MENEMENE TEKERI NA PERESI
JF-Expert Member
- Mar 11, 2022
- 5,392
- 14,646
Gupatrick kumepigwa pigo takatifu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unashaangaa tu sio!
People are not punished for their sins, they're punished by their sins.Hakuna aliye mkamilifu, malipo nayalipa hapa hapa duniani endelea kufatilia na mimi nilikutana na aliyeninyoosha
Huyo kapondaa na kusigina kabisa 😅😅Umeyakanyaga mkuu, 😃
Mkuu umeliwa na usipoangalia hicho kibarua kitaota nyasiHuyu wivu juu yangu umepitiliza maana imekuwa kero sasa. Nikisema nikuorodheshee anayoyafanya mpaka wafanyakazi wenzangu wa kike wananitenga kimawasiliano kwa kuogopa kuvuruga uhusiano wangu na huyu girl, sometimes week ends mchana naweza kuwa sehemu na rafiki au marafiki ila huku nyuma nitafutwa kwenye ma bars yote nisipokuwa nyumbani. Yaani yeye anataka muda wote tuwe pamoja achilia mbali muda wa ofisi tu. Akisikia sms au simu imepigwa tu ye hajui nani anataka apokee yeye kwanza. Hapa aliongea na boss wangu mama mtu mzima aliponipigia simu niliacha ndani jioni mi niko uwanjani nacheza mpira. Baada ya kama wiki mbili kuoita ndio boss wangu akaniuliza huyo mwanamke ninaeishi nae awe na heshima na ajue jinsi ya kuongea mtu na mtu sio wote mahawala wa mumewe. Nilijisikia vibaya sana, alafu yeye kanyuti tu wala hakuniambia lolote.
Baadhi wenye majina ya Rachel huwa ni shoti hatari...unapigwa huku unabembelezwa, kijana ukanasa kwa "Nashukuru Umerudiiii" 🤣🤣Season 2 episode 1 Mwanza
Huyo mimi mpaka mwanza nikaanza kazi kule na maisha mapya yakaanza, kusahau relationship za dar haikua rahisi ila wanasema muda unaponya na umbali pia ulisaidia, nikaanza maisha sasa jijiji mwanza, kuna mgahawa mmoja nikawa kila siku naenda kula hapo jioni nikatokea kuzoeana na mdada mwenye mgahawa sana, sasa pembeni kuna kibanda kimoja kuna dada alikua anakata matunda anauza pale, nikawa natoka napitia matunda naondoka zangu, muda ukaenda yule dada wa mgahawa alikua ashakua rafiki yangu sana, hapo nishaaanza kuvutiwa na yule dada muuza matunda sasa alikua na aina flani hivi ya shepu, chuchu bado mpya kabisa na sura flani ivi innocent sana, nikaanza mdadisi yule dada wa mgahawani ndo siku akaniambia yule anaitwa rachel( sio jina halisi) nakaa nae ghetto moja
Maisha yakaendelea kuna kipindi nikawa simuoni huyo rachel kwenye matunda sasa, nikaja muuliza mwenzake ndo akaniambia sa ivi yupo nyumbani tu walishindwana bei na mwenye kibanda chake, nikamuuliza kwanini asije akusaidie hapa mgahawani akaishia kucheka tu akasema huyo na jiko wapi na wapi, basi tukaishia hapo, nikawa kila nikienda kula pale mgahawani namuachie yule dada wa pale elfu 10 au 5 namwambia mpelekee mwenzako sa ivi si hana kazi, nikawa nafanya hivo kila nikipata nafasi... Sasa kuna siku nikawakuta wapo wote pale mgahawani nilivyomaliza kula nikamuita rachel nikamsalimia alikua kapendeza kwelikweli na umbo analo,huyu binti nimemzidi miaka 7 so by that time alikua na kama miaka 18 tu hapo, akaitika nikaanza kumtania naona maisha yamekua matamu umeacha kazi, akaniambia wapi kaka yangu nyumbani nakosa hata hela ya vocha, nikamwambia acha zako za kwangu tu nazotuma huwezi maliza kwenye vocha akabaki anashangaa za kwako zipi
Sasa wanawake sijui ni kutopendana au nini, yule dada wa mgahawa kumbe hakuwahi fikisha hata senti 5 wala salamu kwa huyu binti rachel tukabaki wote tunashangaa tu, basi tukabadilishana namba pale nikampa elf 10 mi nikaondoka zangu, baada ya kama wiki nikawafata nikawatoe out tukatembea tembea jijini nikawarudisha badae, sasa akili ikaanza kuwaza huyu binti mbona kama anafaa ngoja nijaribu kua nae tuone itakuwaje
Nikaja siku nikampeleka mahali nikamuambia live kabisa sikumficha kitu akaniambia haya kaka yangu ntakujibu, ikapita kama siku 2 akanitumia sms hapana kaka yangu sitoweza nikamjibu sawa tu wala sikuwaza sana, sasa sijui wanawake hua wanawaza nini, akawa amenikataa ila ye ndo kila muda anatuma sms mi nikawa namwangalia tu, sasa siku nipo na mfanyakazi mwenzangu tumetoka job tumepita mahali tunapiga gambe huyu binti rachel akaanza sana kuntumia sms whatsap nikawa simjibu, baadae akili ya pombe ikanituma ngoja nimrushe roho huyu kwanza ananichukulia poa sio, nikaingia whatsap nikahide watu wote wasione status yangu isipokua yeye na rafiki yake yule dada wa mgahawa, nikazama google photo nikadownload picha moja ya samira(huyu msomali alikua mzuri kweli) nikaweka status nikaandika miss you maa, nikaacha bomu langu lijipike😀
Baada kama lisaa dada wa mgahawa akapiga simu nikapokea akaniuliza umefanya nini, nikamjibu kwani vipi, akasema nimekuja namkuta rachel analia, nikamuuliza kwani vipi mbona sielewi, akaanza we si umeweka wanawake zako status, nikasema kwani kwani shida gani kwani rachel ni nani kwangu, akaniambia hapana usimfanyie ivo anaumia, nikakata simu nikacheka sana nikajua hapo mtego wangu wa bomu ushalipuka,
Wanakuambia kingaacho sio dhahabu, rachel ndo mwanamke alinifanya huu msemo niuamini kwa asilimia mia
Kaona "Nashukuru Umerudii" panafaa 🤣🤣🤣Ee si kija Mary uliwakataa recho ndio anakufaa 😂😂
Weka neno Demi, weka neno 😄Aisee
leta episode nyingne
njoo ghettoNdefu mno
Aliyemaliza kusoma anisimulie
Njoo kwangu nikuondolee hayo matesoMapenzi!!
Yamenitesa sana
Unafanya kazi sikukuu hii!Nitarudi ngoja nifanye kazi za watu kwanza