Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

We jamaa ni mwamba sana,nakubali, kila mtu anamapito yake,hapa nina msala mzito nimelamba mke wa mtu,wanataka nihame huu mtaa na nimejenga,siwezi,wamekomaa niwape milioni 4,nimewapa, ila kila nikipita mtaani naona kama jamii inaniona kama msaidizi wa shetani kitengo cha ngono,nisaidie namba ya Marry
Ah wee wanadamu hawakosi lakusema muhimu kidume umekula mbususu ya mme wa mtu. Sii kajipendekeza wee unaisasambua mbususu.
Hela kitu gani bwana utatafuta
 
Wanaume wengi sana wamefanya makosa katika mahusiano ambayo yamewapa majuto yasiyoisha milele.

Wanaume wengi wamejitafutia pressure na visukari kutokana na maamuzi ya kijinga waliyo yafanya katika suala zima la sex.

Mwanaume anayeweza kuzuia zipu yake amefanikiwa duniani na mbinguni
 
1. Ndivyo akili za wanaume 90% zilivyo...sijui tumeumbwaje.
2. Hatujawahi kuwapenda wanaotupenda.
3. Umenikumbusha kitu nimeishia kulia.
4. Ndio maana mwaka huu kwangu nilijiweka mbali na mapenzi, nikachagua kazi.
4. Wanawake wengi huwa ni watakatifu hadi alipovunjwa moyo na mwanaume ndipo huharibika
Noma sana!
 
S2 episode 9


Mama namjua ni mtu wa maneno mengi nikawa nimempotezea tu mpaka kesho yake nikampigia tukaongea nakamuambia jipangane tu mje mumuone mjukuu sasa akasema hakuna shaka

Baada ya Rachel kujifungua imepita kama wiki 2 ivi kuna siku mama mkwe ananipigia anauliza baba upo wapi namuambia npo najiandaa kutoka kazini hapa akaniambia njoo mara moja kuna shida nyumbani, basi nikatoka haraka nikaenda kufika pale nakuta kama kuna hali ambayo siielewi kama kuna watu watu wengi, nafika nikamvuta mama mkwe pembeni namuuliza nini tena hapa ndo ananiambia kua Rachel anadaiwa na wanakikundi wenzake sijui wameenda dukani kwake wamesafisha kila kitu hapa wapo kwangu wanataka kuchukua tv yangu kwa nguvu, nikachoka kwanza nikauliza kikundi gani hiki, na dukani wamechukuaje vitu mbona pamefungwa yeye mwenyewe ni kama haelewi


Basi nikamuita sijui ndo mkubwa wa kikundi naona wanakuja kama wote nikawapiga biti pale nataka kuongea na mmoja tu, akaja namuuliza mnadai bei gani anadai bado kama laki 6, kutokana na ile hali ya aibu pale nikaingia kwenye gari nikatoa laki 3 nikampa na namba zangu nikamuambia hio nyingine ntakupa kesho, ni kama alitaka kugoma ila kuna jicho fulani nilimkata akapokea hio pesa



Mama mkwe nae akaanza kuniomba msamaha pale ananiambia mwenzako sijui ana shida gani mbona mambo ya aibu haya mwanangu, sikumjibu kitu mi nikaondoka zangu, nikawa nawaza hapa sichezewi michezo ya kiswahili kweli? Hivi kweli ndo nimekuja tengeneza familia na watu kama hawa kweli? Hio siku yalinishinda kuna rafiki yangu mmoja nilimpigia nikamuelezea situation zote aisee mpaka akashangaa, mwishowe akanionea huruma akaniambia tu we angalia jinsi utavyokuja kumpata mwanao basi



Huku maisha yakasonga mi nikawa naenda tu wasalimia pale kwa kina Rachel nawapelekea mahitaji na nini, sasa ikapita zaidi ya mwezi mama na sister wakawa wanakuja mwanza, hapa katikati mahusiano na Rachel ndo yapo ivo ivo sema moyoni nilikua nishamtoa namuwaza mwanangu tu, nikampa taarifa mama mkwe kua amuandae binti aje huku kwangu ila akifika mama amkute nipo nae huku


