Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

s3 episode 7


katika kitu nilichojaliwa ni mtulivu sana kwenye situations ngumu, hapa nikawaza hakuna haja ya kupanic wala, maana uzuri nilishajua swala ambalo mama mkwe atakua kaniitia, nikawa nawaza ni swala la picha tu au kuna kingine, ila sasa akili inanituma nijipange tu


wala hata sikuhangaika kujibu ile sms, nikawa nawaza hapa najipangaje, zikaja kama option tatu 3 kichwani, ila katika option zote swala la kusema eti ntaenda kukubali hilo likawa halipo kabisa yaani, maana uzuri G nshaongea nae kwa io najua vizuri kila kitu kinachoendelea, nikawa najipa moyo, nipo mbele ya muda yaani anachoniitia nishakijua ni swala tu la kujua nafanyaje


sasa nikapate mawazo kama matatu ivi ya kufanya

i) nikienda nimskize tu anasemaje alafu mimi nikatae tu hayo madai maana nishajua litakua ni swala la kutembea na G tu wala hakuna kingine, na uzuri G nilishaongea nae nina uhakika hajasema chochote, nikawa nawaza hata kama ndo ishatokea lakini hakuna kitu kibaya kama kujifanya mwema ukamwambia mtu ukweli ambao hawezi vumilia, kama hana ushahidi wa kutosha ni bora ukatae tu


ii) akishanipa hizo tuhuma niwe mkali sana, nibadilike tu nimhoji kama mimi kua karibu na familia ndo inàkua shida bora nifanye tu mpango mwingine wa kumlea mwanangu maana naona kila siku tuhuma kwangu Haziishi


iii) nimpotezee kwanza mama mkwe, nije kumtafuta siku nyingine kabisa, ila asione kua kama kaniamrisha na mimi nikaja siku hio hio, hii ni kwanza atulize presha na pia asijione kama anaweza kuni control, ili hata siku tukikaa asione kama ana upperhand katika maongezi yetu, kiufupi nisimuonyesha kua yeye ndo mkubwa katika hayo maongezi



nikatulia nikawa nawaza niende na option gani kwanza, badae nikawaza nikasema nianze na ya iii)... hivyo huo muda sikumjibu kwanza.... nikakaa mpaka muda umeenda sana nikamtumia sms "nina ratiba ngumu kazini, nikipata muda ntakuja tuongee mama wala usijali"


nikarudi kwa G sasa, nae analalamika tu maswali huku hayaishi, nikamuuliza kwani mmeishia wapi, nae akasema kama nilivyokuambia jana mi mwenyewe nimejifanya nashangaa ila mama anagomba muda wote tu nimeamua kua kimya, nikamwambia sawa usijali we kaa hivo hivo tu ila nikamtahadharisha awe makini tu asije akajiachia na simu yake, nikamuomba tuwe tunawasiliana ila sio kama zamani, sio kila muda kutaftana nikamwambie kaa kimya kwanza ntakua nakutafuta mimi mpaka tuone hii hali inaenda vipi akasema sawa


sasa mama mkwe nae sijui ni hasira hata ile sms nayomwambia ntakuja nikipata muda nayo hakujibu nikasema sawa tu tutajua



zikapita kama siku mbili ndo nampigia namwambia leo nina muda ntakukuta wapi, akaniambia ukitoka we njoo nyumbani utanikuta nikamwambia sawa



kweli badae nimetoka nikaenda mpaka kwake, nikamkuta mwenyewe G wala dogo siwaoni, akanikaribisha pale tukajuliana hali za siku mbili tatu na nini, badae namuuliza vipi mbona hawa hawapo akaniambia hawa wapo kwa jirani tu hapo, hapo nimepata ahueni kiasi maana njiani nilikua navuta picha kua hawa hawaeleweki naweza kufika nikavikuta vile vizee vya siku ile



basi tunaongea kawaida tu ikabidi sasa mi ndo nivunje ukimya, hapa bado nacheza na akili yake ili asijione kua ana upperhand katika hiki kikao, nikaanza



mimi: enhe mama nimekuja leta habari

sasa hapo akaanza kujisemesha mambo mengi, oh unajua mwanangu tumekua kama familia mimi hatujawahi kugombana, japo mlitofautiana na mwenzako(rachel) lakini tumeendelea kua familia, na we ushakua kama mwanangu..... na maneno mengi tu mpaka sasa akaja kwenye point


mama mkwe: mwanangu kuna vitu vinaendelea mimi hata sijui niseme nini, majuzi rachel kanipigia simu kawa mkali kweli mpaka nikakosa amani, anadai sijui wewe na G mshaanza kutuma picha mitandaoni mara mnavaliana nguo yaani kaniambia mambo mengi mpaka nikawa sielewi, na unakumbuka baba ile siku mpaka mi nikakuuliza, maana nilimuona G ile siku tulivyofika kwako yupo tofauti sana mpaka ikabidi niulize kuna nini, na haya maneno ya dada yake sasa nashindwa kujua hata kuna nini


