Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Wahi daladala = chai
Demu alikuomba namba= chai
Na kama kweli uliebnda huko basi www ndio ulijetegesha tegesha hadi waondoke ofisini ili uwaoneshe una gari.

Japo kastory ni kama kakutunga hivi.
 
Heshimu ofisi za watu kwa kuvaa kiheshima. Pensi na sendo ni kuonyesha dharau. Ulianza wewe kuwadharau.
muonekano wako ndiyo uliosababisha udharaulike na hata ulichoandika huku bado unajidharaulisha. Huwezi kwenda ofisi yoyote na pensi na sando hiyo moja ni dalili za ushamba. Ofisini kuna aina ya mavazi yanakubalika. Pili kujisifia sijui BMW nao ni ushamba mwingine. Kuna watu hata magari hawana lakini wakifika sehemu wanapewa heshima siyo kwa anachomiliki bali jinsi muonekano wake tu na heshima yake.
 
Aisee Huwa mimi linanikuta sana sana , sababu ni mavazi , na ndevu niziachia ,siku nimeingia bank card yangu ilikuwa imepasuka nitengenezewe nyingine yule demu anaongea na kuniona Sina hekima kabisa nawezaje pasua card na imechoka dah watu wanasikia ,sijui aliona nini kwenye account yangu akaishia tu kuwa mpole na sasa Huwa namkula mara moja moja nikipita mbeya ila Haina maana nimetoboa najitafta kwa shida sana
 
Wakuu, habari za jioni,

Katika maisha, mtu anaweza kuwa na kariba ya kawaida kabisa kiasi cha mtu mwingine kutojua au kutozoea tabia yake, hali inayoweza kusababisha kudharauliwa. Hata hivyo, baadaye watu hao huweza kugundua kwamba mtu waliyemdhani si wa kawaida kabisa na mawazo yao yanabadilika.

Iliwahi kunitokea siku moja nilipoenda ofisi fulani na kuwakuta wafanyakazi wote wakiwa wanawake. Nilipowasalimia, mmoja tu alijibu, tena kwa nyodo sana. Nilipowaambia kwamba nilihitaji bahasha zilizoachwa na bosi wao, waliniangalia kwa dharau. Wakati huo, nilikuwa nimevaa mavazi rahisi—pensi na sandle—na waliniuliza, "Wewe unazichukua kama nani?" Nikajibu kuwa nimeagizwa, lakini bado walinidharau na kuniambia, "Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi."

Kumbe nilikuwa nimekuja na BMW nje ya ofisi. Walipokuwa wakijiandaa kuondoka, nikashuka ngazi na kwenda kwenye gari langu. Nilipofika kwenye eneo la kuegesha, walionekana kushangaa. Kwa heshima, nikawaambia, "Ingieni niwasogeze." Walikubali, lakini ndani ya gari walikuwa kimya kama wamemwagiwa maji. Walianza kucheka na kutabasamu huku wakifurahia upepo wa AC. Mmoja aliyekaa mbele aliniomba namba yangu ya simu, lakini sikufanya juhudi zozote za kuendelea mazungumzo naye, nikalipotezea tu.

Je, wewe umewahi kudharauliwa na watu, familia, au marafiki kutokana na mwonekano au hali fulani katika harakati za maisha?
"Haya chukua, wahi daladala zimejaa sasa hivi." Really???? Mkuu...
 
umetumia nguvu sana kutaka kutuaminisha kuwa una BMW..acha ushamba..wanawake wengi hawayajuagi magari..wao wanajali kama linatembea basi...una kariba ya KIHAYA...
 
umetumia nguvu sana kutaka kutuaminisha kuwa una BMW..acha ushamba..wanawake wengi hawayajuagi magari..wao wanajali kama linatembea basi...una kariba ya KIHAYA...
We ndio unaroho ya kishamba kucritisize anachokizungumza mtu na kilichotokea sasa kariba ya kihaya ndio inathibitisha kabisa 100% ulichokuwaza, njoo na positive mindset sio upuuzi uliouabdika, inathibitisha kitu kilichopo kichwani mwako!!!
 
Kuna watu vichwa nunda hata wakikuona na hiyo BMW yako Bado watakuchukulia poa tu.. wenyewe wanachojari kula, kulala,kuamka, kazini, imeisha iyo
Shida ya watanzania Mna NEGATIVITY sana Yani mtu akionesha sentence zinazodhaniwa ni kujigamba basi kosa kubwa sana, nani kasema najionesha kuwa Nina BMW? Hapa nimeandika kilichonitokea, na si masuala ya watu kuniona na kunipotezea sasa yanaingiliana vipi na kile nilichokisema kama sio UPUMBAVU Ninini akilini mwako mkuu??
 
Mimi kazi yangu ina jina kubwa sanaa.Sasa watu wanafikiri nalipwa mamilioni masikini ya Mungu ,kumbe nakunja mia tisa na chenji kabla ya makato mpaka kurudi laki nne na kitu mfukoni.Basi watu mara waniombe niwaazime milioni kumi,mara niletewe prado linauzwa,mara mgeni rasmi wa kuongoza harambee.Kadi za harusi ndio hazina idadi.Kumbe ni masikini mwenye jina kubwaaaa.
Ndio hivyo mkuu kikubwa ni kumantain status tuu
 
Back
Top Bottom