drugdealer
Senior Member
- Nov 8, 2024
- 133
- 245
ngoja tumsubilNiliitwa nikaitika na sasa nimelowea...nimesoma zoteee ni nzuri na zinavutia nasubiri muendelezo...
nakazia, kujibizana na hawa viumbe ni kujilisha tu upepo.achana na hao jamaaa story ni nzuri sana tunajifunza mengi hongera sanaaaa ,Endelea kushusha vitu mkuu
Mwana kulitafuta πS3 epi 8
Basi bana maisha yakaendelea hapo G tunawasiliana tu ila si kama mwanzo Kwa machale tu na huku kwangu wakawa wamekata mguu nadhani ni kwa maelekezo ya mama mkwe, nikiwa nataka kuwaona mi ndo nakua wa kwenda nawasalimu naondoka zangu..
Ikapita kama mwezi Kuna siku nipo kazini mama mkwe anapiga anasema nimtumie Hela ya nauli Kuna mahali amepata Binti wa kazi, basi nikatuma zikapita kama siku 2 Binti wa kazi akawa amekuja, hapo Sasa nawaza mama mkwe atakua kwenye mkakati wa kunipiga pini kabisa nisije nikapata nafasi ya kua na G tena huku kama ilivyokua awali, nikasema hapa hakijaharibika kitu....
Muda ukaenda yule dada kaanza kuzoeana na mtoto ikafika wakati G anaweza kupata muda anatoka tukaonana ila sikuwahi kumruhusu kabisa aje kwangu maana mama mkwe alikua anapajua nikasema hapa niwe makini huyu mama kashahisi kitu anaweza kuja kunipiga ambush....
Fast forward.....
Penzi na G likaendelea hivo hivo kiwizi wizi tu hatukupata changa moto yoyote hapo katikati, hapo naye Sasa kaanza kunizoea sio kama mwanzo mnaweza Sasa mkakaa mkaongea mkacheka yaani kashakua huru, na mi nishanasa hapo nawaza huyu simuachi hata kikitokea nini
Matokea ya form 4 yakaja kutoka bahati mbaya hayakua mazuri Kwa upande wa G,ila nikawa nae karibu namwambia asijali Kila mtu kapangiwa njia yake katika maisha, ukiona huku pamezibwa ujue Kuna mahali pengine unapaswa upite, basi nikawa namshauri atafute tu chuo achague kitu ambacho anataka kufanya aende kusomea, akaniambia sawa ache niwaze ntakujulisha, hapo mama mkwe Sasa tukawa tunaongea Sana kuhusu swala la G ukizingatia mama mkwe ni mtu hakua na exposure Sana hivo akawa ananitegemea mimi Sana Sana kwenye ushauri
Zimepita kama wiki 2 siku nipo na G ndo ananiambia kama utaweza nitafutie tu mimi kazi yoyote nijishikishe kwanza mi naona mambo ya shule ntaenda kupoteza tu pesa huko, basi nikawa namshauri pale maana Kuna chuo nilishaanza Anza kuulizia nikawa namwambia asikate tamaa Bado ni mdogo awaze kufanya shule kwanza, ikaenda hivo hivo nae mama yake sio mtu wa kujali Sana akawa ananiambia huyu kama utaweza mtafutie sehemu yoyote apate kazi tu maana naona mambo ya shule ni kama hataki tena
Nikashauri wee mpaka nikachoka, badae nikaja mtafutia kazi Kuna mdada mmoja nilikua nafanya nae kazi alikua na cash point mjini kama viwili baada ya kumuomba Sana badae akamchomeka sehemu Moja akaanza kufanya kazi Sasa huko, hapo mama yake ana furaha tu anaona Bora hata mwanangu amepata mahali akiamka anajua pa kwenda
Akili za kitoto Sasa, hapo G anaanza kunishawishi afanye kazi hata miezi minne Ili aje amuombe mama yake aende kupanga Ili tuwe free Sasa, nikamwambia hapana we endelea tu kukaa nyumbani kwanza mambo mengine tutapanga huko mbeleni, na mtoto ashakuzoea Bora hata hio jioni mnakua wote ukirudi, maana hapo Sasa nawaza haya mambo ya mapenzi tutakuja kujiachia Sana itakua rahisi mama mkwe ajue jambo.