uzuri sasa hapo mi ni kitu ambacho nilitegemea angeuliza wala hata sikupanic, nikaanza


mimi: mama mbona hata sikuelewi, picha tena mitandaoni? alafu mi kuvaliana nguo na G tena mbona sielewi



hapo nikajifanya sijui kabisa lolote kuhusu hayo maswala anayoniambia


mama mkwe: yaani hapa hata mi ndo nashindwa kuwaelewa, rachel alipiga anasema sijui mdogo wake alituma picha zako mtandaoni, mara sijui amevaa nini cha kwako, alivyokua mkali tulishindwa hata kusikilizana


mimi: mama sasa hapo ndo naanza kupata picha maana majuzi rachel nae kantukana sana nikawa sielewi hata ni kwanini ila mi sikumjibu, sasa hata mi sijui ni picha gani, alafu mdogo wake na nguo zangu wapi na wapi mbona mnanichanganya




akavuta pumzi pale mara akatoka akaita, we Grace hebu njoo huku, baada ya muda G kafika, mama mkwe akaanza kumuuliza hivi we ni nini ulituma na hayo mambo yenu ya mitandao mbona mnanipa mawazo mimi, Grace nae akaanza kumwambia ni picha tu nilipost ile siku tumeenda kula na we ukiwepo sasa hata sielewi kwanini imekua shida, hapo hapo na mi nikadakia



" ni ile picha ulipost ile siku tuko ma mama tunakula?"

akajibu ndio, nikaanza sasa.... " mmmh si ile picha tunakula tupo ma mtoto, sasa kuna shida gani, kweli mama ndo ulichoniitia hicho mama?"



hapo mama mkwe nae ni kama haelewi akaanza kuniambia " mi hata sielewi hayo mambo yenu ya mtandaoni, sasa na hayo maswala ya nguo yametoka wapi mbona mnanichanganya wanangu?"


grace akamwambia "mama sasa mi nguo za shemeji wapi na wapi ni kofia nilimvalisha mtoto badae akawa ameniwekea kichwani ndo nikawa nimepiga picha tu, tatizo dada anapenda sana maneno na yeye"



kimya kikapita kidogo, mama mkwe akamwambia G haya we nenda sasa


hapo ndo nikaona ni wakati sahihi wa kufanya sasa ile option ya ii).... nikamwambia mama unajua sisi tushakua kama familia, huyu Grace namchukulia kama mdogo wangu, hata ile siku ulivyoniuliza vile nilishangaa ila sikutilia maanani, leo tena nashangaa swala lile lile tu,


hapo kidogo nishaonyesha kuchukia, nikaendelea


" tumekua karibu kwasababu niliamini hata kama tumetofautiana na mwenzangu(rachel) ila niliamini mtoto bado ana familia hapa hakuna kilichoharibika, ila sasa naona mambo yanakua magumu, ni bora tu unipe muda nitafute mtu akae na mtoto nije nimchukue au niongee na nyumbani huyu ashakua aende kule tu maana sasa sielewi haya mambo yanatoka wapi na sitaki nije niwagombanishe(rachel na G) ukizingatia hawa ni ndugu.... naona nifanye hivo maana najiskia vibaya hata haya mnayoniambia, sikutegemea kabisa ndo ulichoniitia hiki mama"



mama mkwe nae hapo akaanza kuntuliza, "acha hasira mwanangu hayo mambo ya watoto ndo maana hata mimi nilikua siwaelewi.... sasa huyu dada ake sijui kaona nini nashangaa anakua mkali tu"



badae namwambia sasa huyu Rachel kaenda kuolewa huko mimi siku zote nipo kimya au ndo ameamua kutafuta tu sababu ili na mimi nikose amani huku?



mama kimya hapo anasikitika tu....



badae nikamwambia mama fanya tu mpango upate binti wa kazi akae na mtoto siku nikitaka kuwaona aje nae maana hili lishakua jambo sitaki liendelee hivi ili kila mtu awe na amani, maana maneno nayo sio mazuri yatakuja kuleta balaa huko mbele... huyu Grace tumuache tu maana imeshakua chokochoko


akaniambia sawa mwanangu ngoja ntakujibu, ila nisamehe tu maana hawa watoto wananchanganya na mambo yao ambayo sielewi....


tukaongea basi tu mambo mengine badae akaja mtoto nikakaa nao pale nikaaga nikaondoka



njiani sasa najiskia vibaya, hakuna kitu kibaya kama mtu anakuamini alafu aje kujua ulikua unamwongopea, nawaza narudia yale yale maisha yangu ya dar ya uongo uongo, nawaza sawa leo limepita ila sasa mwisho wangu na grace ndo utakua vipi
Muendelezo Jamani 😅nimesubiri weeee
 
Back
Top Bottom