Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

My take on this, mume wako anakuelewa na anakupenda sana tu, ila kaamua kukunyoosha kidogo.
Jambo la msingi ,tafuteni namna bora ya kumanage hizo conflicts zenu, either kwa kushirikisha professionals au wazee wenye busara.
 
Wiki 2 bila tendo la ndoa ni nyingi za kulalamika JF?
Hadi mtu mzima amelalamika; basi kwake ni tatizo. Hapa hatu-generalise kwa sababu binadamu hatufanani; wengine kumaliza hiyo week tu ni mtihani especially wanapokuwa pamoja. Afu alisema week mbili; hatujui kama iliishia hapo kwa week mbili au inaendelea hadi lini
 
Basi mwenzio nilijifanyia assumptions zangu tu lol. Nikasema kwa situation aliyonayo hadi ananza na kuumwa now kisa stress sidhani kama hata kama ana hamu ya tendo. Though it will reach a time atarelax kidogo so hamu zitarudi tu afu ndo hivyo mume analala naye daily; mwili u dhaifu nao. Sasa sijui aendelee kujiombesha dudu la yuyu au asubiri hadi siku akipewa offer mweeh. But ikifika stage tendo la ndoa limekuwa kitendawili na yeye analihitaji haswa; ataamua afanyaje of coz itabidi afanye maamuzi magumu tu. Siwezi kumshauri achepuke though kwa sababu atakuwa ameongeza petrol kwenye moto and cheating sio hata temporary solution; ni kujichimbia kaburi. Ni dhambi itakayomzalia mauti

Btw nikawa najiuliza kitu moyoni mwangu hapa; mtu mwenye situation kama hii; je asiongeze mtoto kwa sababu mume haeleweki na hata yeye uchumi wake haupo stable for now? Au akishakuwa stable aongeze watoto atakaoona yeye binafsi ataweza kuwatunza? Maana wanawake wa kiafrica tuna ile notion kwamba; kwanza ni mume wa ndoa lakini pia hatupendi kuchanganya mababa kwa watoto wetu (naamini bado ana ndoto ya kuongeza watoto wengine). Your general opinion please
Sasa sijui aendelee kujiombesha dudu la yuyu au asubiri hadi siku akipewa offer mweeh.


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] walah we mtoto umejua kunichekesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF sio sehemu salama ya kuchukua ushauri unaoenda kuamua maisha tako. Huku ni sehemu salama ya kutua mizigo uliyoshindwa kuitua uraiani tu ila sio utatuzi wa matatizo kama haya.

-Humu utashauriwa na watu walio-single vijana wa kiume na wake ambao bado wanakula kwao.

-Huku utashauriwa na wanawake wasio ndani ya ndoa walioumizwa na wanaume kibao kilichobaki mioyoni mwao ni mwanaume nini bwana. Waogope saana hawa.

-Huku utashauriwa na wanaume walioshindwana na wake zao kwasababu zao wazijuayo wenyewe.

-Huku utashauriwa na single parents hasa wanawake.. hawa kamwe hawawezi kukupa ushauri wa kukujenga..hawaamini katika ndoa wengi wao.

Tafuta watu walioishi kwenye ndoa miaka na miaka na wanaojiheshimu kwenye jamii yako wapo wengi tu. Waeleze A- Z ya mkasa wako au kama wamekuwa wakiyashuhudia utapata mawili matatu ya kuchukua. Wao wanamjua mmeo ni mtu wa namna gani na wanakujua wewe ni mwanamke wa namna gani.

Ila hapa unatuomba ushauri kuntu kama huu tusiokujua tutasema nini? Hatumjui mmeo tutasema nini? Hili suala yapaswa uwajue wote kwa undani ndipo utie neno. Ndiyo maana nikauliza kwanini unahisi mmeo alianza kubadilika???
Ukiniuliza; the right person kumwomba ushauri ni Mungu tu + watumishi wa Mungu. Sisi wengine wote; regardless of status zetu; tutakupa ushauri kutokana na tunavyojisikia. Hata hao wenye miaka 50 ya ndoa, sio kwamba wamepitia exactly anachopitia na sio kwamba wana stamina sawa ya kuhimili changamoto hiyo. Viatu vyake ni vya kwake peke yake; yeye ndo ataamua afanyaje kwa sababu ndoa yake ni yake haifanani na ya mwingine na yeye ndo anayeiishi.

