Nakumbuka mwaka 2006 natoka Iringa nakwenda Moro nilisafiri na kampuni hiyo,nili pata chakula pale aljazera baada ya mwendo kidogo tumbo likapoteza network nili vumiliaaa hadi nika ona kuendelea kuvumilia nita haribu safari ya wengine.
Nlipo amua kuelekea kwa dereva niombe fair daaa MUNGU mkubwa basi lika anza kumiss dereva bila shuruti kaweka kando niliteremka kwa spidi nikazama chaka nika sevu ngoma tartiiibu bahati nilikuwa na kopo la maji nika jiswafi vizuri.
Walipo maliza kukorokocha safari ikaendelea baada muda tena tumbo lika badilika tenaa,na gari ika zingua tenaa hapo tulikuwa kwenye maeneo wanaishi wamasai pale nika omba kwenye nyumba ingawa kuingia mle toilet ilibidi ni cha gue pa kuka nyaga manake watoto walikuwa wame kichafuaa vibayaa nashukuru nika maliza shida zangu pale.
Toka hapo tumbo haliku zingua tena na gari haikusumbua hadi tuna ingia Morogoro, hakuna mtu aliye jua kama nilikuwa na endesha siku ile sipati picha ninge haribu mambo kwenye basi.