korino
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 1,004
- 666
Aisee!!!! Mungu azidi kukubariki kaka wamebaki wachache km ww dunianidah na mim umenifanya nilete kisa changu ambacho hakina hata miezi miwili.
kuna mdada jina yupo katika ofisi fulani ni majirani zetu(home).Ni wale watu wanaoringa kupita kiasi ukimsalimia kama hakuoni vile( hii ishatokea kama mara 3) last time niko zangu na town anafanya kazi pale benjamin mkapa,nmemkuta yupo na wenzake wakati huo nilikuwa niko na kaka yangu mkubwa.
Nikamchangamkia ila mwenzangu kanilia buyu namtambulisha kwa bro kuwa huyu ndo jirani dah mixer mfyonyo juu hakuna siku roho ilikuwa inaniuma kama siku siyo.
sasa week kama 3 nyuma natokea moro nmeingia kama saa 6 hivi nikasema ngoja sku ya leo nikasalie pale upanga maamur ni mskiti ambao waislamu wengi sana wanapenda kuosha maiti pale na kwenda kuzikia makaburi ya kisutu.
Nilivyofika pale pakawa kama na stori za chini kwa chini kuwa muosha maiti amekimbia baada ya kuosha maiti zaidi ya tano kitu ambacho syo cha kawaida, basi kwenye maongezi maongezi ikajulikana kuwa kuna maiti kama 2 zimeshndwa kuoshwa ndugu hawajui na muoshaji kakimbia(hofu ya corona)
Basi tukajitokeza mimi na mwenzangu tukaingia chumba cha maiti tulikuwa kama wa 4,tukaiosha ile ya kwanza,then tukafata ile ya pili zote tukaandaa safi kabisa ila ile ya pili niligundua alikuwa na baba wa yule dada maringo.
wakati tunatoka kuosha ndugu wakatuvuta pembeni wakatupa kama laki 3,wenzangu walichukua ila mimi sikuchukua hata cent sasa kumbe aliyekuwa anatoa hela ni mdogo wa yule(dada maringo) ambae anaishi nairobi kaja kumzika mzee wake but hanijui.
basi tukachukua maiti tukaenda zetu kuzika makaburi ya kisutu, wakati narudi zangu maeneo ya home ndo nakuta msiba sasa huku zogo pembeni likiwa ni muosha maiti kukimbi, basi jamaa akaniona mdogo mtu tukasalimiana pale ile furaha aliyokuwa nayo akanishika mkono mpaka uwani ambako kulikuwa na dada zake na mjane akanitambulisha na jinsi nilivyowasaidia dada mtu(cha maringo) aliangua kilio kupita maeleozo akaniomba namba nkampa.
baada ya kama dakika 30 baada ya kurudi home nikatumiwa mesage kama gazeti ya kuniomba radhi/msamaha mie nka act humble tu japo kila siku anataka tuonane but kila akinipigia namwambia niko moro japo anafosi anitumie hata nauli nikaonane nae au aje yeye but namchomolea.
katika maisha usimdharau mtu kwani huwezi jua nani atakaekufaa kwani unaweza kuwa trilionea but msaada wako ukatoka kwa mwenye kupata sh 500 kwa siku