia kucheka.siku moja naenda kazini niko kituoni daladala inakuja ile naanza kuingia konda akanisukuma akasema kwa sauti sipakii mwanafunzi.nikambembeleza akanipakia nikatoa 200 na miaka yangu 30
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji86][emoji86]pole mkuu
 
Naona simulizi nyingi za magari,wadada,hotel ,ATM nk chukueni hii ya kijijini!
Mwishoni mwa miaka ya 90' nikiwa mwanafunzi Udsm,nilienda likizo!
Nyumbani tunapakana na Taasisi moja ya Elimu ya Kati!
Jioni moja niliwatoa ng'ombe wakulima,wapate majani embeni mwa bara2 ili kesho wawe fit shambani!
Nilikuwa nilienda nyumbani navaa kinyumbani,jinsi iliyochoka kidogo,makata mbuga,mgolole wa kimasai ,fimbo ,kisu kitefu kiunoni, nkachukua Radio enzi nzile Rising Kama mkulima ( aisee RIP baba)
Basi wakapita wanachuo wakasikia nasikiliza kipindi Cha Mjadala Dw Saa 12 Jioni enzi Immune Kher na Othman Miraj mjadala ilikuwa Miaka Kumi baada ya Anguko la Ujamaa Afrika ipo Wapi!
Jamaa kuona Mara Ile wakaona huyu Mlugaluga hata haelewi kinachoadiliw!
Wakaanza kubwabwaja kwa Kingereza kibovu kuwa.. zisi poor,peasant is just deceiving himself listening to International radio,ili wapate muda wa kunisema walisogea wakiniambia nisiingize ng'ombe eneo la Chuo nikawajibu kuwa naijua mipaka!
Siku mbili baadaye kulikuwa na debate pale Chuoni kuhusu ,Demokrasia ya kiliberali na Mustakabali wa Nchi zilizokuwa za Kijamaa...kwa kuzingatia Azimio la Arusha! ...Walikuwa na Mwalimu mwenye upeo mkubwa Sana!
Basi yule Mwalimu kwa kutambua Moto wangu yangu Primary,Sekondary alinialika niwe mchokoza mada!
Nilienda nimevaa makatambuka vilevile na mojawapo ya yule aliyekuwa ananizidoa na ng"ombe wangu kumbe Ni Kiongozi wa Wanachuo na alikuwa Hightable!
Kimsingi walijuta kunifahamu!
[emoji23] [emoji23] safi mkuu dawa dawani tu
 
Wanaume mnaolalamika wanawake wanawadharau, sasa, kama umevaa na kukaa hovyo unategemea nini?
Mbona hamshobokei wanawake walio hovyo kama ni kweli hamtilii maanani outward appearance? Mjitafakari
Kingine, inaonekana tunashida kubwa kwenye maadili yetu. Kwanini tunaambizana ya kuwa tunatakiwa tuheshimu watu wote kwasababu anaweza kuwa na kazi nzuri au unaweza kupata shida akakusaidia nk? Kwanini tusifundishane kuheshimiana kwa upendo kutoka moyoni kuliko kutishana? Hi ndio sababu tunakua wanafiki na chini kwa chini tunachukiana.
Mimi binafsi uwe muokota machupa jalalani au meneja wa wapi, nita watreat sawa bila kujali chochote. Ndio maana kwa watu wenye position kubwa au wanaotegemea special treatment kutoka kwangu wananiona nina dharau, ili hali wale watu wanadharaulika na jamii wananiona sina shida yeyote.
Kuhusu kudharaulika kwasababu ya muonekano wa nje, sijawahi. Sana sana watu wakiniona matarajio yao yanazidi hata uhalisia wangu. Lakini watu wengi, hasa wanaume wananiona nipo shallow kichwani (sexism). Wanahisi siwezi kufanya maamuzi magumu, kuchanganua mambo, kutetea hoja au kuwa na skills kwenye male-dominant fields. Wanahisi nipo kama pambo na nikiwaprove wrong kuna wanaofurahi na kuna wanaonichukia na kunipiga vitu kwa nguvu zao zote.
Faida za kumheshimu kila mtu ni nyingi kuliko hasara.
 
