Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Mkuu usisumbuke hapa JF kuna maskini vichaa hata 1m hawajawahi kushika mkononi achilia kumiliki. Maskini ukimwabia una laki 5 mfukoni daily na 5m kwenye simu kama ya emergency hakuamini kabisa.

Ukisema unamiliki Nyumba na gari kadhaa wanaona unajipa promo tu, ukibishana na chizi wenye akili watakuja kukudharau. Hata kama umevaa smart
 
Hadi leo nina kesi na wife nilimshika matako mdgo ake. Hii story naisoma kwa kujificha asije sema najifunzia huku, na kumbe ndio tabia yangu, Lkn nipo siti ya mbele hapa namcheki Rachel aache usumbufu
[emoji38][emoji38]
 
S3 epi 20



Hizi habari za Rachel kurudi hapa hazikua nzuri kabisa kwangu, nilijua tu zitaleta tension kubwa huku amani Kwa namna Moja au nyingine itakua hakuna.... Sasa G yeye hata siku moja hawezi kukuambia habari yoyote kuhusu dada yake, hakuwahi kabisa kuanzisha mada au ukute mnaongea akamzungumzia dada yake



Mama mkwe nae huku kwetu hakuwahi kutia mguu, wao ndo walikua wanaenda kumsalimia na mtoto, baada ya kuona Rachel amerudi nikawa nimempa G maelekezo kua aache kwanza kwenda kule mpaka tuone Hali itakuaje....



Muda hausimami, Kuna siku nipo tu na washkaji wa kazini weekend Moja tunapiga kinywaji kidogo, kukawa na vibe flani tu hivi nikajikuta nimechelewa kurudi nyumbani, nimerudi nyumbani naingia ndani mpaka chumbani Nakuta mtoto amelala G analia tu, kumuuliza nini ni kilio tu, nikaja Jua hapa ni swala la uchungu wa uzazi tu, nikampigia mshkaji wangu mmoja tukutane home, nikamuandaa pale vitu vyake mtoto nikamuacha Kwa dada wa kazi, hao tukaongozana mpaka hospitali....


Kufika huko tumekaa mpaka asubuhi bila bila, kesho yake nikawa nimeondoka G Bado yupo hospital nikaenda nyumbani mara Moja Ila Kuna dokta tukawa tunawasiliana, Ile najiandaa kurudi hospital yule dokta akaniambia huyu nampeleka theater naona anazidi kuchoka tu, nakamwambia sawa ila hapo nishapatwa na kaubaridi flani hivi, nikaenda mpaka hospital nikaambiwa yupo theater, Sasa hapo mama mkwe sikua nimemwambia chochote, ikabidi tu Sasa nivunje ukimya nikampigia nikamuelezea Kila kitu, haikupita muda akawa amefika pale basi tu tumekaa nje pale tunasubiri Kila mtu yupo busy na mawazo yake



Mungu ni mwema G akajifungua mtoto wa kike, japo Kwa operation, na mtoto hakua fully developed (njiti wanaita) hivo ikabidi wakamueke kwenye vile vyumba vya joto, ikifika muda mama(G Sasa) wanakuja kumchukua anaenda kumnyonyesha mtoto anamuacha huko huko ye anarudi wodini huko, hapo mama mkwe akaanza kuniambia nitafute mtu Sasa wa kukaa na mzazi( ni kama yeye alikua hataki kushiriki kabisa)



Sasa tuna wale ndugu zetu kijijini hua tunawaona hawana maana mpaka siku tupatwe na jambo, nikafanya mawasiliano Kuna ndugu yangu ni mtu mzima kiasi alikua kijijini ikabidi nimuombe nikatuma nauli akaja, baada ya kama wiki tukaruhusiwa pale hospitali tukarudi nyumbani..... Yule ndugu yangu Sasa ndo akawa Kila kitu Kwa mzazi, kumpikia, kumuosha mtoto,kumkanda mzazi n.k



