Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka unawaza hapo nyuma ulikosea wapi? Part[2]

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka unawaza hapo nyuma ulikosea wapi? Part[2]

Epi 2


Siku hazigandi weekend hio ikafika, kwanza nawaza it's weird kuonana na mtu hamjaonana mda mrefu ivo, anyway namuuliza ni wapi huko tukutane? Ananiambia nakuja kufata twende wote, nataka kukataa ila anatia msisitizo anyway nikam elekeza akaja, kafika kwanza it's just weird sana, tunashangaana tu na vicheko vya hapa na pale..... Tumekaa Sana tunaongea, vibe checking na nini..... Samira ni binti flani dini Bado ipo kwenye damu... Yaani hata ukimuangalia mavazi kajitanda Kila mahali anakuachia sura tu na mikono ya kuona.... Story mbili tatu pale tukaondoka.... Location...? Food spot Moja mjini kati, na mimi Sasa sio mlaji kivile ila hakuna shaka..... Tunakaaa pale ongea Sana mambo mengi, yeye yupo busy kuniuliza kuhusu familia na nini... Nakua muwazi tu ila mambo mengi hata sikumwambia....




Hapo mi hata mambo ya mapenzi siwazi Sana maana napiga mahesabu hapa hamna kitu tena tunaweza tengeneza kati yetu, nshakua mtu wa familia na nini, basi bana tumetoka hapo tumehama mahali pengine tulivu tu, nikaagiza zangu pombe kidogo maana naona sielewi, akaanza kucheka anauliza

"We patrick hujaachaga pombe tu?.."

Namwambia dada hii ni kama ibada japokua Sasa Muda unabana ila ndo ivo muda ukipatikana tunatumia tu


Hapo ndo anaanza kuniambia Kuna mahusiano alipitia ila hayakwenda vizuri na nini na yeye akaanza kunywa ila alishaacha muda Sana .. nikaanza kumtania


"We ambavyo ulikua hupendi pombe mpaka ukaanza kunywa inaonekana jamaa alikuumiza Sana na nini"


Uzuri Sana Samira nikaja gundua ni mtu flani yupo very open, hamna Mambo ya kufichana na nini, basi kweli akawa ananielezea kua walikua deep Sana na mshkaji sema tu Kuna mambo yeye Samira alikua anakosea sijui Kwa maksudi au vipi maana Kwa maelezo yake aliniambia alijua jamaa hawezi kumuacha hata ikitokea vipi, basi baada ya mahusiano ya ugomvi na nini wakaja kuachana ndo Binti akaniambia akaanza kunywa na nini japo Kwa Siri maana aliniambia kwao wangejua ingekua balaa Sana familia ya dini Sana wasingemuelewa....



Namuuliza Sasa is it over na jamaa au ndo mmepeana tu likizo, ananiambia ni muda tu yeye hata ashasahau.... Akaanza kunidadisi Sasa na mimi kuhusu maisha yangu ila nikawa mjanja nikampa details za juu juu Wala sikutaka ajue mambo mengi kuhusu mimi..


Basi tumekaa pale akaanza kunielezea kuhusu career yake na biashara zake.... Akatoa Simu akaanza kunionyesha biashara zake anavyofanya via hizi social platforms... Kuangalia tu I could tell she is very successful, sema Sasa mimi kwenye hizi social outings Wala sipendi Sana kuongelea mambo yangu ya biashara Wala kazi, sijui kwanini ila Niko hivyo tu.... Tumekaa Sana kule mpaka usiku mnene baadae akanirudisha hotel nilipokua nimefika, kufika huko tena tumekaa Sana kuongea tu hapo parking mpaka baadae akaniaga akaondoka



Amefika kapiga Simu ni kama tuliongea tu mpaka asubuhi, kesho yake nafatwa tena tumezurura mjini kanipitisha kwenye maeneo yake ya biashara japo nilikua sitaki ila she insisted, baadae tumeenda sehemu tu maongezi na kucatch up, Sasa hizo route zote tunafanya hataki nilipe any bill hata nikisisitiza ananiambia relax tu we ni mgeni wangu Wala usijali, naona sio poa ila na play along tu.....




Jumatatu mi nipo huko kwenye kazi za watu Sasa, mara naitwa na receptionist ananiambia Nina mzigo wangu umetumwa hapo, kwanza nashangaa mzigo gani ukizingatia ile ofisi mi na mwenzangu ni wageni, anyway namwambia ngoja nikimaliza kazi ntakuja kuupitia ... Muda unaenda baadae naenda nakutana Samira katuma maua na sms cards na nini, kwanza nashangaa, pili naona kama ni kunichoresha ofisini pale ntaanza kuonekana lover boy... Ila it felt good... Baadae natoka nampigia namuambia suprise Yako nimeiona anaishia kucheka tu, ananiambia kama tutaweza kuonana namuambia it's Monday afu nimechoka ntamcheki ratiba zikitulia kidogo



Sasa kuanzia kesho yake ikawa sama routine, Kila siku ntakutana na maua mapokezi muda wa kutoka, najisemea hii Sasa mbona mpya, jamaa yangu niliyetoka nae mwanza Kila tukipita akawa anacheka tu.... Anantania.

" bwana mdogo fanya wakupe tu full transfer huku sikuoni ukirudi mwanza Kwa Hali hii"


Nikawa namuambia tu kiutani, dar huku nilikimbia mwenyewe sioni nikirudi tena Kwa hiari yangu mwenyewe


Hapo maongezi na Samira yamepamba moto tunawasiliana Sana tu, huku nae mke ananiambia niwe makini mjini huku.... Acha tu...


