Wakuu, habari za jioni,
Katika maisha, mtu anaweza kuwa na kariba ya kawaida kabisa kiasi cha mtu mwingine kutojua au kutozoea tabia yake, hali inayoweza kusababisha kudharauliwa. Hata hivyo, baadaye watu hao huweza kugundua kwamba mtu waliyemdhani si wa kawaida kabisa na mawazo yao yanabadilika.
Iliwahi kunitokea siku moja nilipoenda ofisi fulani na kuwakuta wafanyakazi wote wakiwa wanawake. Nilipowasalimia, mmoja tu alijibu, tena kwa nyodo sana. Nilipowaambia kwamba nilihitaji bahasha zilizoachwa na bosi wao, waliniangalia kwa dharau. Wakati huo, nilikuwa nimevaa mavazi rahisi—pensi na sandle—na waliniuliza, "Wewe unazichukua kama nani?" Nikajibu kuwa nimeagizwa, lakini bado walinidharau na kuniambia, "Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi."
Kumbe nilikuwa nimekuja na BMW nje ya ofisi. Walipokuwa wakijiandaa kuondoka, nikashuka ngazi na kwenda kwenye gari langu. Nilipofika kwenye eneo la kuegesha, walionekana kushangaa. Kwa heshima, nikawaambia, "Ingieni niwasogeze." Walikubali, lakini ndani ya gari walikuwa kimya kama wamemwagiwa maji. Walianza kucheka na kutabasamu huku wakifurahia upepo wa AC. Mmoja aliyekaa mbele aliniomba namba yangu ya simu, lakini sikufanya juhudi zozote za kuendelea mazungumzo naye, nikalipotezea tu.
Je, wewe umewahi kudharauliwa na watu, familia, au marafiki kutokana na mwonekano au hali fulani katika harakati za maisha?