Afu miaka mingi ya ndoa haimaanishi mtu amepitia experience zote; tena siku hizi majority ya wanandoa mioyo imeshakuwa ya baridi; wanahesabu tu siku pamoja; hakuna cha furaha ni kupeleka tu siku pamoja; watakushauri nini positive?

Mtu yeyote hata aliye single anaweza kukupa ushauri constructive; ni wewe kuchanganya za kuambiwa na akili zako. Mfano akikwambia "muombe Mungu tu", hutomsikiliza kwa sababu ni single au?
 
Mtaendelea kuchepuka bila sababu ya msingi...
ama pia hujasoma nilipomwambia HS ya kuwa inajulikana wanawake tunauwezo wa kusurvive muda mrefu bila kufanya mapenzi, na sifikirii ni sahihi wewe kudhani kudai haki ya kufanywa after two weeks ni ‘nymphomania’ na je ni dhambi kuwa na nymphomia?

hujajibu maswali yangu bado.
 
Inciden
Pole sana Masai Dada!
Kwa kina kabisa nimeelewa na kuguswa sana na tatizo lako. Kubwa babisa ni ni ule ukweli kuwa wewe ni mke halali wa ndoa na ndicho kimepelekea wewe kujitoa kwa moyo wako wote kuihudumia nyumba yako na kudumisha upendo ndani ya ndoa yako. Ni una ndoto na malengo makubwa juu ya familia yako.....mume, mtoto na wewe mwenyewe..... na ndiyo maana umetafuta hata mikopo kusaidia ujenzi wa nyumba.
Sina hakika sana japo natamani kusikia historia yako na mwenza wako namna mlivyoanza mahusiano na hatimaye kuingia kwenye hiyo ndoa. Hili kama nikilifahamu linaweza kunipa picha pana ya aina ya mahusiano yenu na nini kilipelekea hadi kuingia kwenye hiyo ndoa. Ninachotaka maanisha hapa si kwa nia mbaya bali kutengeneza njia ya namna gani kugundua tatizo lilipoanzia na hapo unaweza kupata chanzo sahihi cha kuanza kulitibu.
Nashawishika kusema huenda kuna maqmbo yako nyuma ya panzia na hivyo kuzuia hata watoa ushauri wakatoa ushauri wa kuweza kutibu hili tataizo. Mambo yanayoweza kuwa nyuma ya panzia ni mf uwiano wenu ki haiba......mnafananaje urembo wako na utanashati wake...... Mali anazomiliki yeye na zile unazomiliki wewe...... viwango vya elimu zenu nk. Haya ni mambo muhimu sana japo unaweze kuyaona si yamsingi kwa kudhani tu mwanaume vile alisha kubali kufunga ndoa na wewe haya si muhimu.
Wanaume tunatofautiana mambo mengi sana. kuna mwanaume anaethamini mahusiano yake yaliyo halali mbele za mungu bila kujali aliingia mahusiano hayo na mtu mwenye viwango gani kwa chochote kile katika uumbwaji wake huyo mwenza na vile avimilikivyo. Lakini pia uwezo wa kujitambua kwamba umekuwa nani baada ya kuingia kwenye ndoa na ni kwa jinsi gani kuchukuliana na mke wako kwa nyakati zote. Nachelea kusema wapo wengi tu wenye utambuzi mdogo kabisa kwenye haya mambo. Sitaki kumshutumu mumeo moja kwa moja lakini inaelekea kwa maelezo yako mume ni tatatizo/cahanzo cha hili tatizo maana wewe umekuwa ukumshauri mambo mengi kwa busara kubwa lkn yeye anabisha tu sababu ni mwanaume au sababu ya hadhi yako kama nilivyoeleza awali hawezi kukusikiliza.