Ijumaa hio, tulikua tushapanga kwenda mahali na Samira, imefika tumetoka.... Baadae naona Sasa nivunje ukimya, tumeongea mambo mengi nikawa namuambia Kwa Hali tuliyofikia chochote tunachohisi kipo kati yetu ni illusion tu Wala hakina uhalisia, mi nishakua na familia na nini, hata tukisema tufanyaje Hali ishakua complicated Sana Wala hakuna Cha maana kinaweza kua kati yetu




Akawa anacheka tu, ananiambia "kijana acha kuchukulia maisha serious ivo, ride with the tide,kwanini mi nimefanya nini au unahisi nataka nikuchukue kutoka Kwa mkeo?"



Hapo na mimi Sasa naanza kuhisi nipo njia panda, maana akili inakataa ila kamoyon Nako kanashinikiza mambo mengine, tumekaa Sana pale naona tunaanza kuboreka namuuliza tuhame hapa twende wapi.... Mara ananijibu it's up to you, wewe sio ndo mwanaume, the ball is in your court...



Anyway naona moyo nao ukauzidi ushawishi akili, tumetoka hapo mpaka nilipofikia, ndo mara ya kwanza namkaribisha ndani.... It was a wild night, hakuondoka hiyo siku.... Whatever happened happened!!!!. Baadae Sasa napata call kutoka Kwa wife, Kuna ka feeling flani Cha kujilaumu, nawaza nipokee hapa hapa mbele yake au nikaongelee pembeni, badae naona Sasa hapa Cha kuficha nini, napokea hapo hapo tukaongea kama dakika 20 tukaagana ivo....


Baada ya Simu Sasa, Samira akaanza niuliza mambo mengi kuhusu mke wangu, hapo namjibu juu juu tu sikutaka kumpa details Sana, badae anaanza kuniuliza vitu vya ndani kabisa kama sexual life na mke wangu na nini, anyway tukaongea Sana hio siku, Bado nikawa namuuliza anawaza nini kua na mimi maana huko mbele ni kama mi naona Giza tu, basi ye anaongea kimasihara tu ananiambia hata mama yake alikua mke mdogo Kwa baba Yao yeye Wala Hilo swala Kwa Sasa hataki kuwaza kwanza.....



Kesho yake tumekaa pale ananiambia anataka kunipeleka mahali, Mida ya mchana tumetoka nashangaa mtu kanipeleka kwake, akaanza kulalamika kua hataki tena tulale hotels na nini anajiskia ovyo, siku nikutaka tuonane niwe naenda kwake, hapo mi akili ni kama inakataa ila basi nasema acha tuone itakuwaje huko mbele.... Rest of the weekend huko nimepikiwa, mapenzi kama yote mpaka inafika siku ya kazi nimeondoka.... Hapo huombwi na shilingi Moja



Nikaanza kuona naanza ku catch ma feelings Sasa, Kila nikizuia hisia ndo nazidi kuzama tu, akaja kuniambia amemwambia dada yake mkubwa kuhusu mimi, nimuuliza Sasa kwanini umemwambia? Ananiambia tu nataka akujue sitaki tufanye Siri maana we ni mtu wangu, akaniambia siku akapata muda atanikutanisha tuonane, mmmhh hapo sielewi naona tu kama sio sawa Wala nini, katikati ya wiki tumekutana ndo nikaanza kumhoji vipi ulimwambia dada yako kuhusu situation yetu ikoje, anajua kama mimi nipo mwanza na Nina familia au ulimficha, yeye ni kucheka tu akatoa Simu akaniambia angalia mwenyewe uone tulivyokua tunabishana....



Hapo nawaza wanabishana nini Tena, chukua Simu nakuta Sasa wanavyochat, aisee dada mtu Kawa mkali kinoma, analalamika Kwa mdogo wake kwanini ameamua kua na relationship na mme wa mtu, tena jamaa mwenyewe ana watoto wanne, aisee huko kamchamba Sana anamuambia wewe umerogwa si bureee, una maisha Yako mazuri huyo mwanaume we nini Sasa, Bora hata kipindi kile ungeolewa na flani ningekuelewa



Inaonekana kuna mtu alikua na interest Binti akachomoa, kiufupi huko dada mtu kanisagia Sumu si utani Samira anajieleza weeee ila dada mtu hakubaliana kabisa na Hilo swala..... Kamsema mpaka basi.....



Nikiwa namuambia Samira Sasa kua dada yake ana point pia, kama nilivyokuambia mwanzo situation yetu ishakua ngumu Sana kua wote, yeye ananiambia kua yeye ndo mwenye maamuzi na maisha yake na nini... Hataki mtu mwingine ampangie, anataka kuishi maisha anayooona yanampa furaha....



Kibishi hivo hivo tumeenda mpaka weekend ndo Sasa naalikwa nikakutane na huyo dada mtu ambae nilishajua hanikubali hata kidogo japokua sijawahi kuonana nae, mwanzo sikutaka kabisa ila nikaombwa Sana na Samira akiamini huenda akinijua atabadilisha mawazo na nini, ikafika weekend tu nikasema sawa hivo hivo tu maana tulikua tunabishana kuhusu hili swala kama siku 2 nyuma.....


Imefika weekend, nikaenda Kwa Samira maana waliambia wao watakua nyumbani....


Badae nafika napokelewa mara namuona dada mtu Kwa bashasha ananikaribisha " shem wangu karibu Sana"


Ila watu ni wanafki sana
Tuko na wewe mpaka urogwe Na mdogo akupeleke kwa mganga 😂👌
 
Back
Top Bottom