Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Kama ataweza kumpuuza na kukaa kimya hakuna presha hapo nakuhakikishia, labda Kama ataendelea kuwaza kwa nini hapendwi/ hathaminiwi kwa sasa, furaha Ni wewe mwenyewe usitegemee kupewa na hawa wanaume, ajitahidi kuwa mtu wa maombi na kumdhujuru Mungu, naamini atavuka salama.
Hii kauli ya iko siku atakupigia magoti ni siku gani hiyo kumbuka kuna presha kwa ajili ya mawazo hajui lini atafurahia ndoa yake tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa kwenye mahusiano na mtu mwenye watoto kabla yako ni ngumu sana. Birthday yangu ni New Year, huo mwaka nilichukua holiday kazini nilijua New Year na birthday itakuwa romantic time. Khee nimeambiwa wanakwenda sea side
Hukuweka booking kabla
 
Hukuweka booking kabla
Pole na mm Nina mtoto kabla ila naishi naye toka 4yrs old leo yuko form3 tuliyaweka swwa kabla na mama yake likizo moja kwangu ingine kuwa mama yake she has two mamas she told me she is among the lucky child to have two mother..... Sijui kama iko practical kwa wengine
 
Mijianaume mingine khaaa !Apo mtu akitoka nje ya ndoa utalaumu kweli. Ila hiyo kitu ya kusema nyumba ni yake na E aisee sio vizuri kabisa. Watu wakijenga kisirisiri wanachukiwa mambo ndio huanzaga hivi!!!
 
1. heri ya mwaka mpya 2020.

2. Napingana na wanaoshauri “ignore”. akili na roho haijaumbwa hivyo, tumeumbwa kujali, tumeumbwa na remorse, feelings, love nk. na hata hao wanaosema wamekufa eneo hilo, si wakweli kwako na kwao binafsi.

3. You can’t attach whats built in silence. yani una vita kama 100 ivi na kila moja naona ina anzia over nothing or normal things, huwezi pigana kila vita! chagua njia ifwate ikamilike. anza na vitu vidogo, kama, just a peaceful tomorrow! embu focus na kesho tu tuone.

4. Heri ya mwaka tena, ila hii ya kweli. wanasema “peace is not the absence of trouble but its the attitude in the midst of problems”. kubali kwanza rohoni huu ni mwaka mpya uenda na attitude hio.

Kwa ufupi, decide and become!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yaani hata mimi nasema niwe na ujasiri tu wa kuignore mambo yake ila nahisi ninampenda ndp maana nasumbuka
Too much of anything is harmful. .si unaona alivo take advantage? ? Kuna mahala Hawachi amesema " kwenye mahusiano/ ndoa kuna sehemu inatulazimu tuwe katili tu inapobidi. . No wayy


Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masai dada jipe raha, muhimu hulipi kodi na pesa ya kula anatoa na hakupi physical abuse.
Kuwa kimya usiongelee lolote wakati watu wanajadili ya kufanya hapa.
Mumeo ana mentality ile wewe ni mama wa kambo.
Nikitulia nitarudi tena kushauri hapa nipo juu juu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
My dear abuse is abuse no matter it's form...kua abused sio lazima physically. Huyo mume ana mu abuse emotionally,mentally and financially....which in my view is far worse than physical abuse.Why?Because in my opinion ukiwa abused physically unaweza kujitetea kwa kurudisha mapigo (if you can)na ni rahisi watu kukutetea kwasabu watakuona na majeraha.

Financially,mentally and emotionally ki Africa sionagi hata can it's considered abuse.Matokeo yake mtu anakua na stress mpka anakufa au anaishia kucheat,kuugua na kama anakua abused financially ndo anajenga na kufanya mambo kwa siri .
Maasai dada huyo mume anaku abuse...he is a sadist the more you beg him for attention the more atakuumiza coz hajali hisia zako.
Nawaambiaga watu Life is too short ...live a life that you're content with and never regret!!! Create your own happiness....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sipo after mali dear...ndo maana nilipambana na ninapambana...
Mkuu, as long as anahudumia familia, wewe mambo yote yapuuze. Focus maisha yako na wanao. Kikubwa ukipata pesa anza ujenzi wa nyumba yako jina andika la mama yako, hati usiweke nyumbani mwako. Pia hakikisha mama yako anaandika usia na kusainiwa na ndugu na mwanasheria kukurithisha nyumba hiyo wewe peke yako ili huko mbele ndugu wasijegombea kusema mgawane wakidhani ni ya mama au wengine kulazimisha kuwa ni ya mama huku wakiwa wanajua ni yako.

Mheshimu mumeo, komaa kuhakikisha unapata haki yako ya ndoa, relax. Sheria ipo wazi, chumo lolote la ndani ya ndoa ni la familia, so mumeo hana chake. Ila hakikisha hati haiandikwi mtoto wa nje bali jina la mtoto wa ndani au jina la mke na mume.

Mali ni vitu vya kupita, tutaviacha duniani. Kipekee kabisa nakushauri jitihada kubwa wekeza katika kuimarisha mahusiano yenu kwa kupuuza baadhi ya mambo yake ya kipuuzi na kufanya mambo yanayowaunganisha na kuwaleta pamoja. Usiwaze sana juu ya mali (nyumba), amini nakuambia huko ni kufukuza upepo, ni ubatili! Focus kuimarisha mahusiano yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
masai dada,

Pole sana Najua unapitia wakati mgumu, ila mie naona bado kuna mwangaza. Naamini mumeo anakupenda sema hajali. Nimefurahi pia kusikia kuwa binti wa mumeo unaishi naye vizuri . Ushauri wangu, simama uiombee ndoa yako na familia yako kwa ujumla. Iombee sana ndoa yako bado ni changa sana kwa wewe kutaka kutengana. Watoto wako watateseka bure. Pray and never stop praying. Mungu ataleta upatanisho.
 
Back
Top Bottom