Aiseee...!
Umenikumbusha mkasa mzuri tena wa zamani kidogo.
Ni mkasa wa kweli wa umfikiriaye ni mswahili wa low class, kumbe miaka ikipita ndo anakuwa matawi ya juu.
Kulikuwa na dame, mzuri sana , miguu ya kupendeza figure eight na kwa kweli kila nikimuona moyo waenda mbio.
Na alikuwa ni cheusi mangala, super black, akicheka meno meupee ya kuvutia, juu ni afro zuri natural, hadi leo hii.
Wazazi wake nilikuwa nawafahamu, nivyo nikaona itakuwa rahisi kukubalika.
Ndo kwanza miaka hiyo nimemaliza Form six, dame anaelekea kumaliza form IV.
Sasa nikawa nimepata kibarua cha ukarani benki, hivyo vijisenti vya kununua soda sikosi.
Nikamwaga sera kwa dame yule.
Yeye akawa kama ananihurumia tu, maana anaona nampenda sana lakini anashindwa kuwa muwazi.
Miezi ikapita mingi tu, tuna date na kila tukionana naona hakuna maendeleo, hadi dada zangu wakaanza kunihurumia pia, penzi linavyonitesa.
Mwisho yule dame akaniambia wazi, we bwana si saizi yangu, kwanza watoka Uswazi.
Akaniambia nina mchumba mtoto wa balozi fulani, famous hapa mjini.
Na wazazi wa yule dame walilielewa hilo, kulingana na dame mzuri.
Basi sikukata tamaa, nilijahidi kumweleza dame wangu huyu kuwa mimi haipiti miaka miwili nitaingia chuo kikuu na nikimaliza sitakosa noti ndefu kukutunza wewe na familia, nikubalie tu.
Dame akakataa kata kata.
Siku aliyohitimisha maneno ya kunikataa niliugua, tena homa kali na ya kweli kabisa.
Sikujua kuwa penzi literaly ni homa ya moyo!
Nilinyong’onyea na kulala kitandani siku mbili.
Ile homa naikumbuka vizuri sana.
Slowly homa iliondoa na kukausha upendo wote kwa yule dada.
Nilistaajabu hata mimi kwani nikajiuliza , kwa nini niteseke?
Na kwa muda mrefu sikutafuta tena msichana mwingine awe girlfriend wangu wa kudumu, ile homa iliniumiza ifikra.
Miaka ikapita, na kweli nikaenda UDSM, na kukamilisha kadigilii kangu na kazi nzuri nikapata.
Kazi nikaendelea kupata nzuri zaidi, kumbe yule dame, cheusi mangala, ananifuatilia kwa mbaali.
Miaka mingi ikapita, na mambo yangu alhamdulilhi yakawa si mabaya sana.
Wakati huo ikawa nimepata fiancee kwa kweli mzuri sana, tena half caste.
Huku nyuma dame cheusi akajileta, na tukala mzigo.
Aliponiuliza itakuwaje sasa, nikamwambia tu ukweli kuwa naoa miezi michache ijayo, ile chance haikuwa yetu.
Alilia sana yule dame mzuri.
Mbaya zaidi mie kikazi nikawa matawi ya juu sana, kama nilivyomuahidi dame cheusi nilipokuwa namtongoza na akakataa.
Sikumuuliza imekuwaje na yule mtoto wa balozi, maana sikuona kama yananihusu.
Dame cheusi mangala bado ni mzuri na akajaolewa na classmate wangu.
UPDATE:
Tunaandika hadithi ambazo ni za ukweli kabisa.
Cheusi Mngala baadaye niliambiwa mume wake alikuja fariki kwa ugonjwa wa sukari.
Ingawaje wengi tuihisi ni kale kaugonjwa kanako sumbua.
Kilichonishtua majuzi ni kuambiwa Cheusi Mangala naye kafariki, nilivyompenda nililia!