Season 2 episode 1 Mwanza
Huyo mimi mpaka mwanza nikaanza kazi kule na maisha mapya yakaanza, kusahau relationship za dar haikua rahisi ila wanasema muda unaponya na umbali pia ulisaidia, nikaanza maisha sasa jijiji mwanza, kuna mgahawa mmoja nikawa kila siku naenda kula hapo jioni nikatokea kuzoeana na mdada mwenye mgahawa sana, sasa pembeni kuna kibanda kimoja kuna dada alikua anakata matunda anauza pale, nikawa natoka napitia matunda naondoka zangu, muda ukaenda yule dada wa mgahawa alikua ashakua rafiki yangu sana, hapo nishaaanza kuvutiwa na yule dada muuza matunda sasa alikua na aina flani hivi ya shepu, chuchu bado mpya kabisa na sura flani ivi innocent sana, nikaanza mdadisi yule dada wa mgahawani ndo siku akaniambia yule anaitwa rachel( sio jina halisi) nakaa nae ghetto moja
Maisha yakaendelea kuna kipindi nikawa simuoni huyo rachel kwenye matunda sasa, nikaja muuliza mwenzake ndo akaniambia sa ivi yupo nyumbani tu walishindwana bei na mwenye kibanda chake, nikamuuliza kwanini asije akusaidie hapa mgahawani akaishia kucheka tu akasema huyo na jiko wapi na wapi, basi tukaishia hapo, nikawa kila nikienda kula pale mgahawani namuachie yule dada wa pale elfu 10 au 5 namwambia mpelekee mwenzako sa ivi si hana kazi, nikawa nafanya hivo kila nikipata nafasi... Sasa kuna siku nikawakuta wapo wote pale mgahawani nilivyomaliza kula nikamuita rachel nikamsalimia alikua kapendeza kwelikweli na umbo analo,huyu binti nimemzidi miaka 7 so by that time alikua na kama miaka 18 tu hapo, akaitika nikaanza kumtania naona maisha yamekua matamu umeacha kazi, akaniambia wapi kaka yangu nyumbani nakosa hata hela ya vocha, nikamwambia acha zako za kwangu tu nazotuma huwezi maliza kwenye vocha akabaki anashangaa za kwako zipi
Sasa wanawake sijui ni kutopendana au nini, yule dada wa mgahawa kumbe hakuwahi fikisha hata senti 5 wala salamu kwa huyu binti rachel tukabaki wote tunashangaa tu, basi tukabadilishana namba pale nikampa elf 10 mi nikaondoka zangu, baada ya kama wiki nikawafata nikawatoe out tukatembea tembea jijini nikawarudisha badae, sasa akili ikaanza kuwaza huyu binti mbona kama anafaa ngoja nijaribu kua nae tuone itakuwaje
Nikaja siku nikampeleka mahali nikamuambia live kabisa sikumficha kitu akaniambia haya kaka yangu ntakujibu, ikapita kama siku 2 akanitumia sms hapana kaka yangu sitoweza nikamjibu sawa tu wala sikuwaza sana, sasa sijui wanawake hua wanawaza nini, akawa amenikataa ila ye ndo kila muda anatuma sms mi nikawa namwangalia tu, sasa siku nipo na mfanyakazi mwenzangu tumetoka job tumepita mahali tunapiga gambe huyu binti rachel akaanza sana kuntumia sms whatsap nikawa simjibu, baadae akili ya pombe ikanituma ngoja nimrushe roho huyu kwanza ananichukulia poa sio, nikaingia whatsap nikahide watu wote wasione status yangu isipokua yeye na rafiki yake yule dada wa mgahawa, nikazama google photo nikadownload picha moja ya samira(huyu msomali alikua mzuri kweli) nikaweka status nikaandika miss you maa, nikaacha bomu langu lijipikeπ
Baada kama lisaa dada wa mgahawa akapiga simu nikapokea akaniuliza umefanya nini, nikamjibu kwani vipi, akasema nimekuja namkuta rachel analia, nikamuuliza kwani vipi mbona sielewi, akaanza we si umeweka wanawake zako status, nikasema kwani kwani shida gani kwani rachel ni nani kwangu, akaniambia hapana usimfanyie ivo anaumia, nikakata simu nikacheka sana nikajua hapo mtego wangu wa bomu ushalipuka,
Wanakuambia kingaacho sio dhahabu, rachel ndo mwanamke alinifanya huu msemo niuamini kwa asilimia mia