Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Kilambimkwidu [emoji23][emoji23][emoji23]upo?
 
Duh.
 
Mbona awamu hizi za karibuni ni kawaida tu kwa wateuliwa au mmeshasahau visa vya waziri Ngereja na Mlinzi wa ATM?


tps://www.jamiiforums.com/threads/kisa-cha-waziri-ngeleja-na-mlinzi-kwenye-atm.49162/page-3
Itume Tena
 
ikawaje mwisho wake?
 
yule dada wa reception aliyekujibu nyodo vipi??[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mwaka juzi natoka kijijini nkafika himo pale nikakuta nyomi ya abiria, nkapanga nichukue vichwa au la maana kuna siku nilichukua abiria aisee alinitesa sanaa, yaani gari ikifika speed 100 ni anaongea adi napunguza mwendo afu alikua mmama, na abiria wenzie wakawa wanamsapoti na mi napenda speed kali,

Nkapaki gari nkaenda kuzurura kuangalia mazingira nikinunua na mahitaji mbalimbali, nkaona mabinti wa3 wamekaa kinyonge baada ya kukosa usafiri na ni saa sita mchana, nkaenda kuwasalimu huku nawahoji vimaswali vya hapa na pale wa2 wakadharau ila yule mmoja akawa ananipa ushirikiano kiasi lkn mwenzie akamwambia kwa kilugha "achana na hilo limtu njoo tuongee mambo ya maana" (nilikua nmevaa ovyo tu na nguo chafu kidogo maana nilitoka porini) hapo wanalaumiana kwanini hawakwenda kupandia gari moshi mjini...

Nkamaliza kununua mahitaji yangu nkaenda washa gari nkawafuata nkamwita yule mmoja alieonyesha ushirikiano akaja nkamwambia mna sh ngapi niwapeleke dar, akasema wana elfu15, nkawaambia ungeni iwe 50 tuende wakafanya hivyo japo kwa aibu na shikamoo wakanipa[emoji23][emoji23][emoji23].

Njiani wanaongea kilugha japo sio cha kwetu kabisa ila nawaelewa sana, hapo wananiteta kiana huku wakilaumiana pengine ningewapunguzia kama wasingenidharau... Waliuliza kabla kama najua kilugha nkawadanganya mi mchaga lakini sijakulia wala kujua hiyo lugha zaidi ya salamu tu

Nkafanya makusudi nkapiga simu kwa jamaa ninaemwazima gari "oyaa mshua vipi, nipo njiani saa 3 ntakua dar nakuletea gari yako" kuskia ivo ndio wakaanza kuniteta tena nawachora tu.

Pale segera nkadakwa na trafiki kwa speed, wakati nawabembeleza nkawaambia sina kitu hii gari ilikua mkoani imeharibika mwenye nayo kaniomba niirudishe dar akaomba kadi ya gari kusoma na leseni akasema unadanganya? Au na leseni ya mwenye gari? Hayo yote walikua wanaskia, nkamalizana nae nkampoza elfu 5 akauliza hao kwenye gari ndugu zako nkamwambia hapana, akasema aliekaa mbele nimemuelewa, akaniambia zuga kidogo nichukue namba akaenda kaongea nae kachukua namba nkarudi kuendelea na safari.

Nkaskia wanaambiana "kumbe ikari li la kajamaa ka, keusani nalo hata ku" mmoja akajibu "tra isarau vandu utevaishi" alimaaninisha kumbe hili gari la haka kajamaa, wala hafanani nalo, mwenzie akamjibu, acha kudharau watu usiowajua.

Kufika dar heshima debe, kumbe walikua wanachuo niliwapeka adi UDSM,

Pisi moja niliielewa kesho yake nkala mzigo baada ya hapo anataka kunifanya kitega uchumi kanijazia mzigo wa shida zake nkampotezea.
 
ndo shida za kuwa na boss mwanamke [emoji2][emoji2]
 
mimi shobo na watu nisiowajua ndo siwezagi kabisa[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kuna dogo mmoja mchafu tu hivi kimuonekano anauza karanga mbichi zile zilizokobolewa na kitenga anatembeza kkoo kuanzia asubuhi na jioni ana kijiwe cha kahawa,
Siku nimekutana nae kule mbagala saku ana nyumba kubwa afu kali kinyama, na nje pana fremu 4 kuna duka kubwa tu anauza mke wake, aliniambia kwake lkn kiukweli sikuamini adi nilienda kuuliza maana nilikokua nimeenda ni karibu.

