Ushawahi kufedheheka (kupata dharura) ukiwa safarini kwenye usafiri wa umma?

Ushawahi kufedheheka (kupata dharura) ukiwa safarini kwenye usafiri wa umma?

Nakumbuka mwaka 2006 natoka Iringa nakwenda Moro nilisafiri na kampuni hiyo,nili pata chakula pale aljazera baada ya mwendo kidogo tumbo likapoteza network nili vumiliaaa hadi nika ona kuendelea kuvumilia nita haribu safari ya wengine.

Nlipo amua kuelekea kwa dereva niombe fair daaa MUNGU mkubwa basi lika anza kumiss dereva bila shuruti kaweka kando niliteremka kwa spidi nikazama chaka nika sevu ngoma tartiiibu bahati nilikuwa na kopo la maji nika jiswafi vizuri.

Walipo maliza kukorokocha safari ikaendelea baada muda tena tumbo lika badilika tenaa,na gari ika zingua tenaa hapo tulikuwa kwenye maeneo wanaishi wamasai pale nika omba kwenye nyumba ingawa kuingia mle toilet ilibidi ni cha gue pa kuka nyaga manake watoto walikuwa wame kichafuaa vibayaa nashukuru nika maliza shida zangu pale.

Toka hapo tumbo haliku zingua tena na gari haikusumbua hadi tuna ingia Morogoro, hakuna mtu aliye jua kama nilikuwa na endesha siku ile sipati picha ninge haribu mambo kwenye basi.
Mara ya kwanza ulikuwa na chupa ya maji vipi kwa wamasai kulikuwa na maji toi
 
Mwaka 2013 natoka songea nakuja dar na wenzangu tumetoka jkt na mabasi ya SUPER FEO. Picha linaanza kambi ya jeshi tunatoka kwa mabogi mabogi sasa sisi bogi letu likawa la mwisho ..

Basi bhna ile tunatoka tu stendi kumbe ndani ya basi letu kuna "kurutu" amejichanganya badala ya kupanda super Feo namba 5 amepanda namba 3 na siti aliyokalia imeuzwa kwa mtu [emoji849]sasa si masoja wakasimamisha basi letu na kuanza kukagua ni nani amekalia siti ya abiria, tema sana mkwara pale lkn jamaa kabana tu[emoji38][emoji38] ebhana mpk wanakuja mpata tumeunguza kaa nusu saa hivi jamaa wamepanik alikula makofi ya kutosha pale + mabuti na ngumi kaa 2 hivi hadi sisi wenyewe tukakasirika mwenzetu kuwa humiliated na wale bakabaka sema ndiyo hivo nani ataongea wote kmy tunaangalia tu... Tukatoka pale tumerusiwa sasa kuondoka hasira zikaamia kwa dreva tunamfokea "dereva si unaona tumekula muda wa watu[emoji38], Ole wako utembee kama unanyata"... Basi kitendo cha kuongea vile tu tukawa tumekosea bhana dereva alipiga mafuta kari ikawa bati balaa huku sisi tunashangilia tu[emoji119][emoji119][emoji119][emoji23].... Ebhanae punde si punde tukazifikia kona flani kali sana hv kama unakaribia njombe . Kwa anayezifaham hizi kona ni nyingi sio moja na zmekaa vibaya sana yani kona Kali upande bonge la bonde upande bonge la jabali limechongwa kiasi ukikaa dirishani huchungulii kwenye bonde Wala huangalii mbele we ni upande mmoja tu [emoji2]..... picha linaanza kwanza gari nzima ikawa kimya km tumemwagiwa maji, kila mtu anamsilizia dereva tu aamue anachoweza.kifupi tulisarender wenyewe maana hata kumwambia apunguze hatuwezi tunaona aibu wala kumchochea aongeze haiwezekani ule tuliokuwa tunatembelea TU ni kifo tosha, dereva analala na zote kwenye kona....haikupita dk 10 watu wakaanza kutapika karibia gari nzima "kurutu" wanatapika[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Ndugu zangu kwa mara ya kwanza toka nimeanza kusafiri siku ile ndiyo nilipata kizai zai hakina mfano maana baada ya wenzangu kuanza tapika nami nikaanza kujiskia vibaya kichef chef balaa nikaomba nami mfuko wa dharura hali mbaya, mbaya zaidi na ule mwendo nikaanza hisi naishiwa nguvu + kizungu zungu[emoji31]. Kufupisha stor ni kwamba yule dereva hakupunguza mwendo mpk tunaingia stendi ya Ubungo kipindi hcho na nilifika home nikiwa na hali mbaya sanaaa.
 
Back
Top Bottom