Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Huyu wivu juu yangu umepitiliza maana imekuwa kero sasa. Nikisema nikuorodheshee anayoyafanya mpaka wafanyakazi wenzangu wa kike wananitenga kimawasiliano kwa kuogopa kuvuruga uhusiano wangu na huyu girl, sometimes week ends mchana naweza kuwa sehemu na rafiki au marafiki ila huku nyuma nitafutwa kwenye ma bars yote nisipokuwa nyumbani. Yaani yeye anataka muda wote tuwe pamoja achilia mbali muda wa ofisi tu. Akisikia sms au simu imepigwa tu ye hajui nani anataka apokee yeye kwanza. Hapa aliongea na boss wangu mama mtu mzima aliponipigia simu niliacha ndani jioni mi niko uwanjani nacheza mpira. Baada ya kama wiki mbili kuoita ndio boss wangu akaniuliza huyo mwanamke ninaeishi nae awe na heshima na ajue jinsi ya kuongea mtu na mtu sio wote mahawala wa mumewe. Nilijisikia vibaya sana, alafu yeye kanyuti tu wala hakuniambia lolote.
Mkuu umeliwa na usipoangalia hicho kibarua kitaota nyasi
 
Season 2 episode 1 Mwanza


Huyo mimi mpaka mwanza nikaanza kazi kule na maisha mapya yakaanza, kusahau relationship za dar haikua rahisi ila wanasema muda unaponya na umbali pia ulisaidia, nikaanza maisha sasa jijiji mwanza, kuna mgahawa mmoja nikawa kila siku naenda kula hapo jioni nikatokea kuzoeana na mdada mwenye mgahawa sana, sasa pembeni kuna kibanda kimoja kuna dada alikua anakata matunda anauza pale, nikawa natoka napitia matunda naondoka zangu, muda ukaenda yule dada wa mgahawa alikua ashakua rafiki yangu sana, hapo nishaaanza kuvutiwa na yule dada muuza matunda sasa alikua na aina flani hivi ya shepu, chuchu bado mpya kabisa na sura flani ivi innocent sana, nikaanza mdadisi yule dada wa mgahawani ndo siku akaniambia yule anaitwa rachel( sio jina halisi) nakaa nae ghetto moja


Maisha yakaendelea kuna kipindi nikawa simuoni huyo rachel kwenye matunda sasa, nikaja muuliza mwenzake ndo akaniambia sa ivi yupo nyumbani tu walishindwana bei na mwenye kibanda chake, nikamuuliza kwanini asije akusaidie hapa mgahawani akaishia kucheka tu akasema huyo na jiko wapi na wapi, basi tukaishia hapo, nikawa kila nikienda kula pale mgahawani namuachie yule dada wa pale elfu 10 au 5 namwambia mpelekee mwenzako sa ivi si hana kazi, nikawa nafanya hivo kila nikipata nafasi... Sasa kuna siku nikawakuta wapo wote pale mgahawani nilivyomaliza kula nikamuita rachel nikamsalimia alikua kapendeza kwelikweli na umbo analo,huyu binti nimemzidi miaka 7 so by that time alikua na kama miaka 18 tu hapo, akaitika nikaanza kumtania naona maisha yamekua matamu umeacha kazi, akaniambia wapi kaka yangu nyumbani nakosa hata hela ya vocha, nikamwambia acha zako za kwangu tu nazotuma huwezi maliza kwenye vocha akabaki anashangaa za kwako zipi



Sasa wanawake sijui ni kutopendana au nini, yule dada wa mgahawa kumbe hakuwahi fikisha hata senti 5 wala salamu kwa huyu binti rachel tukabaki wote tunashangaa tu, basi tukabadilishana namba pale nikampa elf 10 mi nikaondoka zangu, baada ya kama wiki nikawafata nikawatoe out tukatembea tembea jijini nikawarudisha badae, sasa akili ikaanza kuwaza huyu binti mbona kama anafaa ngoja nijaribu kua nae tuone itakuwaje



Nikaja siku nikampeleka mahali nikamuambia live kabisa sikumficha kitu akaniambia haya kaka yangu ntakujibu, ikapita kama siku 2 akanitumia sms hapana kaka yangu sitoweza nikamjibu sawa tu wala sikuwaza sana, sasa sijui wanawake hua wanawaza nini, akawa amenikataa ila ye ndo kila muda anatuma sms mi nikawa namwangalia tu, sasa siku nipo na mfanyakazi mwenzangu tumetoka job tumepita mahali tunapiga gambe huyu binti rachel akaanza sana kuntumia sms whatsap nikawa simjibu, baadae akili ya pombe ikanituma ngoja nimrushe roho huyu kwanza ananichukulia poa sio, nikaingia whatsap nikahide watu wote wasione status yangu isipokua yeye na rafiki yake yule dada wa mgahawa, nikazama google photo nikadownload picha moja ya samira(huyu msomali alikua mzuri kweli) nikaweka status nikaandika miss you maa, nikaacha bomu langu lijipike😀



Baada kama lisaa dada wa mgahawa akapiga simu nikapokea akaniuliza umefanya nini, nikamjibu kwani vipi, akasema nimekuja namkuta rachel analia, nikamuuliza kwani vipi mbona sielewi, akaanza we si umeweka wanawake zako status, nikasema kwani kwani shida gani kwani rachel ni nani kwangu, akaniambia hapana usimfanyie ivo anaumia, nikakata simu nikacheka sana nikajua hapo mtego wangu wa bomu ushalipuka,


