Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ulichukua namba kwa malengo gan? Kama ni kuanzisha nae mahusiano ya kudumu hakufai huyo siku ukiyumba siyo wako
Hapo kwenye kuchukua namba ndio alitimbanga dogo. Alitakiwa ajifanye kama hamjui vile. Ata demu angejileta jamani kaka samahani kwa yaliyotokea jana, angemjibu jana? kimetokea nini?

Unajua sikujua kama, hapana mm mbona mlokole siendagi bar dada. Itakua labda umenifananisha dada. Tuendelee na kazi dada. Huo ndio mvungo sasa.
 
Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka...
Dah hiii Safi Sana[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Dah mkuu umenikumbusha mbali sana, nlikua na mwanangu nae ana mshkaji wake flan mtumishi wa halmashauri, siku moja mwana kaniambia tukutane chako, mitaa flan Dom, akaja na yule mwana, tukapiga misosi na story wakapotea, kumbe jamaa aliona mimi mrugaruga flan hivi sistahiki kampani yao.

Akamchana mwana kwa text kwamba amsindikize maeneo wakasepa ili kunikataa! Njiani akamwambia yule mpuuz anakuaje rafiki yako?

Jamaa akamwambia mwana anapiga PhD afu ana geto mbili mjini hapa...heshima tangu siku hiyo
 
Mie ni tofauti kidogo , tulikuwa safari ya mkoa basi likaharibika njiani , wakati wanatatua tatizo abiria mmoja akashauri kitu Fulani akward dizaini za kuwa harrass wenye basi .nikampinga kibabe na kupata support kutoka kwa abiria wenzangu.

Kesho yake nimefika kwa ajili ya mishe kumbe jamaa niliyejibishana naye Jana yake safarin ndio top wa ofisi niliyoifungia safari ., Ila hakuwa na kinyongo alifanikisha mission yangu
 
Mi kuna mwaka flani nilipewa promotion kwenda kuwa branch manager mkoa flani. Sasa sabab nilikua bachelor nikauza vitu vyote nikabaki na mabegi ya nguo nikapaki kwenye ndinga nikaamsha. Nikafika mkoani mida ya sa 9 na mafuta yalikua yamekaribia kuisha nikasema nikachomoe mpunga kwenye atm ya hiyo bank ninayofanyia kazi. Nilivomaliza kutoa hela na muda wa bank bado nikasema niingie kumsalimia branch manager aliyepo maana tulikua tunafahamiana. Ile kuingia reception mdada mmoja matata sana ndo yupo pale na pembeni kaka jamaa mwingine..nikamsalimia akaitika vizuri tu,nikamwambia naomba kuonana na meneja..akainua macho kuniangalia...akanambia sema shida yako...nikamwambia shida yangu ni personal,akasema huwezi kumuona ..tena kwa madharau. Na yule jamaa wa pembeni akaniangalia akaendelea na ishu zake.Nikamwambia basi sawa ntampigia simu,akanijibu kwa kejeli kumbe namba yake unayo...yule jamaa wa pembeni akacheka..nikasepa nikaenda kuchkua hotel. Jion nikamcall meneja nikamwambia nipo nishafika akafurahi sana maana kama nilimsurprise na skumwambia kama nilifika ofisin. Jioni akanitafuta tukapiga vyombo huku akinionesha machimbo. Kesho yake asubuhi kwenye morning talk akawaambia staff meneja mpya kashafika atakuja mchana kuwasalimia. Mchana wake nikaibuka... Hahahahaaaa basi wapenzi wasikilizaji mtamalizia wenyewe kilichofuata.

Kisa cha pili ni sehem nilipoenda kupanga room maana sikua na familia na vitu niliuza so nikazama kama ninja...wakawa na madharau yao mi sina time nao mpaka wamekuja kujua badae sana ndo wanajichekesha maana hata gari nilikua silazi pale hapakua na parking.
walivyojichekesha ukarespond vipi?
 
It was a suprise kwangu.

Jirani yangu aliokuwa wanajifanya ni Boss wa Ikulu mtaani muda wote kanuna na miwani yake mieusi alikuja kunihudumia Chai Ofisini kwa Mama Salma Kikwete wakati wa WAMA, kumbe Alikuwa Office attendant pale tena wale wa oya oya na mie na wenzangu tulienda kupeleka project paper ya ki NGO chetu ambacho ni Hayati kwa sasa kuanzia 2015.
Mkuu, unamaanisha ki NGO kilikufa tangu 2015??
 
