Naona simulizi nyingi za magari,wadada,hotel ,ATM nk chukueni hii ya kijijini!
Mwishoni mwa miaka ya 90' nikiwa mwanafunzi Udsm,nilienda likizo!
Nyumbani tunapakana na Taasisi moja ya Elimu ya Kati!
Jioni moja niliwatoa ng'ombe wakulima,wapate majani embeni mwa bara2 ili kesho wawe fit shambani!
Nilikuwa nilienda nyumbani navaa kinyumbani,jinsi iliyochoka kidogo,makata mbuga,mgolole wa kimasai ,fimbo ,kisu kitefu kiunoni, nkachukua Radio enzi nzile Rising Kama mkulima ( aisee RIP baba)
Basi wakapita wanachuo wakasikia nasikiliza kipindi Cha Mjadala Dw Saa 12 Jioni enzi Immune Kher na Othman Miraj mjadala ilikuwa Miaka Kumi baada ya Anguko la Ujamaa Afrika ipo Wapi!
Jamaa kuona Mara Ile wakaona huyu Mlugaluga hata haelewi kinachoadiliw!
Wakaanza kubwabwaja kwa Kingereza kibovu kuwa.. zisi poor,peasant is just deceiving himself listening to International radio,ili wapate muda wa kunisema walisogea wakiniambia nisiingize ng'ombe eneo la Chuo nikawajibu kuwa naijua mipaka!
Siku mbili baadaye kulikuwa na debate pale Chuoni kuhusu ,Demokrasia ya kiliberali na Mustakabali wa Nchi zilizokuwa za Kijamaa...kwa kuzingatia Azimio la Arusha! ...Walikuwa na Mwalimu mwenye upeo mkubwa Sana!
Basi yule Mwalimu kwa kutambua Moto wangu yangu Primary,Sekondary alinialika niwe mchokoza mada!
Nilienda nimevaa makatambuka vilevile na mojawapo ya yule aliyekuwa ananizidoa na ng"ombe wangu kumbe Ni Kiongozi wa Wanachuo na alikuwa Hightable!
Kimsingi walijuta kunifahamu!