Kesho yake kaja kuniuzia karanga ilibidi nimuulize kujua labda alikua na maisha mazuri kabla, ndio akaniambia yale yote niliyoyaona yamechangiwa kwa 90% na kuuza karanga, yaani ananunua gunia zima mbichi zilizokobolewa akaomaa akitembeza na zingine anakaangia kashata adi analimaliza kwa mwezi mmoja na akikosa sana faida ni laki 7.
Aisee usidharau usiemjua
 
Kuna jamaa yangu mmoja miaka hiyo anauza duka la ndugu yake pale kawe akatoke dada mmoja mdogo tu akamuelewa sana yaani zaidi ya sana na jamaa umri umeenda na alikua bado hajaoa, yule dada akamtaka amuoe jamaa hataki, nia yake anataka aoe wa kabila lake pia akawa ananiambia huyu dada mzuri sana atakuja kutesa, demu hakua mzuri wa sura kiviile ila hiyo shepu weka mbali na watoto, jamaa akamtosa kaenda kuoa kwao.

Akajajua yule dada ni mjeda pale lugalo na alikua na nyota 3 lkn alikua anamficha na nyumba waliokua wanaenda kufanya yao goba ilikua ya kwake yeye alihisi kapanga,
Jamaa hadi leo anajilaumu na kujitukana kabisa mana yule dada alikuja kuolewa na jamaa anaemfahamu na ndoa kubwa tu kamfungulia mme wake biashara kubwa tu kwenye fremu zake huko goba wanakula maisha tu.
 
Hii hali wahanga wakubwa ni WANAWAKE NA ZILE NJEMBA ZINAZOISHI KIBISHOO MJINI.
Kwangu imewahi kunitokea mara 2 lkn hapa nitaeleza hii moja ambayo imepelekea kumpata huyu mama wa watoto wangu.
Mwaka fulani nikiwa zangu DASALAMA nilikuwa nina tabia ya kwenda kisuper market fulani kupata bidhaa za hapa na pale, sasa kulikuwa na mhudumu mmoha nilimwelewa saaaaaaana, nikajaribu kumsemesha lkn wapi, na hata uvaaji wangu kwa kweli haurudhishi nywele mtihani kuchana, ndevu kama brash ya chachandu, lkn pia kila nikienda huwa nilikuwa naenda na pikpk yangu Boxer, nilimfukuzia yule manzi kama miezi miwili na nusu na sikupata hata namba yake. Mwisho ikawa nikienda pale namsalimia nanunua vitu niwezavyo kwa 30k yangu ndukiiii. Ukapita mwezi bila mm kutokea pale, nyuma huko ile PISI ikaacha kazi yake nami nilikuwa sijui, ikatokea siku moja yule pisi amekuja kwa ajili ya ishu za biashara yake ofisini kwetu. Lahaulaaaaaaa anayemuona anazunguka kwenye kiti ni mimi na nina mamlaka kidogo ya kumtuma mtu na akatii, ile pisi kwanza ilishtuka mm kuniona pale, mi nkaona isiwe kesi nikateremka chini ili niende zangu pata lunch, ila nimefika mapokezi nikajisahau napiga soga na dadaetu wa pale mapokezi ile ikawa inateremka ngazi ikanikuta pale down, akanisalimia nikaitikia akaniambia samahani kuna kitu nimesahau atarudi ili tuongee, mi nkasema fresh huku nikiondoka nje kabisa ya ofisi na kuwasha gari yangu kaliii, yule dada akaniwahi kuomba lift mi nkampatia na sikutaka kabisa mazoea sijui ya kuulizana ilikuwaje wala nn, sikutaka kumpa hata nafasi hiyo nikambwaga alipotaka mi nkaenda pata BIRIANI fureeeesh. Sasa nilivyorudi yule demu akakoma lazima nimuhudumie mm, akalazimisha mi nkamhudumia akaomba no yangu tangia hapo nimemzalisha watoto 2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…