Hapo Rachel hakuwahi kutia mguu Wala hata Simu au sms ya kinafki Kwa mdogo wake..... Home kwetu nikawapa taarifa bila kumsahau ba mdogo wakasema watajipanga watakuja acha mtoto afumbue hata macho kwanza, kitendo Cha kufika kwangu tu mama mkwe nae hakutia mguu tena, tofauti na kule hospitali huku ikawa basi, ila utakuta kampigia Simu mtoto wake




Maisha yakaendelea nakumbuka imepita kama mwezi hivi ndo ujinga ukaanza, siku moja nipo kazini, G ananipigia Simu anaongea tu Kwa kupanic mie hata simuelewi vizuri, nikakata simu nimpigie, kabla sijapiga Simu ya dada wa mtoto hio hapo, napokea ananiambia kaka njoo kuna shida huku, nae namuuliza hata hatuelewani.....



Nikatoka Ile kufika ndo naambiwa Sasa, Rachel kaja pale kamchukua mtoto Kwa nguvu kaondoka nae, hapo kashawacharua vibaya G na yule dada wa mtoto, kama mjuavyo watu wa kijijini hawapendi maneno yule ndugu yangu kimya tu Wala hakuingilia, mi hata sikupanic, nikatoka hapo Moja Kwa Moja mpaka kwao..... Kufika Nakuta mama mkwe hayupo, ni Rachel na mtoto tu




Sasa nature ya watoto Sasa, ukimuacha mda mrefu akiwa mdogo haijilishi ni baba au mama yaani hawezi tu kukubali kua na mtu ambae hajamzoea kabisa, nikakuta mtoto analia Sana, kuniona at least Sasa akapunguza kulia, hapo Nina hasira kinoma namuuliza mbona unafanya mambo kama huna akili? Nae hapo Kawa mbogo tukaanza kugombana Sana, Sasa namuuliza mtoto mwenyewe hajakuzoea analia muda wote unakaa nae vipi, nikawa nataka TU kumchukua dogo niondoke nae



Sasa katika kugombana na kurushiana maneno kuna kauli Moja akatamka " niachieni mwanangu, mtaenda kumfunza nini zaidi ya umalaya tu huko" dah in a split second mkono ukanitoka nikajikuta nimemzaba kibao usoni alafu nilikua nimeshika funguo, akaanza kuugulia maumivu pale mi sikujali nikambeba mtoto nikaondoka nae mpaka nyumbani, kufika nikamuacha pale nikawaambia akija mtu yoyote wasifungue geti mpaka wanipigie, nikarudi kazini



Kufika kule sikukaa hata Sana nikapigiwa Simu nifike kituoni, nikawaambia ntakuja nikitoka kazini, yule afande akawa anafoka " uje Sasa hivi, unajipangia muda wa kuja unadhani hapa ni hotelini, ole wako tukufate" ..... Sikutilia maanani Yale maneno, nikakaa mpaka tumetoka kazini Kuna jamaa nikawa nimemueleza nikaenda nae...



Kufika pale counter ndo najielezea Sasa nilipigiwa Simu nifike hapa, Ile kujielezea kuna afande akatokea kwenye chumba flani akasema tena huyo muweke ndani ana dharau Sana huyo.... Kiutani utani naambiwa vua mkanda,saa,viatu uingie ndani, nikawa sielewi pale nikawa nimegoma, Kuna afande sijui alitokea wapi akinipiga bonge la rungu mgongoni....


dah nikaona Hawa Sasa watakuja kuniumiza, na askari wetu hawataki hata kumsikiliza mtu wanatumia nguvu tu, basi bana nikavua mkanda pale,viatu..... Saa na wallet na funguo nikakataa kukabidhi counter pale nikampa yule jamaa niliyekuja nae....



Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nikawa nimefichwa ghetto(kuingia selo)
 
Nimecheka kauli ya mama,Asante kwa mjukuu,Anza kutafuta mke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…