Ushawahi kufedheheka (kupata dharura) ukiwa safarini kwenye usafiri wa umma?

Sisi ilikuwa tofauti...dereva wetu ndio alipata fadhaa wakati akiwa anaendesha basi.
Ilikuwa tunatoka Mwanza kuja Dar, yule dereva sijui alikula nini usiku kabla ya safari.
Yaani ilikuwa ni mwendo wa kusimama na kuingia machakani na maji ya chupa.
Basi ilikuwa raha sana, hakuna aliyelalamika kuwa anataka kuchimba dawa wala kushangaa njiani maana dereva akibanwa tu, akishuka nasi tunashuka kujinyoosha, kupunga upepo au kuchimba dawa...tumeingia Dar, dereva yuko hoi maana si kwa kuhara kule njia nzima.

Mbuzi alifia kwa muuza supu aisee.
 
Kawaida nikiwa safarin sipendelei kula njiani, siku moja nasafir mwanza to kibondo kwa mara ya kwanza ile njia nilikuwa siijui kabisa. Sasa tumefika sehemu moja tukaacha rami tukaingia barabara ya vumbi tu aseee basi za kule zinakimbia balaa yaan zile mabonde ni kama hawazioni mzee ilifika hatua nikahisi tumbo linauma balaa kama vile utumbo unataka kukatika, safari ikawachungu natamani nipae nifike mwisho wa safari.
Ikanibidi nimuulize jiran yangu vipi tu karibu kufika, akanijibu bado sana. Hapo na maumivu yakazidi zaidi ilinibid niachie siti nisimame kwa muda kidogo hadi nilivyofika kituo kinachofuata ilinibid ninunue ndizi mbivu nikaweka tumboni angalau nikapata afadhali.
 
Pole saana[emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] usicheze na tumbo aisee
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Pole sana
 
Ilikuwa mwaka 2009 nikirudi St John Dodona Chuoni, nikiwa katika basi la Scandinavia, baada ya kuimaliza Morogoro kwa mbele, tumbo likaanza kuuma, nikahisi kuharisha. Nikamuomba konda wa basi, akaniruhusu, nikaenda polini maana ilikuwa polini na sikuwa na namna, akanipa maji, nikakaa huko kama dakika 1, najua wajua tumbo la kuhara, unahisi kama mzigo bado upo. Nikamaliza nikarudi kwenye gari. Gali ilinidubiri, kutembea kidogo nikabanwa tena, nikasema na konda, gari ikasimama, kwenye siti nilikaa na Classmate wangu wa kike.

Dah safari haikuwa rahisi ila mwisho wa siku tukafika Dom kwa taabu sana. Sitasahau. Sababu ya madhira yote hayo ilikuwa kula kuku katika harusi ya baba yangu mdogo, wale kuku walikuwa kama wameharibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…