Kwa uchache tu niseme wewe ni mke halali wa hiyo ndoa.....japo sina hakika ya imani gani.....lkn inatosha tu kwa mujibu wa sheria za nchi ambazo ni supreme mbele ya imani ninyi ndiyo wamiliki wa hizo mali hususani nyumba japokuwa huyo mtoto wake anaweza kuwa na sehemu na si umiliki wote kama anavyotaka kukutisha. Labda awe alijenga hiyo nyumba na huyo mwanamke mwingine kabla ya kukuoa japo pia si kweli kwa mujibu wa maelezo yako. Mumeo atakuwa na hulka ya kuongea na kuropoka aidha akikwazwa au kwa nia ya kutaka kukutocha tu ......sadist.... japokuwa ayaongeayo yanakuumiza. ushauri wangu tumia busara zako japo ziwe na kiasi kwa kutoruhusu maneno yake kutengeneza kidonda moyoni mwako. Jaribu kutafuta furaha itakayokufanya uwe huru hata pale anapotafuta kukuumiza. Atakapokuona umejawa amani na huumizwi na makwazo yake ndipo atagundua kuwa kumbe kazi aifanyayo ni bure na hakika atatafuta namna ya kurudi kwako na kukupigia magoti.

Utanisamehe nimeandika kwa haraka sana maana watu wamejaa mlangoni pa ofisi yangu wakihitaji niwahudumie kwa sasa. Nikipata muda nitakushauri vizuri zaidi na hakika faraja itakurudia tena. Pole sana na Mungu akupiganie.
Incidence niliyoiona pale juu, Masai Lady, alikuwa mpweke almost weeks, na kwamba inaonekana jamaa ameanza tabia ya kudu na mkewe yeye akipenda, wkt mwanamke akitaka jamaa hana muda, kwa kifupi jamaa hamjali mkewe kwenye kulila tunda, ama wakati mwingine jamaa hajali mazingira ya kula na kuliwa, kidu na kudukuliwa, mahaba na mahabuba jamaa hana time.

Sasa kisaikolojia jamaa amediss mkewe, According to auther Masai girl, mumewe anatoa mahitaji ya nyumbn ni sawa na tukisema anaweka kodi mezani. Swali ni kwanini hajali!! Anawezaje kulala na mtoto wa 7rys na ameshauriwa wamtenge kwa kuwa kiwasha BBC usiku mtoto yupo haifai,sio maadili, masai aliendelea kumshauri mumewe, huyu jamaa kiburi anakipata wapi??

Mrs anatakani mechi mchana jamaa hadi atake yeye na wakienda wakimamanua, jamaa akimaliza kuchochea moto ukiwaka akitema mate amemaliza, masai anavumilia.

Mm nikasema, kwa tatizo la masai kulalamika, mara ndg wa mumewe wanakaa tu ndani, wifi ake anakaa tu, anakula tu, analala tu, nimeamua kama mzanzibari nirudi upande wa muungano, niangalie maeneo yakukubaliana ktk muungano wa kuwa mwili mmoja

Nimebaini

masai ni mchoyo
Masai anaangalia nani yupo ndani
Masai ananyooshea vidole raia wa upande mwingine wa muundano
Masai akadukuduku
Its as if masai anatamani wawe yeye na mr wake wawili tu ndani, kwani muungano unasemaje, mjiwa mwili mmj mfanyeje ndg wa pande zote wanapowatembelea, kwenye ndoa yao kuna beef la kutoku

Kwenye ndoa hakuna kosa kubwa kama kutengwa na wakwe. Ndg wa wakwe, kubwa ni kwamba tafuta mbinu ya kujenga uhusiano mzur na mamake au babake mumeo, wajomba zake nk

Hakikisha jamaa humuachii nafasi hata kama aanajipa moyo nyumb sijui ya nani, si kweli, kisheria ni yenu wote. madam umeweka jasho lako, usisusie nguruwe shamba lako..watalila
 
Mkuu nilishasaligi huko nyuma mpaka nikaona acha nikae tu labda uenda ndo Mungu kapanga hivi
Daaah pole sana ila usikate tamaa sijui kwa nini mapenzi yana mambo ya kijinga ukimpenda sana mtu anazingua hovyo mpaka kero ubayq ni kwamba unavyozidi kujishusha ndio anazidi kuzingua kiukweli itachukua muda saana mpaka mkae na muelewane sana kuna vitabu viwili vinaweza kukupa idea ufanye nini japo vipo kwa kiingereza
 