Sasa sijui ni kiburi au ujinga wa huyu binti, akagoma kutoka kwao akasema watakuja kumsalimia huko huko, hapa nadhani alikua ananikomoa maana baada ya kumlipia lile deni na kuona ameua biashara niliacha kumpa financial favour yoyote, nikawa mme kwa kipemba kila kitu nanunua au namtuma boda, maisha ya kuniomba mara laki laki 2 nikapiga full stop, kwanza nikawa nawaza huyu sina hata malengo nae, hio siku nilichukia nikaenda kwao kufika baada ya maongezi ndo nikawaambia mama na dada wanakuja inabidi mje kwangu sasa, rachel anadai mi siendi kama kunisalimia watakuja huku huku, nikawa nimechukia nikawaambia basi nipeni mtoto wamkute kwangu kama we hutaki kuja baki



Rachel nae sijui ni wehu au nini akaropoka " mtoto mwenyewe hata mahari hujamlipia unaongelea mtoto gani? "

Sijakaa sawa mama yake akanyanyuka akaanza kumpiga huku analia "mwanangu mbona unanitia aibu kiasi hiki una shida gani mbona huniheshimu au mimi sio mama yako, unajua nimehangaika na wewe vipi?"


Nikaona huu ujinga sasa mimi huyo nikaondoka zangu, nikaanza utaratibu mpya, situmi matumizi wala simu zao nikawa sipokei, haikupita siku mama na sister wakaja tukafanya mpango tukaenda wasalimia, sasa sijui kina mama wanakua na nini naona mama akawa busy tu anamkagua mtoto muda tunaondoka akaniambia huyu ni wa kwetu kuna kishimo nimekiona sikioni wanangu wote niliwazaa mkiwa nacho, nikapata faraja kidogo ila hapo bado machale yanacheza tu


Basi kina mama wakawa wanaenda kusalimia huko wanashinda jioni wanarudi kwangu, sister sasa ndo akaanza kunchamba ananiambia mdogo wangu kweli ulimuacha Mary ndo umeanguka huku..... Nakuonea huruma...... Walikaa kama siku 4 wakaaga wakaondoka wakiwa njiani naona sms ya mama "mwanangu asante kwa mjukuu, anza sasa kutafuta mke hapo hamna mke"
humu tuuu muu tuuh
 
20250110_135658.jpg

Ndio mwenye Story yake nini,,,,
 
S4 epi 2



At least Sasa nikawa nimeshausoma mchezo mzima, Sasa sijui kwanini, badala ya kushtuka nikajikuta tu nimepata hasira Sana siku hio(ntalizungumzia huko mbele)..... Nikachukua zile funguo pale nikaondoka zangu maana hapo Sasa yule mtu wa dukani naona kabisa ashaanza kuniuliza maswali ya uchuro....



Nikafika nyumbani naona kama hapako kawaida, nishazoea kukuta watu na nini, nikaona tu pale nikatupia begi langu huyo nikatoka nikaondoka zangu..... Hapo move ni kama linaenda kimya kimya Rachel nae hajanitafuta Wala nini ila hapo mi nishamshtukia najua yeye ndo mastermind wa huu upuuzi wote....



Wakuambia Kuna mstari mwembamba Sana kati ya mapenzi na chuki, nikajikuta tu napata chuki flani Kwa Rachel tena, upande wa G Sasa Nakua na mixed emotions, unajua sisi wanaume unashajua mtu anakupenda 100% Hilo nalo ni tatizo, unakua unafamfanya kama mtu yeye Hana hisia, nikajikuta moyoni tu namlaumu G, kwanini aondoke bila kuniambia...... Basi tu nikawa na hasira pale.




Nini kilitokea?


Siku Kama nne zikapita hapo siwasiliana na Hawa wahusika wote(G,mama,mama mkwe, Rachel)..... Ndo nikaja Sasa kuanza kupata picha ya nini kilitokea Ile siku, kumbe yule rafiki yake na G Kwa kujifanya sijui anamuonea huruma ndo alimpenyezea G zile taarifa ya mimi kua na dada yake pale kabla sijaenda safari, G nae akamvaa dada yake kumuuliza huko napo akaambulia majibu ya dharau na kejeli.... Hili nilikuja kulijua Kuna siku G amenitumia screenshots za mawasiliano baina yake na dada yake na yule rafiki yake...... Hapo hatusemeshani mi hata sikumjibu.... Kuna sms Rachel akawa anamuambia Sasa mdogo wake " we ndo ulianzisha tabia ya kuiba vya watu, huyo sio wako nilikua nimekuazima tu" 😔😔



Nikawa at least nimejua nini kimetokea



Ikapita wiki, Hali ipo vile vile, Kuna siku nikampigia mama mzazi Sasa...
 


