Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Hii ndoa haina hata miaka 5.
Kwa kweli tubakie mabachelol hivi hivi.
Nakumbuka masai dada alikuwa anatafuta sana mume humu na thread.
Akaja kumpata kimasihara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaiyo huyo ni wa humu? Hizi ndo changamoto tusipoolewa tunasemwa

Lkn asimilia kubwa na ya wanawake ndani ya ndoa wanavumilia maumivu makubwa
 
Kuna mvurugano hapo...
Bi mkubwa anataka arudi kambini,inawezekana anapambana kweli aweze kuchukua jimbo.

Ushuri wangu kwako:-
Angalia maisha yako,na mipangilio yako mingi lenga kwa mtoto wako na wewe.
Muda wowote unaweza kuondolewa hapo.
Jaribu kuwa mtulivu na wala usiwekeze nguvu nyingi kwa huyo Mr. na uwe tayari kwa lolote litakalotokea.
Kimaisha na kiuchumi; jaribu kutafuta shughuli za kufanya ili ujiongezee kipato kwa sababu hapo ulipo kuna lolote linaweza kutokea.
 
Pole sana dada! Heri ya mwaka mpya 2020

Suala la mumeo kukwambia nyumba ni ya mtoto linatokana na alichosikia either kutoka kwa marafiki zako au ndugu zako, huenda ikawa unaongelea sana hiyo nyumba na huenda ukawa unaongelea kwa mazuri hauna maana mbaya ya kuwa unaifikiria sana hiyo nyumba. Jitahidi uache kuongelea mali kwa mtu yeyote yule.

Kuhusu kukataa kufanya mapenzi after P nionavyo mimi either anakukomoa baada ya Kukereka aliposikia unaongelea sana mali au ana mtu nje. Endelea kumpenda na muandalie kila kitu kama zamani ila usiongelee masuala ya mapenzi kwa muda wa mwezi mzima au zaidi na uwe unapendeza mara kwa mara especially jioni ili awe anahisi unataka kutoka out, hiyo itamfanya asitoke au awe anatoka huku roho ikiwa juu juu kuwa na wewe unaweza kutoka muda wowote na uonyeshe uko happy!

Ongea na ndugu yake anaekuelewa zaidi kuhusu matatizo yake na onyesha kuwa bado unampenda na unaipenda ndoa yako.

Endelea kupenda mtoto wake na uwe unamuulizia maendeleo yake ya shuleni na likizo wasiliana na mama yake mtoto ili aje tena ku clear hicho kiwingu kilichojitokeza kuhusu kutompenda.

Wish all the best! Be patient kama umeolewa na mmasai huwa wako hivyo kuna ndugu yangu anateswa kama wewe na hapewi hata mia!! Jamaa huwa anaenda sokoni mwenyewe.

Sijawahi kuongelea nyumba hizo topic yeye ndo anazipenda.
 
Nenda insta kamfolow idd makengo utakutana na wenye shida kama yako na wengine zaidi yako hautabaki kama ulivyoenda utajifunza kitu, sijaolewa ila sikushauri uondoke mpuuze na kitanda wanacholala na mwanaye kitandike tena vizuri kama mnalala wote hichohicho weka mwambie mtoto alale katikati, kwa kuwa anahudumia familia hela yako sasa dunduliza ukipata anza kujenga taratibu usimbugudhi, hapo usiondoke labda aondoke yeye.
 
Kwa sisi wakristo huwa inasemwa alichounganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe. Mbili kaa kimya kama unaweza kukaa kimya maana mawazo yatakuua dada yangu. Tuliza kichwa na kwa vile upo mwenyewe usimwambie mtu maana kama atakua mwanaume ataitumia kama nafasi ya kukutaka na kama ni mwanamke atakutangaza mtaa mzima. Mwambie Mungu kwenye maombi yote na muombe uwezo wa kushinda. Trust me sijapitia yako ila matatizo yangu huwa nalia na Mungu na sina tena msongo wa mawazo maana unaweza kukuua bila kutarajia. Fanya biashara zako ndogo ndogo huku ukilipa mkopo wako taratibu, nunua kiwanja jenga. Andika jina la mama yako maana ukiandika lako anaweza kudai share yake siku ya kuachana.
Baada ya hapo msome anaendaje ila pia jiepushe kuzaa mtoto mwingine na yeye. Hii plan itakuchukua hata miaka miwili ila siku unaondoka kwake hataamini. Maana ukibeba mimba nyingine mateso ya mwanzo yatakua madogo kuliko ya pili. Mvumilie usimuulize chochote ila jipange maana hapo hata wakwe tu inaonekana hawapo upande wako. Umebaki na Mungu pamoja na kichwa chako. Fanya uamuzi mwenyewe dada yangu la sivyo utalia mpaka utakua kichaa
Naogopaga hata kumshakia kwa Mungu maana kuna jambo lilimpata acha tu..acha
Yaani basemaga maombi ya mnyonge usikilizwa ila naomba Mungu asimuadhibu
 
kupigwa mswaki kwenye ndoa kunauma Sana. Imagine unasubiri mechi kwa hamu halafu mwenzio anakataa dah hakuna mateso makali kama hayo. Huyo jamaa angekuwa anapasha hata kimoja kwa siku angekupunguzia machungu sana. Pole Masaidada ugwadu ugonjwa mbaya sana
Afu bora mru awe mbali akiwa karibu unakua unahamu afu yeye hana mpango
 
Hapana hajatokea humu.
masai dada nimeona unaishi karibu na shule kwenye hiyo id ya mimi90.
Funga asikirimu zile za mia mia za ukwaju na ubuyu uza huwezi kosa pockey money wakati mengine yanajisort out.
Ukiwa financial haupo poa na mtu anakuvuruga hivo ni hatari zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani ndo nimechanganyikiwa zaidi na zaidi.nimeamua kukaa kimya tu sina namna kwa sasa.
 
Na mimi nimeandika hivyo hivyo!
Wanaume watatuona jeuri lakini hapaana, nyuma ya hizo nyumba za siri kuna siri nyingi saaana!
Laiti wangekumbuka zile akili waliambiwa watumie maisha yangekuwa rahisi sana. Hakuna mwanamke jeuri kwa mwanaume mwenye akili jamani, hayo yote ni matokeo ya ufurushi wao.
Ndoa nyingi zipo kwasababu zina wanawake wavumilivu wa maumivu mengi.
 
Back
Top Bottom