Ushawahi Kupokea muujiza gani ukaamini kuwa Mungu yupo?

Mungu yupo, amini usiamini hainihusu....

Nasema pokea sifa na utukufu Mungu ๐Ÿ™
 
Ukiwachunguza wanatoa ushuhuda wa muujiza waliokutana nao wakaamuni mungu yupo, utakutana nao jumapili wanaomba toba mbele ya mifuko miwili ya cement iliyochanganywa na kokoto
 
Mungu ni muweza.
 
Mkurugenzi fulani aliniachisha kazi bila sababu ya msingi kumbe alikuwa na mtu wake niliumia mno nkamuuliza Mungu ntaishije ..kwa nn hili limetokea nimekosea wapi ..Tramp akafanya yake saivi kawa jobless kweli Mungu yupo na anajibu kwa wakati
 
Shida ya kiranga na wafuasi wake wanataka kulinganisha spiritual world na material world kitu ambacho hakiwezekani abadani.

Spiritual world iko dominated na faith, na faith zote zimeelekezwa kwa Mungu kama Mfalme wa watu wamuaminio.

Imani ndiyo silaha ya binadamu wote haijalishi unaamini katika kitu gani ila iman yako ndiyo chanzo cha mwenendo mzima wa tabia, matendo na maisha ya binadamu kwa ujumla.

Imani huleta tumaini.
Imani huleta amani na utulivu kwa binadamu.
Imani humsukuma binadamu kuamka hasubuhi na kuamini kuna kitu kinachomsukuma aamke akafanye kitu akiamini anaweza kukitimiza na kikaleta manufaa kwenye maisha yake.

Kuamini katika Mungu kunatokana na jinsi mtu alivyoikuza imani yake na namna imani yake inavyofanya kazi.
Wengi wenye imani juu ya uwepo wa Mungu tunaamini Mungu ndiyo ameumba ulimwengu na viumbe vyote vilivyomo kutokana na complexity ya viumbe vyenyewe, nikiwa na maana kwamba haikuwa rahisi hivi vitu katika ulimwengu kutokea vyenyewe tu bali kuna alieviunda ndiyo maana tunaamini Mungu ndiye ameviumba.
Huenda tafsiri ya neno Mungu inapelekwa kuwa ni kiumbe kama binadam ndiyo maana watu wanacomplain wakitaka kumuona, la hasha Mungu ni nguvu iliowezesha vyote kuwa hapa vilovyo na nguvu hiyo wajuzi wa mambo wa kiroho wanaamini inasifa kama za kibinadamu ikiwemo kuona na kusikia ndiyo maana inasemekana tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, ndiyo maana tunaambiwa tuabudu na kusifu nguvu ya kiungu hupenda matendo kama hayo.

Kiranga yeye ni mtu anaeamini katika material world na science, anachokitaka yeye ni kulonganisha spiritual world ifanane na material world, kwa kuwepo na facts, evidences ili aprove kila kitu.

Spiritual world ni ulimwengu wa vitu intangible, ila hisia na imani ndiyo nyenzo kuu ya kuishi ndani yake.

Naweza kuuliza je binadamu hana roho?
Je kuna mtu anaweza kuishika roho?
Je binadanamu hatumii oxygen?
Kuna mtu anaweza kutuonesha oxygen tukaiona kwa macho tuiprove kwamba ndiyo hii?
Kwahiyo dunia ndivyo ilivyo, imegawanyika katika sehemu mbili na moja ni invisible world nyingine ni visible world.

Mungu ni King wa watu wanaoamini katika spiritual world haimaanishi kwamba hayupo.
Yupo ila spiritually.
 
aise toa ufafanuzi wako juu ya hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