Hivo Sasa mara nyingi G akitoka kazini maana wao wanachelewa lazima tutakutana tu ndo aende nyumbani, maisha yakaendelea ivo ivo pakawa hapana shida Kila mtu ana amani.
Shetani Sasa nae sio ndugu Yako
G mzunguko wake wa hedhi nilikua naujua vizuri na yeye nilim downlodia application kabisa iwe inampa alert, Sasa tukaanza ujinga mmoja, siku ambazo ni za hatari tukaanza kutumia withdrawal method, Ile nikitaka kumaliza namalizia pembeni, kumbe hii njia ni ya kijinga Sana, nilikuja kuelewa Kwa gharama kubwa Sana
Kuna siku nipo na G hapo yeye ana kama miezi 6 kazini, na mwanangu hapo kashaanza kwenda shule, Kuna shule ioo jirani basi wanampeleka kanacheza cheza saa 6 anamfata huyo dada wake wa kazi, Sasa hio siku nipo na G ndo ananiambia ni kama hajaona siku zake lastly, aisee sikujibu kwanza kitu chochote nilihisi kama nimepigwa shoti, tukajipa moyo pale kua Kuna circle inacheza ye atulie kwanza, nikawa Sasa Sina Raha nimekua mtu wa mawazo yaani Kila siku namuulizia vipi, umeingia period??? Jibu ni hapana.... Ikaenda mpaka siku namwambia tafuta mahali ukacheki, jibu likaja positive ana mimba
Maisha yangu yakawa magumu ghafla hapo Sasa Nina mawazo Sina Raha, tukaacha na mambo ya kusex hapo na yeye Kila siku ananiambia ananitegemea mimi nimwambie tunafanyaje, kiukweli mimi sipendi na sio muumini kabisa wa abortion ila hio siku Kila nikiangalia option nilizonazo, na madhara ya maamuzi yangu naona Sina namna hapa ni abortion tu,katika kitu kilichokua kinanipa mawazo nakumbuka kipindi tupo chuo Kwa kuskia au kuona kabisa, Kuna cases nyingi za wadada walifanya abortion zikaenda tofauti Sana,wengine waliumwa mpaka kupostpone( kuahirisha) mwaka wa chuo, chuo mimba zinatolewa Sana hivyo nilishapata story za madhara huko
Nikawa nawaza Sasa ikienda vibaya mtoto wa watu akapata shida, tofauti na kuogopa reaction za Rachel na mama mkwe ila hapo na mimi Nina feelings nae namuwazia tu basi namuonea huruma
Upande mwingine nawaza timbwili la Rachel, huyu mama mkwe ataniona mi ni kiumbe wa aina gani? Mama yangu Sasa na sister ndo balaa wakiskia ndo itakuaje Sasa, watu walinishauri nikate mizizi na hii familia, wakafurahi hata walivyoskia tumeachana na Rachel,wakanishauri kikubwa niangalia mwanangu, waje waskie tena nimejisimika kabisa kwenye hii familia dah itakuaje
Nikapima option zote nikaona abortion is the way to go, siku nikamuita G nikamtuliza kweli kiakili tukaongea mambo mengi badae ndo nikampa hili wazo, kwanza akaruka mita mia, akaanza kulia, mara Ina maana muda wote ulikua unanchezea tu, huwezi kuniambia unanipenda alafu uniambie nitoe mimba, hapo akaongea wee maneno mengi mi hapo sielewi kabisa, namuulizia Sasa mama dada wakijua, akasema potelea popote ndo ishatokea Sasa, ongea Sana pale wee ila mwisho wa siku tutakosa muafaka badae akaondoka tukasema tutaongea siku nyingine, hapo hakuna Cha sex Wala nini kwanza mi mood ilishakata kabisa
Sasa bana kashaondoka hapo nakaa kama nusu saa naona G kanitumia sms ambayo kwangu mimi nilitafsiri kama ni ya dharau kwanza maana tangu nijuane nae kwanza ananiheshimu na kuniogopa, pili ikiwa na vitisho ndani yake, kaandika
"Ni wakati Sasa sahihi wa kusimama kama mwanaume, mwanaume hukabili si kukimbia changamoto, tafuta namna ya kujua unafanyaje na ukiendelea kuniambia nitoe hii mimba hizi habari ntazifikisha Kwa mama mwenyewe maana naona kama we unamuogopa Sana"
Fu*ck, nikasema " heeee tena "
Wanaume tumeumbiwa mateso ya tunia kupitia kichwa cha chiniMwana kulitafuta π
Mnakiendekeza π G wa Form Four anakushinda nini?Wanaume tumeumbiwa mateso ya tunia kupitia kichwa cha chini
Tatzo mkishafanya sex akakuzoea power ya kumcontrol inapungua inabaki kujihami tu. Btw Bw.patrick angekuwa mtu wa afya ilitakiwa ile ameambiwa hajaona siku zake angetake action kumpima na kumaliza tatzo kwa vidonge tu.Mnakiendekeza π G wa Form Four anakushinda nini?
