Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Hawa wazee wanasema siku ya tambiko lazima tuwepo hasahasa wewe, tuwe makini Mzee Hawa watu huku ni wajinga Sana tunaweza kwenda kichwa kichwa tukaishia kuchapwa viboko na uzee huu"
Aisee nimecheka Sana🤣🤣🤣🤣
Huyu Mzee wa mission ananikumbusha Baba mdogo wangu mmoja ivi..Yaani maneno kibao utafikiri kazaliwa mjini kumbe hamna kitu😂
 
S3 epi 12


Nikawaza nikasema ba mdogo nae Sasa mbona namuamini ila Kila anapogusa anapigwa za uso, huyu Mzee kamshindwa tena? Mbona balaa Sasa hapa.... Anyway nikasema ngoja amalizane nae atanambia imekuaje tena



Hapo mawasiliano Sasa yashakua magumu, mama mkwe ndo kabisa siwezi hata kumgusa, ikabidi nimpigie dada wa kazi wa mtoto, huyu nilikua naongea nae mara chache Sana , akanisalimu pale naulizia Hali ya mtoto akasema yupo sawa, nikamwambia hebu Kaa sehemu mwenyewe alafu unitafute, akaniambia usikate Simu ngoja nitoke nje, alivyofika nje ndo namuambia hebu Sasa niambie nini kinaendelea huko



Ndo ananiambia mama anaumwa, yupo Kwa jirani hapo rafiki yake ndo wanamuuguzia huko, haya, namuulizia G, huyu dada nae anasema G kuanzia asubuhi aliondoka pale hajarudi mpaka Sasa... Kwa Io ye amebaki mwenyewe na mtoto tu ndani, Sasa mama mkwe hua Nampa Hela ya matumizi ya Kila mwezi nikawaza huyu nae ndo anaumwa unaweza Kuta hawapati Kila kitu mtoto ataanza kuteseka Bure



Basi yule dada hata alikua hajui password ya m pesa yake, nikamuelekeza dukani akapewa namba ya wakala nikatoa pesa kidogo nikamwambia mtoto akihitaji kitu uwe unamchukulia Sasa, akasema sawa, nikadadisi nikajua Rachel hajafika Bado ila aliskia wanasema Binti Yake mkubwa yupo njiani.... Nikajua atakua Rachel huyo



Badae Sasa namcheki ba mdogo, Sasa kumbe yule Mzee bana baada ya kumchukua maelezo ba mdogo,Mzee akawa mbogo, vita yake kwanza anasema tuna dharau Sana, kwamba hatukupeleka mahari ya Rachel kwanza hio ni dharau kubwa, alafu Kwa kua tumeshawaona wao ni wajinga Sana tumeamua kuzalisha tena hapo hapo maana tumezoea vya Bure( aisee Kuna wazee Wana midomo)



Ba mdogo akajaribu kuleta Siasa pale Mzee haelewi Wala nini ikabidi kikao kife, Sasa kumbe bana kipele kikapata mkunaji( hIi nilikuja kujua badae).... Yule Mzee akamuambia Mzee mmoja kati ya wale tuliowakuta( Hawa wazee walikua kwenye ukoo wa kina Rachel upande wa mama huko maana walikua bila baba)... Ila inaonekana hawakua na ukaribu hata na mama Yao kivile, Sasa bana siku hio hio wakashikana mguu Kwa mguu mpaka Kwa kina Rachel, kufika kule wakamuanzishia varangati tena mama mkwe, kwamba ukoo unadhalilishwa yeye anakaa kimya anashindwa hata kutoa taarifa Kwa wazee, Sasa wakasema wao ndo watashughulikia hilo jambo mpaka mwisho wake ujulikane



Ba mdogo hapo kaniambia we subiri tu kwanza huyu Mzee alisema atashauriana na mwenzake alafu atampa jibu, kweli walivyotoka Kwa kina Rachel wale wazee wakampigia ba mdogo wakawa tena wamekutana nae mjini, mimi hapo naskilizia tu, baada ya kuanza kufanya mazungumzo Kuna mda ba mdogo akanipigia, Ile kuongea nae akaniambia bwana mdogo nipo na wazee hapa ngoja nikupe tu baadhi ya utaratibu wakiwa na wao wanaskia




Sasa walee wazee wakamwambia ba mdogo hapa kwanza kabla ya yote inabidi tambiko lifanyike, mambo ya kuondoa mikosi maana wanasema ishakua mkosi kwenye ukoo wao, Kwa Io wakamuelekeza vitu vyote vinavyotakiwa na inabidi tuvinunue sisi, wao wakadai hawawezi kufanya Hilo tambiko, Kuna wazee ambao ni wakubwa kwao na wamewahi kufanya tambiko kama hili ndo wanaruhusiwa, inabidi wakawatafute, wakaombe na ruhusa kutoka Kwa mkuu wao wa ukoo.... Basi wakasema inahitajika ngombe mmoja na mbuzi dume wawili, Kuna aina ya nguo za kimila za wale wazee wa tambiko na makorokoro kibao wakasema wakishajua tarehe ya tambiko itabidi tulipe hivo vitu kwanza, alafu tambiko likiisha ndo tukae Sasa kikao....



Basi ikabidi niseme tu nimeelewa, ba mdogo akakata akaniambia ngoja tuendelee ntakujulisha nikamwambia sawa, narudi Sasa Kwa dada wa kazi ananiambia G hajarudi Bado, ila Kuna mdada mwingine kaja nikajua atakua Rachel huyo


Hapo nawaza huyu G nae kaenda wapi, na mbona hapatikani, na kama Rachel karudi G ataweza kweli kurudi nyumbani, nikasema Cha msingi awe salama tu hayo mengine tutajua



Sa ba mdogo amekata Simu akaanza kutuma sms " mwanangu Hawa wazee tusikubali watupelekeshe, Hawa tukiwasikiliza Kila kitu watakuja kutufilisi"

Sasa hapo mi namshangaa maana ye ndo Yuko nao huko, anashindwa nini kuongea nao, nikamjibu Mzee we pambana huko mi Niko mbali ntafanya nini Sasa akaniambia sawa hakuna shida


Nimekaa tena kidogo sms tena ya ba mdogo " Hawa wazee wanasema siku ya tambiko lazima tuwepo hasahasa wewe, tuwe makini Mzee Hawa watu huku ni wajinga Sana tunaweza kwenda kichwa kichwa tukaishia kuchapwa viboko na uzee huu"


Nikabaki nashangaa
😀😀eti kuchapwa viboko
 
Back
Top Bottom