Mimi: mama shikamoo, vipi Hali Yako huko?


Mama: marhaba, unaendeleaje huko?


Mimi: nashukuru Mungu mama, vipi Sasa mlimtoa mtoto huku shule ndo itakuaje Sasa?


Mama: aliyekuambia huku hakuna shule ni nani?


Mimi: Sasa na huku ada nilishalipa mbona?



Mama: Kuna mtu amekupigia Simu akikuomba ada???


Dah, nikakata simu pale naona Sasa Hawa wamejipanga kivita ngoja na mimi niwaache tu, hapo sister akawa ananipigia nikaacha kupokea Simu zake, Rachel nae amepiga zake kimya ni kama alijua ashalipua bomu anasikilizia matokeo tu



Nikaanzisha tabia Sasa, tofauti na kazi nikawa sio mtu social kabisa.... Mpaka nahisi kama nimerogwa, nikitoka kazini ntarudi zangu tu home Moja Kwa Moja ntakaa zangu tu chumbani ntakunywa pombe pale, mpaka nipate usingizi kesho tena ratiba Ile Ile, nikishatoka kazini Simu nilikua naiset ukipiga Wala siskii, nikija kuingia kwenye calls Nakuta missed calls zote hapo nachagua wa kumpigia wengine nawapotezea....


Wazo hata la kumfata G Sina hapo, Nina hasira tu naona huyu nae kilichompeleka huko nini, mama nae Nina hasira nae kwanini anachukua familia yangu bila ridhaa yangu, Rachel ndo usiseme, kiufupi hapo najikuta karibu Kila mtu namchukia, nikawa na roho flani sitaki kukubali kua Nina makosa, nikawa ni mtu tu wa kumlaumu Kila mtu....





Muda ukaenda Sasa na wao wakaanza kunitafuta, ntapigiwa Simu na mama,G,sister,ba mdogo,Rachel mama yake Yaani Ile circle nzima hapo ni kama nimepata roho flani tu ya kishetani Wala siwezi pokea Simu zao hata siku moja, Wala kujibu sms, nakumbuka G akawa ananitega pokea basi ongea hata na mtoto mimi wapi kimya tu



Pombe nazo nikaona hazitoshi, nikaanza Sasa vilevi vingine, ntanunua stock kubwa ya pariki ndani, ntakua na tambuu za kutosha ndani..... Ikawa nawaza muda tu wa kutoka kazini ufike nawahi home hapo ndo naona kama ni sehemu ambapo akili yangu inakua Ina amani, ntakunywa pombe pale, ntatafuna hayo na tambuu ntakula pariki pale yaani napata amani ya moyo tu



Nikaanza kua addict Sasa wa hivi vitu, nikitumia naona nipo Dunia ya kwangu kabisa ambayo Haina kelele Wala nini, naskia amani kabisa ya moyo!!! Ujinga wa haya mavitu Sasa nikawa usingizi sipati, najiona tu nipo high muda mwingi naskia Raha.... Kuna kipindi sitalala kabisa asubuhi naamkia tu kazini, mpaka macho yakaanza kubadilika rangi.....



Weekend ndo naweza nisitoke hata ndani kabisa, na haya ma vitu yanaua appetite kabisa Wala Sina hamu ya kula, ikafika mahali weekend kuzima Simu kabisa naona ni kitu Cha kawaida tu, hapo nyumba inaanza kua chafu Sasa muda wa kufanya usafi Wala hata siwazi



Kuna jamaa yangu walikuaga wa kishua Sana nakumbuka kipindi tupo chuo Kuna pills flani jamaa alikua anatumia zipo kama drugs kabisa, nikaja kumcheki sijui ikawaje nikamtumia Hela akanitumia kikopo flani hivi, nikaanza kutumia na hivo vidonge,ukimeza kimoja aisee unahisi Dunia ni Mali Yako, dah nikawa sijui Nakua kama Teja Sasa



Nikaanza kutembea Sasa na zana zangu kwenye gari, tupo kazini nikiona stimu zinapingua ntaenda kwenye gari najitupia mzigo narudi kazini, aisee Ile kitu ikaanza kuniongezea confidence, nikawa mtu naongea karibu na Kila mtu yaani najiamini basi tu mpaka nahisi kazini wakawa kama wananishangaa....