Sio 41 hapo anzia 61 maana kuanzia 20 mpaka 55 kuelekea 60 wote nyegenyege tu, kuna mmoja ana 55 nmekuta kwenye app anatafuta mume ni 55 kwa hio usiseme nyege zina umriMunaohangaika pat alete hii story nikiwacheki kwa makini munacheza na miaka kuanzia 20 had 40.
Ukivuka 41 mwanaume/ke huwezi ukambebeleza mtu akupe story ya namna alivyongegeda mbususu ya grace maana yake utakuwa umevuka enzi za nyenge kichaaa.
Njoo pm nikupee ile zawadi yako ya janaMnakiendekeza π G wa Form Four anakushinda nini?
Hii Epsode imenichekesha sanaaaS3 epi 9
Nikatafakari Sana nikasema hapa nisipokua makini haya mambo yataenda kua magumu unaweza Kuta unataka kukimbia mkoa tena kama Yale Yale ya dar... Ila nawaza Nina option gani? Nikawaza wee... Nikaja na mawazo kama matatu hivi
i) kwanza kabisa ni kumuweka G under my control, kitendo Cha huyu Binti kuanza kunitisha sio Cha kukichekea kabisa, Sasa hapa nafanyaje? Huyu natakiwa mimi ndo nimcontrol mpaka ntapopata suluhisho,either Kwa kumuweka karibu tu(kumbembeleza) au kwenda nae kitemi, hapa nikawaza jawabu likaja huyu Bado mtoto mdogo nikimuendekeza hachelewi kunivua nguo, huyu ntaenda nae kitemi
Ii) hata kama huyu asipotoa mimba, swala la mimi kumuambia mama mkwe is a no go zone! Kiufupi hata iwaje swala la kwenda kujisalimisha Hilo nikalitoa akilini kabisa nikasema siwezi kufanya ivo hata iweje....
iii) hapa Sasa nikajipanga for the worst, huyu akigoma kutoa mimba, nafanyaje? Hapa it's either nishirikishe mtu mzima Sasa akapambane na mama mkwe ila sio mimi kabisa....
Nikaingia kazini nikaanza na mpango kazi wa kwanza(option i)... Kwanza hio sms ya G ya vitisho sikujibu, badae akatuma sms zingine mie nipo kimya tu, akapiga Simu sikupokei kabisa, kesho tena nipo kazini anapiga Simu tu naziangalia, badae nikatoka kazini nikapita kwenye duka lao hapo akaniona akatoka akaanza mbona hupokei Simu dear Kuna shida, hapo nipo serious kiasi, nikamwambia ukitoka tuonane, sikutaka mambo mengi nikaondoka..... Badae katoka kanitafuta nikamuelekeza mahali akaja, akafika sikutaka kupindisha maneno Wala nini, namuuliza sms gani unanitumia Jana? Anauliza ipi? Namwambia hivi kweli tumefikia unanitishia mimi kua utaenda kumuambia mama? Yaani tupo wote kwenye tatizo hunipi hata muda wa kufikiri nafanyaje unaanza kunitisha? Mbona huna adabu siku izi, nikamsema pale akaanza tu kujitetea kuomba msamaha pale kua zilikua hasira... Sasa hapo ndo nikamwambia point black kua mimi ndo mwenye maamuzi ya mwisho, akae atulie mpaka nitakapopata suluhisho, akienda kinyume na hapo atajua mwenyewe Wala mi sitahusika na chochote, hapo nimechukia kweli, nikamwambia "Sasa we ukiona sawa nenda kamuambie mama alafu kuanzia hapo mi sitahusika na chochote mtajua wenyewe, na kwanza atanifanya nini"
Kuona vile akaomba msamaha kweli, akaanza kulia, anasema Ina maana nikitoa hii mimba alafu inakuaje, Ina maana huna malengo na mimi Patrick???
