Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

U

Unayemjua ndio unamdharau? Haitakiwi umdharau mja yeyote uwe unamjua au humjui
Over!
Sio kwamba ninaemjua ndio namdharau, hapana namaanisha mara nyingi watu huwa wanawadharau watu wasiowajua since hawajui status zao mwisho anaona sio alivyomdhania refer shuhuda zote humu. Mimi nawaheshimu wote ninaemjua na nisiemjua. Sababu hata unaemjua ukamdharau huwezi jua lini atakuwa msaada kwako.
 
Jamaa limekuja mtaani kujenga kamjengo kake,katukuta wenyeji tuna mwagilia moyo,yupo na mkewe hata salamu yaani kakausha tu,kachukua mafundi akawaelekeza kazi pale,zikaja semi 2 zimekula nondo na cememt, kisa anajenga ki gorofa hahaaa,kilicho tokea kabakia kwenye msingi tu wabane wae kwara kuanzia nondo mpaka cement mpaka tofali yaani,kaja kushuka baada ya wiki,wenyeji wamejenga kupitia jamaa kuja kushtuka hana pakuanzia,tunasiki yowee tu huko jamaa hana wakumuuliza ,ndugu zangu ukifika sehem usi mdharamu mtu,huwezi jua atakusaidia lini na wapi.
 
Hii bank ishanitokea sana, hasa wale walinzi wa suma jkt wanadharau sana

Ninapoondoka huwa na maswali mengi sana na wasinielewe


Sometimes nafanyaga transaction kubwa kwa niaba ya walionipa kazi fulani ya kuwasaidia.
 
Ulitisha Sana mkuu😂
 
Aisee wahuni walibebaa Bidhaaa zotee na nyie mkakaushaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Miaka flani hivi 1994 nikiwa nasoma college, nilikuwa napiga kazi za taxi bubu hapa Dar. Kijiwe flani mitaa ya mwenge. Hiyo kazi nilipiga miaka yote nikiwa nasoma college. Sasa gari yenyewe nliyokuwa napiga nayo taxi, ilikua gari ya kuungaunga kwa sana. Yani spana mkononi. Kwakua na mimi nlikua najua ufundi kimtindo, nlikua naimudu vizuri kazi yangu.

Sasa kuna mama mmoja alikua anafanya kazi taasisi flani binafsi inatoa huduma ya kupokea na kusafirisha vifurushi. Huyu mama alikua na nyodo balaa, kila akinikodi, nikimfikisha safari yake nikidai hela, lazima aiseme gari yangu vibaya mno, mi nikawa namezea tu, ilimradi pesa yangu alikua ananipa.

Yani yale maneno yalikua yananiuma sana mwanaume mpaka nikaweka nadhiri kwamba nikimaliza kusoma nikipata kazi lazma ninunue mashine moja kali sana.

huku na huku, mwaka 1998 nikapata kazi ya uhasibu kwenye shirika moja la waswisi. Nikaajiriwa kama mhasibu msaidizi, moja wapo ya majukumu yangu yakawa ni kutayarisha malipo ya suppliers na ku issue checks kwa suppliers, pale zikiwa zimeshasainiwa na mkubwa wa kazi.

Lile shirika analofanya kazi yule mama mteja wangu wa taxi mwenye nyodo na maneno ya kejeli nalo likiwemo kwenye list ya suppliers.

Siku ya siku yule mama katinga ofisini kuja kuchukua check, kanikuta mwamba ndio mhusika pale, hakuamini macho yake, kajitahidi kunisalimia kwa kuchangamka na mbwembwe zote, mi sikuongea sana nikamsalimu, nikamkaribisha, nikamwonyesha sehemu ya kusaini, akapiga wino, nikampa check yake akasepa.

Next time weekend, kanikuta maskani, kanikodisha, maneno yote ya kejeli hayakuwepo tena, na akawa mteja wangu mzuri sana, mpaka nlipopiga chini hiyo kazi ya taxi, na kuamua kuweka muda zaidi kwenye ajira yangu na waswiss.

Hayo ndio maisha, people will judge you by your looks or mazingira utakayokuwepo, but all is good, keep hustling, no matter what.
 
Hii ni update ya hivi karibuni.
Jamani dunia tunapita.
 
Juzi tarehe 20 Jan 2023 nipo zangu Mwanza nimekuja kupiga mishe 2, 3!
Kuna mdada ni mpangaji kwenye nyumba yangu hapa lkn hatukuwahi onana zaidi ya kutumiana contracts kusign na mawasiliano ya simu.

