Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

sisi wengine baada ya hapo ndio huwa tunafunga vioo mazima,yaani fanya kama hatujawahi kukutana.

mimi jamaa alinisimulia hii tabia ya kudharau mikakati ya mtu katika maisha yake, usione mtu kazini yupo yupo tu miaka inaenda ukamdharau kwamba hana mipango, utajichanganya.

jamaa anasema wameanza kazi mwaka mmoja na huyo mshikaji wake, yeye akawa amepanga nyumba ya gharama kama 250k,usafiri wa kusumbulia watumjini nk. mwenzake yupo yupo tu. nyumba katafuta ya 120k, gari hakununua nk.

wamefanya kazi kama miaka 8 hivi. baadae siku moja wanapiga story jamaa yangu sasa akaanza maneno ya kumsimanga jamaa, oooh we vipi bana hela hatuoni wapi unapeleka, upo upo tu kama mshamba.jamaa akakereka ikabidi amuonyeshe salio bank, akasoma kwa utulivu ilikuwa ni 68mil, kwenye simu kuna 7mil.

baada ya pale jamaa siku yake iliharibika sana.
Hahahaa kmmk
 
Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka.

Sasa ile natoka nje nikazikuta ziko bize zinajisnap kwenye gari niliyokua nayo, hiiiiiiiiii bagoshaaa, mbona walikoma kunijua.

Nilianzisha zogo la maana makusudi kabisa, nikaita mpaka uongozi wa pale nikawaambia wawaambie wateja wao wafute picha zote walizopiga gari yangu otherwise niite Askari pale obey waniambie Wana lengo gani na picha za mkwaju wangu?
Hahaa
 
Sasa kama hata uyo wa kupata wapi namba hayupo ntafanyaje[emoji15]
Mimi wanajua nachagua sana kumbe walaa basi tu napenda ustaarabu,mwanaume anaeandika bac,xaxa,kwio ake sitaki kabisa bora niwe mtawa[emoji2]
Mimi siandiki hvyo naomba nikupeleke Kilimanjaro ukamuone mama yake Papaa007
 
Kila mtu kaandika ya kwake ngoja na mimi niandike ya kwangu kipindi ninemaliza form 4 mkoa fulani nikaenda mkoa mwingine kuna ndugu zangu nimekaa pale ndugu yangu kafungua banda la mkaa nikasema ngoja nikae hapa niuze basi watu wanakuchukulipia poa sana km muuza mkaa huna jipya.mara tokeo limetoka huyo advance then chuo ila watu wengi mtaa ule hawakujua harakati zangu baada ya mkaaa maraa eeeh nikapata field karibia na mtaani pale pale kuna shirika la uma nikaa kitengo matata full upepo kwa hiyo wale waliokuwa wananiona muuza mkaaa walikuwa hawaamini kinachoendelea


Funzo usimdharau mtu kwa muonekano
Kabisa
 
Back
Top Bottom