Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

Maelfu ya watu hasa watoto na wanawake wamekufa sana huko Gaza.

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wamekufa sana huko Goma DRC Congo.

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wamekufa sana Afghanistan.

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wamekufa sana huko Yemen, Syria, Lebanon, Palestina.

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wamekufa sana huko Tigray Ethiopia.

Maelfu ya wanawake na watoto wanakufa sana kwa ukame na njaa huko North Kenya Turkana.

Na huyo Mungu hajawahi kusaidia lolote wala kutenda muujiza wowote!!!

Vimbunga Idai, Hidaya, Chido vimeua maelfu ya watu huko Msumbiji na malawi. Huyo Mungu hajafanya chochote.

Matetemeko ya ardhi yaliyopiga Syria na Uturuki yameua maelfu ya watu na huyo Mungu hakufanya chochote wala hakutenda muujiza wowote.

Huyo Mungu hana msaada wowote wala muujiza wowote ule kwa binadamu.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

TRASH GOD...🚮
 
Kwa hiyo mkuu kuna namna Mungu mkamilifu kaumba vitu visivyo vikamilifu ?
Miafrika bado tu toleo la Mwisho katika uumbaji...itoshe kusema udongo ulomfinyanga mwafrika ni wa kichuguu mabaki baada ya kuumbwa kumbikumbi na mchwa.
 
Au huku Mungu kaua hawa watoto labda kuna kitu amekasirika mkuu🤔
Mungu gani anaendeshwa kwa mihemko ya hasira?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?

Huyo Mungu kama ana hasira, Asituletee sisi hayo mahasira yake..!!!

Apeleke hukoooo!!
 
Niliamini kwenye anachokisema(Neno) lake halafu ndipo akaanza kuudhihirisha uweza wa mkono wake hodari(Miujiza). Ni mingi mno!
 
Huyo Mungu wala hakukusaidia kwa chochote.

Huyo Mungu Alishindwaje kukukinga usipatwe na hiyo ajali ya kukatwa na kitu chenye ncha kali?

Shukuru hao waliowahi kukutibu la sivyo unge endelea kukawia ungekufa, Na huyo Mungu asingekuwa na msaada wowote kwako.
 
Nililipwa kiasi kikubwa cha hela kwa ajili ya shughuli fulani,ila nikazifanyia shughuli tofauti,tajiri yangu akanisakama sana hadi niliposikia amefariki nikajua Mungu yupo.
Kila mtu huweza kufariki muda wowote tu.

Kwa hiyo tajiri yako kufariki sio kigezo cha kusema Mungu yupo.

Ni imani zako tu.

Mungu hayupo.
 
Kuwa hai tu mpaka muda huu unasoma hii comment ni muujiza ndugu
Uhai hauna muujiza wowote ule.

Kila mtu lazima atakufa na hatuta kuwa na uhai tena.

Hivyo suala la uhai sio muujiza.

Suala la uhai ni la muda tu, kabla kifo hakijaja.
 
Watadai tulipewa free will
Freewill haipo.

Tunazaliwa bila kuchagua wala kutaka.

Hakuna freewill ya mtu kuchagua uzaliwe ama usizaliwe.

Unashtukia tu umesha zaliwa bila kuamua na bila kutaka.

Huu tayari ni uthibitisho tosha kwamba hakuna freewill.

Tunazaliwa kwenye dunia iliyojaa shida na mahangaiko ya kila aina bila kuchagua wala kupenda.

Freewill haipo.

Freewill is an illusion.
 
Nilisahau kufunga duka asbh ilkuwa nawahi ibada jpili asubh then, narudi mchana nakuta kila kitu vile vile kuanzia money, bidhaa adi phones etc...
Tukio hili sijasahau ukuu wa Mungu kwakweli. Yupo.
 
Alafu akina Kiranga wakiwaambia mthibitishe mnaanza kujilizaliza!
Kuthibitisha ni ngumu ila Mungu anaweza kujidhihirisha maishani mwako kimyakimya ukabaki kusema hi!

Mimi mpaka sasa sijajua kama Mungu yupo ila nikikataga tamaa nikiamuru mambo yanatokea kimiujiza... Sasa sijui ni Mungu anatenda hiyo miujiza au ni mimi
 
Ameen
 
Mungu anatumia watu katika kukusaidia mkuu
 
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa mtu asipopokea muujiza hawezi kuamini? Ni kipi kinatakiwa kitangulie kingine kati ya kuamini na muujiza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…