Hapo Sasa napata hasira tu nazidi kumshangaa, malengo tena? Akilini nikasema haya ndo madhara Sasa ya kua na watoto, nikajiambia utavuna ulichopanda
Basi nikamwambia pale akae atulie na kuanzia hio siku ntachosema mimi ndo final sipendi mashindano, na nikamuonya asije tena kujaribu kuntishia, akasema sawa nimekuelewa.... Nikamtafutia usafiri akaondoka.... Kufika akinitumia sms anaomba msamaha tu
Hapo nawaza Ina maana huyu hata hamuogopi mama au dada yake? Anawaza nini?
Anyway option i) ikawa imeisha ila Sasa shida IPO pale pale, nafanyaje? Abortion hapo mwenyewe nipo 50/50 ni kama namuonea huruma, na hata kama nikisema nifanye hivo Bado Kuna uwezekano akagoma pia
siku zikapita kiasi, hapo tatizo lipo pale pale, nina mawazo Sana hapo Sasa mwenzangu yeye hata Hana presha Wala nini.... Utakaa wee utakutana na sms " Leo najiskia kula kitu flani(.....), Huyu mwanao ananitesa kweli"
Dah, hapa naona huyu anachukulia hii ishu kimzaha Sana, mara aniambia aondoke nyumbani akapange alafu hata mama akijua hatonitaja tufanye Siri tu asiseme baba wa mtoto mpaka hapo badae, stupid idea!!!! Mzee wangu aliyetangulia mbele ya haki kila mara alikua ananisihi "hakuna kitu kibaya kama kuahirisha tatizo"
Nawaza hata akifanya hivo ipo siku ukweli utakua wazi, alafu nini? Tutarudi tu pale pale
Sasa na mimi nikawa kama nimeahirisha tatizo, sipati maamuzi, muda ukaenda mpaka mimba Ina kama miezi miwili na sehemu karibu mitatu, hapo Sasa naona kabisa abortion is out of the options, Kila siku namuambia G mama Yako atagundua tu ni swala la muda, nikawaza we nafanyaje......
Kuna siku nimekaa kazini, G ananitumia sms " ukitoka kazini nipitishie chocholate, mwanao ndo anataka ananisumbua"
Nikawaza huyu Hana hata mawazo ni kama anafurahia tu hii Hali, nikasema Sasa hapa mambo yashaharibika ngoja nitafute mtu anisaidie kuumiza akili
Sasa Nina ba yangu mdogo yule tulienda nae kujitambulisha Kwa kina Rachel, huyu ba mdogo ni mission town Sana mjanjamjanja, alafu alikua peace Sana huyu hata kama mpo sehemu mnakunywa anaweza mtongoza mwanamke mbele Yako, yaani tulikua tumezoeana hivyo....
nikampanga kama baada ya siku 3 akawa amekuja mwanza Sasa, hapo sijamwambia kitu, kazini nika activate likizo, ba mdogo kufika nae namjua ni mtu wa viwanja tukawa Kila siku tunatoka tunakunywa story nyingi ila hapo sijamwambia kitu, Kuna siku G akatoka kazini nikamuita mahali tukakaa wote ila sikufanya utambulisho Wala nini mpaka badae G akaondoka akatuacha
Sasa ba mdogo nae huku mwanza hakuwahi kuja tena tangia kipindi kile Cha utambulisho, akaanza utani "mwanangu unajua ku sort,haka ni ka wapi tena? " Nikamwambia mzee we acha tu hapa Nina balaa, anauliza nini tena? Ndo namwambia huyu ni mdogo wake Rachel, nikamuelezea mambo yalivyoenda mpaka kumuambia nilishaharibu
Sasa hapo nipo serious, jamaa akaanza kucheka vibaya mno, mara ananiambia "huo ndo uanamme Sasa, Hawa wajinga tulienda kujitambulisha wakatupiga faini alafu wakatufanyia mambo ya ajabu, hapo Sasa ndo umebalance mzani'
Nikabaki nashangaa,namwambia Mzee acha masihara hii ishu Iko serious ujue, ye anasema kesi ndogo tu hii, akaanza Sasa kunipa mifano kwenye ukoo wetu, mara mbona yule mjomba wako wa mahali Fulani alioa mtu na dada ake, akaongea we anasema ni mambo ya kawaida hapo mi simuelewi kabisa...