Daaaaahh umeongea kwa hisia Sana hadi nimeumia kwa kweli pole Sana Dada angu

Ninacho weza kukwambia ni kwamba huyo ni mmeo hivyo usifikilie kumsaliti ila fikilia kumuweka karbu Zaid na Zaid haijalishi itakugarimu kiasi gani kwauda wako na kwa hisia zako but hakikisha una fanikiwa katika hili

Unaweza kuomba nafasi ya kutoka out ukiwa wewe na yeye tu hapo nenda kamuoneshe jinsi gani una mpenda na hauko tayar kumpoteza mpe mapenzi kwa hisia za ndani Sana shoe him how worth he is then baada ya yote mwambie you need a peaceful life na yeye ndie mwenye peaceful life kwako hivyo asikuumize tena

Pia katika out yenu akiwa kwenye mudi nzuri ongea nae juu ya future yenu kuhusu mwanao na huyo na mwanae yule mwambie wote ni wake na wote wanajua yeye kama baba yao hakuna mwingine Zaid yake hivyo ni bora kujenga future sawa kwa wote




Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mara nyingi mambo huwa hayaendi hivyo yani binadamu huwa tunahangaika sana na vitu ambavyo hatuna so ukitaka kumuoneshw yeye ndio kila kitu ndio unaharibu kabisa ni ngumu sana kunielewa
 
Pole sana mpenzi. Kama mtu hajapitia unachopitia anaweza fikiri ni story tu kama za Iddi Makengo ila kiukweli haya mambo yapo na yanaumiza.

Kuna muda najikuta najipongeza kwasabu sikufikiri kama maumivu yangu yangeisha na ningekua hivi nilivyo leo.
Kama bado unaipenda ndoa yako fight na pambana hadi isimame na irudi sawa.

Mara nyingine kum-ignore na kupambana kivyako inaweza saidia kumrudisha katika mstari.
Usiishi kwa maumivu kwasabu ukiumia na kukosa furaha itamuathiri mwanao.

Ukishindwa kumbadilisha basi kubali kua imeshindikana na focus on your life n child.

Praying for You.


Sent using Jamii Forums mobile app
This is the best comment ever
 
JF sio sehemu salama ya kuchukua ushauri unaoenda kuamua maisha tako. Huku ni sehemu salama ya kutua mizigo uliyoshindwa kuitua uraiani tu ila sio utatuzi wa matatizo kama haya.

-Humu utashauriwa na watu walio-single vijana wa kiume na wake ambao bado wanakula kwao.

-Huku utashauriwa na wanawake wasio ndani ya ndoa walioumizwa na wanaume kibao kilichobaki mioyoni mwao ni mwanaume nini bwana. Waogope saana hawa.

-Huku utashauriwa na wanaume walioshindwana na wake zao kwasababu zao wazijuayo wenyewe.

-Huku utashauriwa na single parents hasa wanawake.. hawa kamwe hawawezi kukupa ushauri wa kukujenga..hawaamini katika ndoa wengi wao.

Tafuta watu walioishi kwenye ndoa miaka na miaka na wanaojiheshimu kwenye jamii yako wapo wengi tu. Waeleze A- Z ya mkasa wako au kama wamekuwa wakiyashuhudia utapata mawili matatu ya kuchukua. Wao wanamjua mmeo ni mtu wa namna gani na wanakujua wewe ni mwanamke wa namna gani.

Ila hapa unatuomba ushauri kuntu kama huu tusiokujua tutasema nini? Hatumjui mmeo tutasema nini? Hili suala yapaswa uwajue wote kwa undani ndipo utie neno. Ndiyo maana nikauliza kwanini unahisi mmeo alianza kubadilika???
Mkuu, uko sahihi 100%
 
Ningekua nimesimama kiuchumi hata kesho ningeanza upya.
Inaumiza sana kuishi na mtu asiekupenda ila wewe unampenda ni bora na wewe mapenzi yawe yameshaisha
Ukiweza fanya nje na mtu hata mara moja tu itakata hilo wenge juu yake looote ama litapungua sana
 
Asante sana..siwezi kutoka nje ya ndoa

Ila sasa unajua binadamu tupo tofauti tulivyoumbwa yaani mimi ni ile type ya siwezi ku ignore kabisa hata kama nikinyamaza nitaingia chumbni na nitalia sana.