Naheshimu sana watu pamoja na kazi zao. Nimejifunza mengi sana kupitia watu
Yeah maana huwezi jua nani atakusaidia kwa wakati gani.......ni wachache wanalitambua hilo,ila tuliozoea kutembea sehemu mbalimbali ktk kusaka maisha,tulilijua hili mapema sana.....unafika sehemu hujui pakuanzia ila ghafla unasaidiwa na mtu ambaye hukuwahi kutegemea
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu...
Yes, imenitokeaga
 
Dah mkuu umenikumbusha mbali sana, nlikua na mwanangu afu na ana mshkaji flan mtumishi wa halmashauri, siku moja mwana kaniambia tukutane chako, mitaa flan Dom, akaja na yule mwana, tukapiga misosi na story wakapotea, kumbe jamaa aliona mimi mrugaruga flan hivi sistahiki kamapani yao. Akamchana mwana kwa text kwamba amsindikize maeneo wakasepa ili kunikataa! Njiani akamwambia yule mpuuz anakuaje rafiki yako? Jamaa akamwambia mwana anapiga PhD afu ana geto mbili mjini hapa...heshima tangu siku hiyo
kwa hiyo hapo ulipo una PhD mkuu?kwa uandishi huo?
 
Mimi uzuri nina adabu simdharau mtu kwakweli ila kuna Mtu aliwahi kuvuka matarajio yangu yani sikutegemea.

Maana jamaa alitaka nikamfanyie kazi fulani akanambia niandike namba atanicheki anatumia Tecno S series😂 nikadharau nikajisemea huyu nae nani🤣, siku ya kazi kaja kunichukua Offisini na Range rover sport anaishi Cliffside resiidence toure dr hakuna kazi nililipwa kama hio mtu unafanya kazi huku unakunywa Moet Chandon Shampaigne.
 
Juzi tu NMB Dodoma:

Jamaa flan kavaavaa tu afu na midevudevu hivi

Kaenda NMB ATM kakuta na wadada wa benki wameweka meza ya kutoa huduma kwa wateja pemben hapo. Akafika tu kauliza (bila hata kusalimia).....kwanini kadi yangu inakataa kuniunganisha NMB mkononi

Dada kamjia juu...."kwanza salimia;...vipi habari za huko,...haya tukusaidie nini??"

Jamaa hakupokea. Mie nawaangalia tu.

Dada karudia tena ...."vipi mzima mwenzetu?? Za ulikotoka??!.....mbona umekuja kasi sana??!"....

Jamaa anaeaangalia tu. Mara akauliza...."ivi ni lazima kusalimia/ au kupokea salam ya mhudumu ili nipewe huduma NMB???...

Wakaanza kumshangaa ..."unatokea wapi wewe, yani unakuja kuvamia tu bila kusalimia..." ....wamamzodoa flan.

Jamaa akaingia Benki ndani. Straight kwa Meneja. Nafkiri hakueleza shida aliyopata nje. Alimueleza tu kama kutaka kusaidiwa shida yake. Sijui ndani waliongea nini??

Wametoka na meneja...hadi pale ATM kwenye meza ya wale wadada....meneja akiwa kashika mkononi kadi ya yule mshua....akawambia wale wadada mmoja wao (sikumbuki jina)...

Meneja: .....hebu msaidie Katibu Mkuu hapa kumuunganisha na NMB Mkononi...(Meneja akaongeza:....mkuu hapa utahudumiwa)...mara meneja katuomba wote wa kwenye foleni ya ATM..."naomba ndugu tumpishe kiongozi anajambo kidogo kwenye ATM ...samahani"...wakaingia ATM meneja, mshua na yule dada.

Wakafanya mambo humo ...kidogo wakatoka. Tukaendelea.

Meneja akamsindikiza yule mshua hadi kwenye gari akaondoka meneja anapunga mkono.

Niliwaangalia wale akina dada mavi yalivyowagonga chupi. Walitoa macho sana wakawa na wasiwasi mkubwa....

Walimchukulia poa
 
Back
Top Bottom