Huwezi nilazimisha nikusalimie wakati wa kupokea huduma. Sio lazima kabisa wala haiongezi au kupunguza chochote.
Nikija customer care nahitaji huduma, salamu naweza enda shule ya msingi wakanisalimia watu zaidi ya 1000 na shida yangu isitatuliwe.
Binafsi huwa sipendi MTU anayependekeza salamu. Ujue salamu ni aina ya malipo ama kumnunua MTU moyo wake ili akusaidie kitu Fulani. Ina mana bila ya salamu husaidiwi.
MIE hata ukinipita bila ya salamu afu unarudi umepotea njia nakuelekeza kiroho safi na hata ukinisalimia kama kuninunua ili ndipo nikuelekeze MIE naipotezea salamu yako na kama Nina muda nakupeleka mpaka unakoenda.
Warusi ukiwauliza kitu afu wakakusaidia na ukiwashukuru wanaikataa shukrani yako kwa kuuliza ya nini iyo shukrani. Ina mana wako willing kukusaidia bila hata kuwalipa.
Sasa bongo ndipo utashangaa MTU anakomalia salamu utadhani itamuwekea chakula mezani.
Binafsi sipendi kusalimiwa naonaga kama ni utumwa Fulani yaani ni lazima usalimie kila asubuhi. MIE wangu aishanielewa hakuna salamu hata kama nikitoka kwa wiki nzima. Nikirudi unapita muda kidogo tunaanza story za huku home na huko nilikokuwa.
Wazazi wangu hawakuwa watu wa kudemand salamu kila siku asubuhi. Ilikuwa ni kuamshwa kuwahi shambani basis.
Mpaka umri huu huwa nikienda home salamu ni zile siku za ugeni wiki ikishapita hakuna salamu.
Pia siamini kuwa salamu ndio heshima.
Nina imani masikini anapenda sana salamu mana kwa njia hiyo anajisikia faraja sana anadhani naye anajariwa. Masikini ndiye anayetembelea ndugu zake waliofanikiwa na kuwaongelea na kuringishia watu. Kuwa usinidharau yule karibu mkuu ni mdogo wangu nimemsomesha MIE. Ni kama Mwita weitara akasomeshwa na kaka yake aliyekuwa nauza mayai hapo kipunguni saivi sijui wanakaa kivule.
Ni mfano tu nimetolea hapa kwa karibu mkuu.
Salamu ni muhimu ila isiwe lazima jamani .yaani kuna watu wanaifanya kuwa basic needs kwao.
Binafsi nikiwaga home kwetu huwa siishi kwa furaha mana kila unayepishana naye yabidi u pay attention kwake na umpatie salamu tena usimame mpige story kidogo.sasa ole wako uje upite usalimie ukipunga mkono nakuambia ,Fulani anaringa kisa akasoma ,ama ana Hela.
Ila nikiwa town salamu sio lazima naishi kwa Uhuru hakuna MTU anayejiliza kuwa umetupita bila ya salamu rafiki.
Binafsi kunyenyekea ama kunyenyekewa sipendi.
Haya shikamooni wana jf wote waliozaliwa 65 kurudi nyuma. Wa 66 mpaka 1990 mambo vipi. Waliozaliwa 90 mpaka 2020 mnipe heshima Yangu
Unadhani kwa salamu Umepata nini katika maisha yako hata nisingekusamia si ungebaki na shida zako zilezile ama kuna kitu kimeongezeka.
Binafsi I hate salamu ingawa ni opener ya maongezi. Kuna watu naowakubali sana binafsi unamuuliza MTU kitu anakujibu mwishoni unashukuru na kumpatia salamu yake unasepa. Watu wa ivyo huwa naowanga ni matajiri rohoni kwao ni matajiri rohoni mwao!!!!!