Sasa bana tunaendelea kukaa pale nina mawazo jamaa ana furaha kinoma, yaani anacheka tu mi simuelewi mpaka muda tukarudi nyumbani anadai Hilo swala dogo niachie mimi
Zikapita kama siku 2 nikamwambia ba mdogo mi naenda nyumbani nikamsalimie mama, we Baki huku pambana na huu msala, akasema Haina shaka, lengo langu mambo yakitibuka huku nisipowepo, nikaanza mipango ya safari, Kuna siku nikamcheki mama mkwe nikamwambia mama siku ukiwa na muda ba mdogo yupo huku anataka kuja kukusalimu amuone na mtoto, akasema jumapili sitoki mwambie aje atanikuta..... Hapo ba mdogo anasema huyu ni kwenda kumshtukiza tu akijua tutakutana na wale wazee tena, G nikamuambia nasafiri mara Moja Kwa mama ila sikawii basi akakubali kishingo upande, nae hatukumuambia, yaani ikawa kimya kimya hapo nawaza mi niondoke hili bomu likilipuka mi niwe mbali
Ikafika siku nikaondoka zangu, ba mdogo nikamkatia fungu la kupambana na huo msala nikiwa sipo, mama mkwe hapo namkwepa nilimuaga kwenye Simu, lengo la kumkwepa maana ningeenda ingebidi niende na ba mdogo alafu lengo la jumapili lingepotea, hapo nikamuaga namwambia ba mdogo yupo Kuna mambo yake amekuja fatilia jumapili atakuja akasema haya...
Nafika home napokelewa vizuri, piga Sana story na mama nilikua na muda sijafika nyumbani, Ile kufika muda wa kulala tunaagana mara mama ananiambia "naona baba Yako kaja huko mwanza wewe nawewe umekuja huku umemuacha, akili zenu nazijua najua mshaharibu huko"
Nikasema kumekuch
Ukiona hivyo jua amenogewa anatumia njia kukuharash ili ukeleke sisi tukubebeleze uendelee. basi ukiendelea atakuja tena kusoma.Yaani kuna watu sijui mnakua na maisha gani? Mimi nimejiunga jf 2012 hii thread ni ya pili kuanzisha, mwaka 2014 nilipandisha uzi hapa Kuna ipads na computer nilikua nauza kipindi hiko Niko chuo, sijawahi kuanzisha thread tena mpaka hii hapa, mpaka Sasa nimeanzisha threads mbili tu
Lakini hilo gap la miaka 10 sijawahi kupitisha siku 3 lazima ntaangalia jf nini kinaendelea, kuna msemo wanasema ukiwa mjanja penda Sana kusikiliza kuliko kuongea
Na ndo maana hua napita tu naona members wanasemaje hata bila ya kucomment
Unavyodai mtu hawezi kukumbuka mazungumzo ya Miaka miwili? Mi nimeweka ya Miaka 7 nyuma......
Navyofanya kuquote ni kama relevance tu lakini si Kila neno Lina asilimia 100 kwenye kumbukumbu, Mzee wangu alifariki kitambo ila mpaka Leo naweza kukaa
Siku Fanya Kwa kupenda ila kulikuwa na sababu zilizonisukuma kufanya hivyo.Hauna adabu kabisa
Kumaliza vipi mkuu na alikataa abortion? Hapo kitumbo kinakua kumbuka na nikawaza Bora mtu umuambie wewe kuliko aje ajue yeye kwanzaUlijivutavuta sana, hii inshu mngepaswa muimalize wewe mwenyewe na G. Halafu baada ya hapo ndio mngejua way forward kama G alivyokuwa anawaza.
Hahah twende ya 11 sasaS3 epi 10
Mama namjua akianza kuongea hamalizi Leo sikumjibu chochote nikampotezea, kesho yake Sasa nawasiliana na ba mdogo yaani tunapanga mbinu utasema tuko vitani, kwanza akaniambia amefanya mawasiliano Kuna mtu kampata mwanza Mzee mmoja wa kwenda nae, akaniambia yule Mzee wa kwanza tulieenda nae wakati wa kujitambulisha Kwa Rachel hafai, anadai yule ni mlaini Sana hii vita hatoiweza inahitaji makamanda kweli, hapo mimi simbishii kitu chochote nipo kimya maana nilishamuachia msala apambane nao....