Basi last week nikampigia simu kuwa nitakuwepo Mwanza kwa ajili ya kazi fulani ya marekebisho hapo nyumbani (kimsingi kuongeza ubora wa nyumba) basi nikafika J2 pale site... nikaanza kazi na mafundi piga kazi hadi jioni nikasepa zangu...J3 nikafika tena site...piga kazi za hapa na pale na mafundi mara pap sister ameingia akanisalimia tu kishikaji nikaitika akaingia ndani baadae akaja kuwapokea watoto wanatoka shule jioni hiyo saa 11 hv... baadae nikamwambia sister sorry niliona simu yako jana lkn late sana nilikuwa nishalala akahamaki; simu nikamwambia ndiyo...nadhani aka recall baadae akasema wewe ndo baba mwenye nyumba nikamwambia yap....ghafla akakunja mikono kama nidhamu fulani akasema sorry sikukutambua nami nikamwambia worry out ... basi akaniletea maji ya kunywa tukapiga story tu kidogo.....

Baadae akafunguka kuwa dah yaani mi naongea na wewe siku zote najua ni bonge la mbaba...nikacheka zangu tu nikamwambia surely ni bonge la mbaba sema nafanya sana mazoezi ndo maana sina nyama zembe wala tumbo la kuwekewa puto....
 
Hukupiga mwanangu??
 

Inaonekana ww mwanangu ni kichwa san yan hauna papara
 

Yan katika nakala zote hii ni best zaid
 
Mimi huwa ni ngumu mtu kunitambua kama najua kitu au niko interested kwenye jambo fulani kwasababu ni mtu nisiyependa show off (kujionesha). Nitaelezea machache katika engo tofautitofauti


Madrasa
Enzi za udogo (ujana) nikiwa madrasa jamaa katika kusoma Quran akakosea halafu yeye ndo ana jukumu la kutufundisha basi alipotoka tu yule mfundishwaji nikamrekebisha kistaarabu kabisa jamaa alistaajabu sana ilibidi amuite yule aliyekuwa akifundishwa arudie upya. Ebana wee tangu hapo nikawa nimechokoza moto vijana (maustadh) karibia wote wakawa wakitaka kwenda kusoma (kuaridhi) kwa mwalimu lazima waanzie kwangu kwanza ili nikague makosa yao na alhamdulillah kwa uwezo wa Allah nilikuwa sibahatishi ingawa sura hizo sikuwa nimezifikia bado

Cherehani
Mzee alikuwa anapokea tenda fulani ya kushona halafu anampa kaka sasa ikafika kipindi kaka hayupo yule mtoa tenda akaambiwa safari hii ile kazi yule uliyemzoea hayupo utafanya na huyu (yaani Mimi) jamaa akawa haniamini tena akasema kabisa "huyu dogo hivi aisee ataweza?" Mzee akamwambia wewe usijali huku Mzee nae akiwa na mashaka kwenye spidi yangu basi nilikamatia ile kazi kwa ubora wa hali ya juu na ni ndani ya muda. Mbona walinyoosha mikono na mpaka kesho yule jamaa ananiita fundi

Sensa
Nimeitwa nikarekebishe kishikwambi cha karani, maudhui kaniambia niwakute ofisi ya kijiji basi nikachukua boda fasta. Kufika nakuta mtendaji anaongea na yule maudhui nawapa hai makarani wanaitikia, nawasogelea mtendaji nampa salamu akageuka tu kuniangalia kisha akaendelea kuongea mazungumzo yake nikaachana nae maana huwa sirudiagi salamu muda huo maudhui anafanya kama anandoka kunielekea eti yule mtendaji anamzuia "bwana aachana nao hao angalia huku bado sijamaliza mimi unaenda wapi?" (Akili yake akijua mimi na yule bodaboda labda ni wageni wake katika ofisi yake). Basi yule maudhui akamwambia huyu anahitajika kwingine akiondoka ndo basi tena basi akaambiwa huyu ndo IT wetu wa kata (kama unavyojua tena kwenye sensa watu tulibandikwa matitle makubwamakubwa wakati hatuna lolote- tulitambulika kama maafisa wa sensa ambapo karani aliitwa tu kawaida afisa wa sensa maudhui aliitwa afisa maudhui, mtu wa tehama aliitwa IT). Basi yule mdada aliduwaa yaani akapoa hadi nikawa namuonea huruma akiniangalia hanimalizi na Mimi kwa sifa nikashuhulikia kilichonipeleka kisha ndefu najidai nina haraka

Muvi
Imezoeleka wa shule za kata hatujui ung'eng'e sasa bana eti tunaangalia muvi enzi hizo ndo nimetoka form four jamaa akaniambia hii muvi hutaielewa maana haijatafsiriwa kama muvi zenu mlizozoea basi nikamwambia kama wanaandika (subtitles) basi nitajikaza akaniambia hakuna hiyo kitu. Kucheki ati jamaa akaanza kunishereheshea baadhi ya vipande sasa ikawa kamba nyingi ikabidi nimtolee uvivu mara paap! Mimi ndo namsaidia kumtafsiria tena


Misikitini
Kwa wale wanaoenda kuswali misikitini mtanielewa zaidi. Tumehamia sehemu kwahiyo ikabidi nihame hata msikiti niende ulio karibia na kwetu. Sasa kawaida yangu (kawaida yetu vijana wa madrasa) huwa hatujirembirembi katika maswala ya dini basi swala ikikimiwa tu tayari nipo beside ya mkimuji mbele kabisa. Basi siku hiyo ustadh mkimuji akanitoa ananambia nikae nyuma hapo mbele niwaachie mashekhe (wakati kiuhalisia nikiwaangalia ni mashekhe umri yaani wazee na sio mashekhe kwa elimu). Mungu si Athumani bwana siku hiyo tumechelewa swala kidogo na yeye akiwemo basi mmoja akasema Fulani tuswalishe bana (akinitaja Mimi) basi tangu hapo yule jamaa akawa akiniangalia tu hanimalizi

Wakati nipo chuoni tena (ualimu) msikiti mmoja jamaa mmoja nae alichelewa nikamswalisha swala ya sauti basi kutoka akaniambia "mbona mtu akikuangalia hawezi kuamini kama ni wewe uliyeswalisha pale? Yaani uvaaji wako na namna ulivyo me nkadhani wewe ni mkristu."

Huku kazini nimeswali nao karibia mwaka hawajanigundua sasa kilichokuja kuniponza ni somo la Dini. Ikabidi nijidhihirishe tu lakini na wao walidhani ni muislamu jina tu hata majina yangu walidhani ni majina tu ya mchongo
 
Hihihihi[emoji23][emoji23]
 
Kitu kingine ambacho sisahau mpaka leo aisee ni wakati nipo mdogo ilikuwa matangazo ya pombe yale mfano Heineken na tusker yalisababisha nikawa napenda sana Heineken. Sasa siku nikaikuta njiani mtu kabakiza ile ya kopo nikaokota namwambia kaka kuwa nataka niinywe. Basi ile nimeinyanyua nataka kupeleka mdomoni jamaa aliniambia acha wewe pombe hiyo! Basinikaitupa. Ebana wee akaipeleka ile hadithi kwa Mzee basi nyumbani wakawa wanaambiana kuwa nikija kuwa mkubwa nitakuwa mlevi mmoja mkubwa na matata sana... Walinitabiria pia kuwa nitakuja kuwa mtukutu sana kutokana na namna nilivyokuwakuwa katika makuzi yangu lakini cha ajabu ni kwamba kufika darasa la 3-4 zile dalili ovu zote zikatoweka nikawa mtoto mwema sana

Tanbihi;
Namshukuru Mola mpaka leo sijawahi kunywa pombe yoyote Wala bangi/sigara/mirungi wala energy wala shampeni. Kisa cha Mimi kuipenda Heineken naomba nitoe fundisho kwa wazazi wenzangu. Tangu nakuwa nimelelewa kwamba pombe ni haramu lakini nguvu ya media (video) ikanifanya niipende kwasababu kwanza hawasemi kwamba ile ni pombe na pia kuipamba pamba kule na maneno mengi basi moyoni nikaamini ile inanifaa na huku nikimchukulia yule wa kwenye tangazo kama ndiye role model wangu. Maana yake nisingekuwa na kaka ningeinywa au hata kaka asingesema ni pombe huenda ningeitafuta kivingine nipoze roho (pombe tulikuwa tunajua za kienyeji tu na bia ilikuwa ni safari na Kilimanjaro). Tuwafuatilie watoto na ma video haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…