EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Kuna mambo mengi yanaweza kukutokea ukiwa safarini
1. Kutapika kwenye gari
2. kubanwa na tumbo la kuharisha
3. Kuachwa na gari wakati wa kuanza safari au wakati mmeshuka kupata chakula.
4. Mengineyo
Mwaka flani nilikuwa natoka Morogoro kwenda Dar. kabla ya safari nakumbuka nlikula zile chapati za Azam (ready made) saivi hazipo sokoni kwenye mgahawa wa wahindi flani pale Morogoro.
Safari ikaanza kufika Mlandizi tumbo likaanza kuuma na nimekaa katikati ya basi la Abood, aisee maumivu yale sidhani kama nishawahi kuumwa makali kama yale nilijitahidi sana kuvumilia ila uzalendo ukanishinda nikaomba kushushwa njiani nikaingia choo cha Bar nikaharisha saaana kama nusu saa nipo chooni, nikaenda kununua dawa pharmacy, baadae nikachukua daladala nikaendelea na safari.
Hebu tupe kisa chochote kilichowahi kukukuta ukiwa safarini kwenye Mabasi.
Karibuni wadau.
Nishamaliza!!