Sasa hapo pombe nikinywa ni kama siskii chochote, ikafika mahali ni kama pombe niliacha tu naona hazina kitu, mirungi nilijaribu ikanishinda.... Mimi hapo ntakula zangu pariki, ntameza kidonge kimoja ntatulia naanza kutafuna tambuu pale..... Nikiskiza mziki yaani nahisi kama mimi ndo nimeimba hio nyimbo



Hapo sitaki kabisa mawasiliano na mtu ni kama nikawa nimejitenga kabisa na jamii, ndo maana unaona mateja wanaishi wao Kwa wao, wanahisi jamii haiwaelewi...... Yakawa ndo maisha yangu mapya mzigo ukikaribia kuisha ntatuma Hela jamaa dar atanitumia faster tu, hizi tambuu na pariki mzigo mpya ukifika lazima ntapigiwa maana nilikua nanunua mzigo mkubwa kama stock vile




Hapo G kashalalamika kwenye Simu mpaka basi, sms zinakua nyingi mpaka ye ndo anaanza kuniomba msamaha.. hapo hata wanangu mi siwawazi, nikawa mbinafsi Sana najiwazia mimi tu, Kuna siku mama mkwe Sasa aliwahi kunifata mpaka kazini nadhani mama ndo alimtuma nikamwambia nipo busy tu ntamtafuta, yaani hivo tu, nikaja kumpotezea..... Rachel nae Kuna kipindi akawa ananisumbua nikaja tu kumjibu siku tukikutana ama zako ama zangu




Majanga!!!


Nakumbuka Kuna siku jumapili hapo npo ndani tu kama kawaida, nimekunywa pombe kidogo Sana kipindi hicho hata siipendi kivile, nshajitupia mizigo yangu kama yote nipo stimu vibaya mno, Sasa hivi vitu tofauti na Bangi ni kua nikitumia Nakua active Sana, Kuna feeling flani ya Raha hivi tofauti na Bangi ambayo ni kama inakupooza(kusizi)..... Ghafla naanza kupata joto Kali Sana... Nikaingia bafuni nikajimwagia maji pale hapo sijavaa chochote nipo peku, Ile nitoke Sasa sijui nilikosea step vipi nikateleza nikaanguka, aisee sijui nini kilitokea nakuja zinduka ishakua usiku kichwa kizito hapo utasema nimebeba scania kichwani... Bado npo uchi aisee, nikajikongoja pale nikaenda kuvaa boxer nikawa nimekaa pale.... Hofu ikanitanda naona ningekuja kufa mimi Leo kifo Cha aibu namna hii, hapo nawaza sijilaumu mimi nawalaumu tu watu walionizunguka naona kama wao ndo wananifanyia makosa... Siku hio hio nikameza tena pills pale nikala mavitu yangu yaani Kwa hasira Sana, kesho nikazima Simu sikuenda kazini, jumatatu nayo ivo ivo nipo tu ndani maisha Yale Yale sikwenda kazini tena kesho yake, Simu nimezima hapo... Kula nakula mara Moja hapo utakuta nimekula kitu simple tu nakaanga ndo inakua imetoka, kazini sijatoa taarifa yoyote, hio jumatano hapo nipo stimu vibaya naskia geti linagongwa kumbe ni wafanyakaz wenzangu, jamaa wanaingia ndani wanashangaa huyu jamaa anaishi vipi... Wananiangalia pale hawanielewi.... Jamaa wanchek pale mezani Kuna vitu hawanielewi, mmoja akaviangalia pale ananiuliza mbona jamaa unatumia hivi vitu una shida gani aisee.....


Wakajadili pale naona wananipotezea muda tu natamani hata kuwafukuza ila kaheshima flani tu hapo, mmoja akasema huyu jamaa inabidi nimpeleke Kwa mtaalam wangu Fulani kashachezewa huyu.... Basi bana tukaongea pale wakaondoka....


Nikapitisha wiki sijaenda kazini bila taarifa yoyote Ile, hapa nimeelezea Kwa ufupi Sana ila Hali ilikua mbaya nilishaanza kua nusu Teja kabisa....



Basi tu Kuna siku flani namuwazia mama mzazi na maisha nayoishi,nawaza wanangu hapo,sijui ikawaje tu Nikapata msukumo flani nikampigia mama Sasa nikamueleza mambo mengi tu pale hapo najihisi Sina amani kabisa mama badae akaniambia "njoo tu huku utengenezwe huko washakuchezea"
 
Back
Top Bottom