I wish niwe na uwezo huo nahisi naweza kusogeza siku mbele maana naona mambo yamenilemea sana.
Ushauri nilimuomba mama yangu ki ukweli huwa anasema nipambanie ndoa ila mimi siwezi kabisa.naona nimeshindwa kuhold on..nazipi kupata maumivu tu kila uchao.
Ndoa usiache its not worth it mana huko nje nako ni tabu tu
Pambana ndani humohumo
Low key tu
Am sure wapo wanaume wanaokutongoza choose one fanya siku moja tu utaniambia
Nyumbani keep low profile

shida kwny ndoa hizi bwn
Unaweza kuwa bize na uaminifu ama uvumilivu ila huo uaminifu mwenzio hauhitaji
Be selfish smtimes ts about you not him
Asijue wala usimdiss potezea tu
Ukirudi home angalia mtoto pika weka nyumba yako sawa, lala
Akitaka mechi toa
Asipotaka pia sawa ushatoa nje huna ukakasi maisha yanaenda utasahau tu utarudi kuwa sawa wala hutojali abt him na hutoumia
 
Kuna kesi zinazohusu hisia kuzitatua kunahitaji uwe na hekima sana maana hapo hatuongelei kitu kingine tunaongelea moyo unaotaka faraja na pumziko.

kesi za namna hii kwa muhusika kama wewe Masai dada,najua unampenda mume wako sana na ndio mana hadi leo hujapata hata wazo la kudanganyia toto umsaliti,hiyo inaonyesha jinsi gani umekwiva kwenye haba na mumeo.

sasa kwa case hii mpk umeifikisha hapa yaonyesha unahitaji pumziko,na hili pumziko ili lisije kwa kudhuru mtu yeyote (hasa mwanao na wewe) nashauri ufunge macho ufanye hiki ninachoenda kukushauri.

Nenda mahakamani,elezea lengo lako lakutaka kuachana na mwanaume Mumeo ataitwa Mtatenganishwa kisheria,kuhusu nyumba ambayo deni lake bado unalilipa itauzwa hiyo nyumba kwa AMRI YA MAHAKAMA kisha pesa zita clear deni na amount itayobaki mtagawana pasu kwa pasu.

Amount utayopewa na mahakama itakua ndio kiinua mgongo chako cha kuanza upya maisha yako hta kama utaanza ktk kupanga its ok as long as upo kwako na moyo wenye amani.

Ambacho sitaki ukifanye kwa sasa ni Kujiingiza tena kwenye mahusiano na mwanaume yeyote simama kwa miguu yako mwenyewe nakuhakikishia hautaanguka tena kwan umeshajua makosa uliyapata wapi.

Ukifika muda sasa umeshaimarika na unaiona future yako sasa ruksa kutafuta yule umtakae ambae una uhakika atakuja na kufukia mashimo na si kuongeza mashimo na majeraha (kuwa makini eneo hilo)

ila kwasasa namalizia kwa kurudia tena Ukiufata moyo wako ukaendekeza mapenzi mazito juu ya mume wako,nakuona utakavyoenda kufa kwa kujiua au kugongwa hata na gari barabarani kisa tu ni mawazo.

Vunja hiyo ndoa mahakamani,Start again.

Asante na pole sana masai dada
 
Run dada run

Ila.tulia

Jipange kiuchumi

Kisha sepa

Huna mume hapo una bazazi tu

Tena ashukuru huchepuki


Anyway usirudie tena kukopa kumpa.mwanaume regardless ni mume au boyfriend

Na ndio.muelewe kwa nini baadhi ya wanawake hujenga nyumba zao kimya kimya

Ila kiufupi hupendwi

Jipange kuishi kivyako

Huyo sio mwanaume pekee duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom