Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

S3 epi 9


Nikatafakari Sana nikasema hapa nisipokua makini haya mambo yataenda kua magumu unaweza Kuta unataka kukimbia mkoa tena kama Yale Yale ya dar... Ila nawaza Nina option gani? Nikawaza wee... Nikaja na mawazo kama matatu hivi


i) kwanza kabisa ni kumuweka G under my control, kitendo Cha huyu Binti kuanza kunitisha sio Cha kukichekea kabisa, Sasa hapa nafanyaje? Huyu natakiwa mimi ndo nimcontrol mpaka ntapopata suluhisho,either Kwa kumuweka karibu tu(kumbembeleza) au kwenda nae kitemi, hapa nikawaza jawabu likaja huyu Bado mtoto mdogo nikimuendekeza hachelewi kunivua nguo, huyu ntaenda nae kitemi

Ii) hata kama huyu asipotoa mimba, swala la mimi kumuambia mama mkwe is a no go zone! Kiufupi hata iwaje swala la kwenda kujisalimisha Hilo nikalitoa akilini kabisa nikasema siwezi kufanya ivo hata iweje....


iii) hapa Sasa nikajipanga for the worst, huyu akigoma kutoa mimba, nafanyaje? Hapa it's either nishirikishe mtu mzima Sasa akapambane na mama mkwe ila sio mimi kabisa....


Nikaingia kazini nikaanza na mpango kazi wa kwanza(option i)... Kwanza hio sms ya G ya vitisho sikujibu, badae akatuma sms zingine mie nipo kimya tu, akapiga Simu sikupokei kabisa, kesho tena nipo kazini anapiga Simu tu naziangalia, badae nikatoka kazini nikapita kwenye duka lao hapo akaniona akatoka akaanza mbona hupokei Simu dear Kuna shida, hapo nipo serious kiasi, nikamwambia ukitoka tuonane, sikutaka mambo mengi nikaondoka..... Badae katoka kanitafuta nikamuelekeza mahali akaja, akafika sikutaka kupindisha maneno Wala nini, namuuliza sms gani unanitumia Jana? Anauliza ipi? Namwambia hivi kweli tumefikia unanitishia mimi kua utaenda kumuambia mama? Yaani tupo wote kwenye tatizo hunipi hata muda wa kufikiri nafanyaje unaanza kunitisha? Mbona huna adabu siku izi, nikamsema pale akaanza tu kujitetea kuomba msamaha pale kua zilikua hasira... Sasa hapo ndo nikamwambia point black kua mimi ndo mwenye maamuzi ya mwisho, akae atulie mpaka nitakapopata suluhisho, akienda kinyume na hapo atajua mwenyewe Wala mi sitahusika na chochote, hapo nimechukia kweli, nikamwambia "Sasa we ukiona sawa nenda kamuambie mama alafu kuanzia hapo mi sitahusika na chochote mtajua wenyewe, na kwanza atanifanya nini"


Kuona vile akaomba msamaha kweli, akaanza kulia, anasema Ina maana nikitoa hii mimba alafu inakuaje, Ina maana huna malengo na mimi Patrick???


Hapo Sasa napata hasira tu nazidi kumshangaa, malengo tena? Akilini nikasema haya ndo madhara Sasa ya kua na watoto, nikajiambia utavuna ulichopanda



Basi nikamwambia pale akae atulie na kuanzia hio siku ntachosema mimi ndo final sipendi mashindano, na nikamuonya asije tena kujaribu kuntishia, akasema sawa nimekuelewa.... Nikamtafutia usafiri akaondoka.... Kufika akinitumia sms anaomba msamaha tu


Hapo nawaza Ina maana huyu hata hamuogopi mama au dada yake? Anawaza nini?

Anyway option i) ikawa imeisha ila Sasa shida IPO pale pale, nafanyaje? Abortion hapo mwenyewe nipo 50/50 ni kama namuonea huruma, na hata kama nikisema nifanye hivo Bado Kuna uwezekano akagoma pia



siku zikapita kiasi, hapo tatizo lipo pale pale, nina mawazo Sana hapo Sasa mwenzangu yeye hata Hana presha Wala nini.... Utakaa wee utakutana na sms " Leo najiskia kula kitu flani(.....), Huyu mwanao ananitesa kweli"


Dah, hapa naona huyu anachukulia hii ishu kimzaha Sana, mara aniambia aondoke nyumbani akapange alafu hata mama akijua hatonitaja tufanye Siri tu asiseme baba wa mtoto mpaka hapo badae, stupid idea!!!! Mzee wangu aliyetangulia mbele ya haki kila mara alikua ananisihi "hakuna kitu kibaya kama kuahirisha tatizo"


Nawaza hata akifanya hivo ipo siku ukweli utakua wazi, alafu nini? Tutarudi tu pale pale



Sasa na mimi nikawa kama nimeahirisha tatizo, sipati maamuzi, muda ukaenda mpaka mimba Ina kama miezi miwili na sehemu karibu mitatu, hapo Sasa naona kabisa abortion is out of the options, Kila siku namuambia G mama Yako atagundua tu ni swala la muda, nikawaza we nafanyaje......


Kuna siku nimekaa kazini, G ananitumia sms " ukitoka kazini nipitishie chocholate, mwanao ndo anataka ananisumbua"

Nikawaza huyu Hana hata mawazo ni kama anafurahia tu hii Hali, nikasema Sasa hapa mambo yashaharibika ngoja nitafute mtu anisaidie kuumiza akili



Sasa Nina ba yangu mdogo yule tulienda nae kujitambulisha Kwa kina Rachel, huyu ba mdogo ni mission town Sana mjanjamjanja, alafu alikua peace Sana huyu hata kama mpo sehemu mnakunywa anaweza mtongoza mwanamke mbele Yako, yaani tulikua tumezoeana hivyo....


nikampanga kama baada ya siku 3 akawa amekuja mwanza Sasa, hapo sijamwambia kitu, kazini nika activate likizo, ba mdogo kufika nae namjua ni mtu wa viwanja tukawa Kila siku tunatoka tunakunywa story nyingi ila hapo sijamwambia kitu, Kuna siku G akatoka kazini nikamuita mahali tukakaa wote ila sikufanya utambulisho Wala nini mpaka badae G akaondoka akatuacha



Sasa ba mdogo nae huku mwanza hakuwahi kuja tena tangia kipindi kile Cha utambulisho, akaanza utani "mwanangu unajua ku sort,haka ni ka wapi tena? " Nikamwambia mzee we acha tu hapa Nina balaa, anauliza nini tena? Ndo namwambia huyu ni mdogo wake Rachel, nikamuelezea mambo yalivyoenda mpaka kumuambia nilishaharibu


Sasa hapo nipo serious, jamaa akaanza kucheka vibaya mno, mara ananiambia "huo ndo uanamme Sasa, Hawa wajinga tulienda kujitambulisha wakatupiga faini alafu wakatufanyia mambo ya ajabu, hapo Sasa ndo umebalance mzani'


Nikabaki nashangaa,namwambia Mzee acha masihara hii ishu Iko serious ujue, ye anasema kesi ndogo tu hii, akaanza Sasa kunipa mifano kwenye ukoo wetu, mara mbona yule mjomba wako wa mahali Fulani alioa mtu na dada ake, akaongea we anasema ni mambo ya kawaida hapo mi simuelewi kabisa...


Sasa bana tunaendelea kukaa pale nina mawazo jamaa ana furaha kinoma, yaani anacheka tu mi simuelewi mpaka muda tukarudi nyumbani anadai Hilo swala dogo niachie mimi



Zikapita kama siku 2 nikamwambia ba mdogo mi naenda nyumbani nikamsalimie mama, we Baki huku pambana na huu msala, akasema Haina shaka, lengo langu mambo yakitibuka huku nisipowepo, nikaanza mipango ya safari, Kuna siku nikamcheki mama mkwe nikamwambia mama siku ukiwa na muda ba mdogo yupo huku anataka kuja kukusalimu amuone na mtoto, akasema jumapili sitoki mwambie aje atanikuta..... Hapo ba mdogo anasema huyu ni kwenda kumshtukiza tu akijua tutakutana na wale wazee tena, G nikamuambia nasafiri mara Moja Kwa mama ila sikawii basi akakubali kishingo upande, nae hatukumuambia, yaani ikawa kimya kimya hapo nawaza mi niondoke hili bomu likilipuka mi niwe mbali


Ikafika siku nikaondoka zangu, ba mdogo nikamkatia fungu la kupambana na huo msala nikiwa sipo, mama mkwe hapo namkwepa nilimuaga kwenye Simu, lengo la kumkwepa maana ningeenda ingebidi niende na ba mdogo alafu lengo la jumapili lingepotea, hapo nikamuaga namwambia ba mdogo yupo Kuna mambo yake amekuja fatilia jumapili atakuja akasema haya...


Nafika home napokelewa vizuri, piga Sana story na mama nilikua na muda sijafika nyumbani, Ile kufika muda wa kulala tunaagana mara mama ananiambia "naona baba Yako kaja huko mwanza wewe nawewe umekuja huku umemuacha, akili zenu nazijua najua mshaharibu huko"

Nikasema kumekucha
 
Back
Top Bottom