Ushawahi zimikiwa na jiko la gesi ukiwa unapika?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna siku nimekata nyanya vitungu karot na pili pil hoho vzur nmeweka kwny sahani kwa ajiri ya kuunga nmeweka mafuta kwny sufuri inachemka ghafla ges imekata afu mtung mkubwa nkaishiwa poz ikabid nmwage kila kitu jiko la mkaa nlikuwa sina
Nunua pressure cooker multi purpose ya umeme., Gesi ikikata unapikia huko.
 
Pole Zurie
 
Pole sana, hizi gesi zinaweza kukufanya ukala vitu vibichi.
 
Imeisha muda si mrefu hapa alafu nimetoka kuinjika maharage ya kukopa kwa Mangi. Akiba nina 1000 tu... hapa navizia watu walale nikaokote mbao nichemshe nje huko na moto wa kuni maana hali sio hali
Hahaaaaaaa kwa nini uvizie mkuu, kuwa huru okota tu
 
Nimejisikia vibaya kuuona huu uzi maana nilihonga bila kujua, ipo hivi Dem wangu alinikaribisha kwake weekend kuinjoy .sasa ilikuwa mchana anajipinda kunipikia kidume gas ikakata akaniangalia kwa huruma,akaita "mmewangu shetani mbaya amepeleka gas".

Nilimpa noti kadhaa akajaze. (UWABATA I'm sorry)
 
Hahaaaaaa pole sana
 
Kama ulilia itakua ulikua na kipre [emoji1768]
 
Kuna siku hili lilitokea nakumbuka nilikua napika kwa jiko la mkaa nje mvua ikanyesha nikazima moto kwa maji nikaamisha chakula ndani kwenye gesi mweeee!! πŸ˜…πŸ˜… Gesi dakika kadhaa kwishaaaa mvua inayesha mida umeenda pesa hakuna moto nimezima

Nilikoma
 
Nna backup ya jiko la umeme plate moja....kabla nlikuwa natukana siku nzima, kifua kinajaa, hasira na jazba gesi ikikata na kitu hakijaiva.
 
Hii imenifanya ninunue plate nne moja ya umeme gesi ikiisha unahamia kwa umeme hapo vipii
 
Mie imekata jana bahati nzuri nilikua nimemaliza pika bagia zangu za kinda.maziwa walikua tayar wala sikupati tabu ..nawaza ninunue kimtungi kidogo cha dharula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…