Ba mdogo akaja Sasa na idea Moja, operation ya kuua ndege wawili Kwa jiwe Moja....
Akaniambia hapa inabidi tulipue mabomu kotekote ibaki tu kazi ya kukabiliana na madhara yatakayojitokeza, jumapili akienda Kwa mama mkwe na mimi huku nikae na mama nimuambie tu Kila kitu, maana hata nisiposema akasema mama mkwe ni lazima tu atampigia mama, hapo Sasa naona nimeruka nimejichanganya tu, mama yangu namjua ataongea mpaka nyumba ipate ufa, ila nikiwaza msala wa mama mkwe kule naona Bora nipambane tu huku kule ni kwa moto zaidi, hapo Rachel yeye Bado Sasa, nawaza huyu nae hawezi kuacha ipite hivi hivi lazima tu ataleta vita ya aina yake,
Hua sifanyi kitu bila ya kua na plan b, nawaza haya mambo yanaweza yakaenda tofauti kabisa na tunavyotarajia hivo plan b yangu ni kua nikiona mambo yameharibika Sana nifanye mpango mtoto nimlete huku Kwa mama maana nilihofia Rachel anaweza pata sababu ya kumchukua mtoto....... Nikashamleta huku mimi Sasa nibaki nipambane na lolote litalokuja
Usiku wa deni haukawi kufika, jumapili hio hapo, nipo busy na askari wangu( ba mdogo) tunapanga mipango wa mwisho, nikampa idea usiende mikono mitupu nunua zawadi za mama mkwe na mtoto kwanza mpate hata pa kuanzia mkienda, Sasa ba mdogo hii ishu yeye anachukulia simple tu yaani anasema " hii ya Leo Haina Cha zawadi Wala nini, Leo tunaenda uwanja wa vita zawadi za nini tena"
Mimi huku swala la kumuambia mama likanishinda, Kuna rafiki yake mmoja mama mtu mzima Sana tulikua tunatenganishwa na ukuta tu huyu mama alikua mcheshi na simple Sana, nikawa nimeshamuambia majanga yote nikamwambia jumapili we njoo umueleze tu huyu Mzee mwenzako akasema hakuna shaka.........
Hio siku yule mama kafika Sasa home, tumekaa Kaa pale ikabidi mi nizuge nikatoka zangu nimuache Sasa afikishe msala huku, nimetoka nimekaa bar Moja nampigia ba mdogo kujua kafikia wapi, anapokea anauliza vipi wewe uko wapi? Namuambia npo bar hapa natuliza kichwa kidogo, jamaa nae anacheka anasema na si tumepitia hapa tunapiga Moja Moja kwanza hii vita sio ya kwenda ivi ivi
G hapo tunawasiliana kawaida ila sijamwambia chochote asije akavujisha taarifa akaharibu, ikafika muda ba mdogo ananiambia wapo njiani wanakaribia kufika....
Mimi ni nani??
Nikachukua Simu yangu, mama mkwe nikamtupia kwenye blacklist, Rachel nae nikamuunga huko huko.... Hapa nasema mpaka nipate kwanza feedback kutoka Kwa ba mdogo ndo ntajua Cha kuongea nao....
Basi wao wakafika kule hapo tukaacha kuwasiliana, hapo Nina mawazo najiuliza mbona nimejiingiza kwenye matatizo kiasi hiki, upande wa mama Wala siwazi Sana najua tu atasema mpaka nikome, huku Sasa Kwa mama mkwe.... Nikakaa pale yaani navyosubiri Simu ya ba mdogo ni sawa na mtu amepeleka mwenzie uzazi yupo nje anasubiri kuambiwa kajifungua salama...
Nikiwa nashusha bia taratibu pale, mama yangu akaanza kupiga nikawa kimya tu Wala simpokelei, akapiga kama mara tatu mie kimya tu.... Nakaa kama dakika 10 naona sms kutoka kwake
" Hivi wewe hizo akili zako umezitoa wapi , mbona baba Yako hakua na akili kama hizo"
Nikawaza hapa bomu la kwanza lishalipuka...
Sijapata hata muda wa kuwaza ba mdogo nae anatuma sms
" Mzee hii Ngoma nzito, tushachemka huku"