Wanakuambia kingaacho sio dhahabu, rachel ndo mwanamke alinifanya huu msemo niuamini kwa asilimia mia
Baadhi wenye majina ya Rachel huwa ni shoti hatari...unapigwa huku unabembelezwa, kijana ukanasa kwa "Nashukuru Umerudiiii" 🤣🤣
 
S2 episode 6


Dah nilitafakari sana nikapata mawazo makali sana, nikawaza maisha na Mary kule dar, nikamuwaza Samira, nikawaza nimekuja kuingia kwenye balaa gani tena, uzuri napenda sana kua mtulivu kwenye situation za kupanic mpaka leo ndo niko hivyo, nikawaza sana nikajilaumu nimemtia mimba binti ambae simjui vizuri, mbaya zaidi nishaenda na kujitambulisha kwao, nikawaza sana kuhusu huyu mwanangu tumboni, badae mawazo yanakuja ni wangu kweli au? Yaani nikawa sielewi tu



Nikarudi home usiku kufika napokelewa sina hata furaha, nikampa simu yake akawa kafurahi kweli anasema ngoja nichukue na picha zangu za zamani,mi hapo namchora tu npo zangu kimya, kanipakulia nikamwambia tumbo linauma siwezi kula basi ananibembeleza hapo sina hata hisia wala amani mpaka muda tukaenda kulala, akataka tusex namuambia tu tumbo linasumbua, akaja pitiwa na usingizi, mi hapo siwezi kulala, huwezi kuamini kuanzia hapo nilipatwa na tatizo la kutopata usingizi mpaka leo linanitesa, nikaanza kumuangalia akiwa amelala, ni binti mrembo, nikaanza kuwaza zile sms, natamani hata nimnyonge!! Ila bado nawaza hiki kiumbe tumboni, au nimconvince atoe mimba nimpige chini, ntampa sababu gani, basi tu mawazo hayaishi


Nikatoka nikaenda sebleni nikamimina pombe nikaanza kunywa huko( mpaka leo nina utamaduni huwezi kukosa pombe kwangu hata kama sio za bei lakini lazima niwe na stock ndani)... Mawazo kama yote sielewi cha kufanya, sasa sijui kwanini nikawa namkumbuka sana Mary nikiwa nimelewa, Samira ikawa rahisi kumsahau labda kwa kua hatukua pamoja kwa muda mrefu, nikashika simu nikampigia Mary ikaita weee haikupokelewa, nikaachana nayo, nimekaa sebleni Rachel mara kanifata,
"Mume wangu mbona huku tena usiku na hio pombe na tumbo kulikoni"

Nikamwambia nina kiporo ofisini nataka malizia alafu nakunywa kidogo labda tumbo litakaa sawa, basi akaja pale ananibembeleza na nini hapo nawaza zile sms, nawaza ile clip yaani napata hasira basi tu, badae akarudi kulala nikawaza nikasema ntapata jibu tu hakuna haja ya kupanic


Kesho nikaenda kazini kama kawaida, natoka nikapita pale golini kwake nikampa hi tukawa tunapiga story tu pale, mara mezani nikaona ile simu niliyomrekebeshia nikamuulizia ulipata picha zako za zamani akasema ndio, basi nimekaa pale nikazuga zuga badae nikashika ile simu kuchungulia nakuta sms zote zipo tu kama jana, hajafuta hata kitu, moyoni nikasema huyu binti tofauti na umalaya mbona tena ni kama hamnazo, ni ujinga au kiburi? Yaani ushahidi wote wa ujinga wake anaacha tu na anajua naweza angalia muda wowote..... Nikajisemea moyoni... Karibu uswahilini patrick

Hasira zikapanda pale tena nikaaga nikaondoka zangu, mi huyo mpaka bar nikanywa kidogo nikakumbuka Mary alinichek sikumjibu ikabidi nimpigie, tukapiga story tu pale nikazuga nipo sawa wala hakuna shida yoyote basi badae nikarudi home siku ikaisha


Kumbuka hapo bado nadaiwa laki 3 kwa kina Rachel ambayo sikumalizia, nawaza hapo nipeleke au niachane nayo tu, nikawa najiona mjinga yaani mimi ndo naenda kulipia K ambayo watu washacheza nayo kiasi kile nikasema dah! Si niliacha K za maana dar nikakimbilia huku, acha nikome sasa


Ujinga sasa, badala kipindi cha mwanzo ndo ningeanza kumdadisi Rachel nikajikuta sa ivi ndo naanza kumhoji kuhusu maisha yake, ndo akaniambia baba yao aliwakimbia wakiwa wadogo, na yule mdogo wao wa mwisho ni mtoto wa baba mwingine, anadai baada ya kumaliza la saba hakuendelea na shule, na alipofikisha miaka 16 ndo akahamia kwa yule rafiki yake mwenye mgahawa akaanza kujitegemea, sasa nikawa namuuliza unajitegemea kwa kazi gani sasa akawa anajiuma uma akilini hapo najiambia patrick acha ujinga kwani majibu huna



Mama mkwe nae hapo alishakua free ananipigia simu tu tunawasiliana kama kawaida na nyumbani akawa anakuja freely tu, nikapanga siku nikaenda kumalizia ile laki 3 lakini safari hii nilienda na baba mkubwa(hakuwepo awamu ya kwanza).... Tukafika tukamkuta mama mkwe,Rachel na mzee mmoja safari hii hapakua na maongezi sana tukalipa ile pesa tukala pale maongezi kidogo tukaondoka


Tukapita mahali nikawa nimekaa na baba mkubwa mara from nowhere ananiambia
"Tatizo lenu vijana mnaharibu kwanza ndo mnakuja kutushirikisha, yule binti kama angekua hana mimba ningekushauri uachane nae tu"
 
Back
Top Bottom