sisi wengine baada ya hapo ndio huwa tunafunga vioo mazima,yaani fanya kama hatujawahi kukutana.
mimi jamaa alinisimulia hii tabia ya kudharau mikakati ya mtu katika maisha yake, usione mtu kazini yupo yupo tu miaka inaenda ukamdharau kwamba hana mipango, utajichanganya.
jamaa anasema wameanza kazi mwaka mmoja na huyo mshikaji wake, yeye akawa amepanga nyumba ya gharama kama 250k,usafiri wa kusumbulia watumjini nk. mwenzake yupo yupo tu. nyumba katafuta ya 120k, gari hakununua nk.
wamefanya kazi kama miaka 8 hivi. baadae siku moja wanapiga story jamaa yangu sasa akaanza maneno ya kumsimanga jamaa, oooh we vipi bana hela hatuoni wapi unapeleka, upo upo tu kama mshamba.jamaa akakereka ikabidi amuonyeshe salio bank, akasoma kwa utulivu ilikuwa ni 68mil, kwenye simu kuna 7mil.
baada ya pale jamaa siku yake iliharibika sana.