Ilikuwa mwaka 2009 nikirudi St John Dodona Chuoni, nikiwa katika basi la Scandinavia, baada ya kuimaliza Morogoro kwa mbele, tumbo likaanza kuuma, nikahisi kuharisha. Nikamuomba konda wa basi, akaniruhusu, nikaenda polini maana ilikuwa polini na sikuwa na namna, akanipa maji, nikakaa huko kama dakika 1, najua wajua tumbo la kuhara, unahisi kama mzigo bado upo. Nikamaliza nikarudi kwenye gari. Gali ilinidubiri, kutembea kidogo nikabanwa tena, nikasema na konda, gari ikasimama, kwenye siti nilikaa na Classmate wangu wa kike.
Dah safari haikuwa rahisi ila mwisho wa siku tukafika Dom kwa taabu sana. Sitasahau. Sababu ya madhira yote hayo ilikuwa kula kuku katika harusi ya baba yangu mdogo, wale kuku walikuwa kama wameharibika.