Kuwa smart ni kama kipawa mkuu si kila mtu anazaliwa nacho. Kuna mwingine hana kitu lakini mara zote kapendeza.
Mwingine ana pesa & etc lakini kupendeza hajui. Yaani design ya wale wagumu wasiojali kuhusu yao.
Nina jamaa yangu toka shule yeye akipata tu sent anawaza akanunue nguo, saa etc. Muda huo me nikipata sent nawaza nikawanunulie pumba kuku wangu😂
Hahahah sawa Mr.Kuku
 
Kuna siku nipo nilikuwa sina kazi nyingi ofisini nikatoka nje hivi nikamweleza PA wangu nipo nje nachukua Juice Fresh kutoka nje kuna gari limeingia Parking kwa speed kidogo liniingie miguuni jamaa hawakuwa na hekima walinitusi Mpuuzi wewe...nimerudi Ofisini naambiwa na PA wangu Meneja kuna wageni wako nikawaruhusu waingie nakuta wale jamaa walionitusi nikawakaribisha na sentensi fupi 'Karibu ABSA' wanageuzageuza nyuso zao hawajui waanze vipi.
 
Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka.

Sasa ile natoka nje nikazikuta ziko bize zinajisnap kwenye gari niliyokua nayo, hiiiiiiiiii bagoshaaa, mbona walikoma kunijua.

Nilianzisha zogo la maana makusudi kabisa, nikaita mpaka uongozi wa pale nikawaambia wawaambie wateja wao wafute picha zote walizopiga gari yangu otherwise niite Askari pale obey waniambie Wana lengo gani na picha za mkwaju wangu?
Uzi huu haujautendea haki maana gari ulilokuwa nalo lilikuwa la kuazima.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
We kaka upo dark ages au?
Umenichekesha mnooo. Sasa mtu kama wewe hatuwezi kulingana kwasababu nimekuzidi kwa kila kitu.
Na kama unataka kuniaminisha kuwa uanamke ni udhaifu, kanye ulale.
Eti mtu mzima una kuja hapa na hoja za vikojoleo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mwanamke utabaki kua mwanamke tu wala usihangaike kujitutumua.
 
ishanitokea zaidi ya mara moja nahisi ni sababu ya mwili mdogo na wembamba pia sio mtu wa kuvunja kabati navaa kawida sana, ndevu hakuna na ki baby face japo nimekula chumvi.

Kuna siku ilikua fiesta wasanii na team ya clouds ilikua imefikia hoteli ambayo na mimi nilikuepo kuhudhuria sherehe ya ufunguzu wa kampuni fulani ya bima ambayo ni wateja wangu nawapa huduma fulani. Nilitoka mida ya saa 3 usiku kabla event kuisha, wakati nashuka chini naenda Launge kuongea na simu nawakuta ma chekibobu wa clouds akina Bdozen, Mchomvu na wengine wengi tu watoto wa mjini pale launge. nikawasalimia na kukaa ila hawakujibu na waliniona kama sio type yao.

Lahaula, kabla sijamaliza kuongea na simu naona binti kanirukia kwa nyuma na bonge la hug na mabusu ya shavuni na kulalamika nimemtupa simtafuti tena. Wale machekibobu wakashtuka macho yakawatoka, wakamuuliza yule dada vipi upo sawa akawajibu "am very happy nahisi hata show leo nitaperform vizuri". Kwa ufupi yule dada ni katika hawa wasanii wa kike wanaosumbua mjini kwa sasa na nyimbo zao na siku ile ndio alikua kati ya wasanii wa kutegemewa katika show. Kanakumbuka mchango wangu tangia kadogo kananifata kuniimbia akapela, nakakosoa na kumpa ushauri sasa am happy kanaishi ndoto yake.
billnass atakuzingua mkuu.
 
Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka.

Sasa ile natoka nje nikazikuta ziko bize zinajisnap kwenye gari niliyokua nayo, hiiiiiiiiii bagoshaaa, mbona walikoma kunijua.

Nilianzisha zogo la maana makusudi kabisa, nikaita mpaka uongozi wa pale nikawaambia wawaambie wateja wao wafute picha zote walizopiga gari yangu otherwise niite Askari pale obey waniambie Wana lengo gani na picha za mkwaju wangu?

Hahahaha noma
 
Yess madame mmoja hivi alikua na home theater iliunguaga zamani
Nkamwambia niletee niifume kwa mfumo wangu itadunda fresh tu.....akawa ananipimiaaa ,Kama hatak Kama anataka,,,, anyways kanipa
Nikasuka transformer,nkaja circuit ya ndani

Alivoikuta inadunda hakuamini
Akachomoa 200000 pale pale


Of course Kati ya machine zangu zakusuka Ile Ina sound good Sana
Nadhan kwasababu ya speaker zile na box design
 
Back
Top Bottom