DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Kwa Tundu Lissu na Freeman Mbowe uwenyekiti wa CHADEMA ni title na umaarufu na wala hauta badilisha sana majukumu ya wote kwenye chama. Mjumbe ambaye anataka kuwa mwenyekiti na hayupo kwenye kamati kuu ya chama, anaweza kupata mabadiliko makubwa ya ushawishi na uwezo wa kutekeleza shughuli za chama endapo ikitokea atashinda uchaguzi na kuwa mwenyekiti wa chama.
Tundu Lissu hata akiendelea kuwa makamu mwenyekiti wa chama, anao uwezo wa kukitumikia chama kwa kufanya mengi akiwa na ushawishi mkubwa na kwasababu hiyo uwenyekiti haumuongezei mengi ya ziada. Mfano mkubwa ni jinsi ambavyo Tundu Lissu aliweza kugombea nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi uliopita bila kushika nafasi ya uwenyekiti. Vilevile Freeman Mbowe tayari yupo kwenye kamati kuu ya chama nani mmoja wa waanzilishi wa CHADEMA. Hii ina maanisha kwamba hata asipokuwa mwenyekiti, ushawishi wake na mchango wake kwenye chama hauta badilika sana.
Mzozo huu unaweza kuwa na maafa endapo ushindani huu utaleta mikwaruzo na migawanyiko kwenye chama kati ya wafuasi wa Tundu Lissu na Freeman Mbowe na kama wahusika hawa wawili watashindwa kuendesha shughuli zao kama team. As a neutral, naona kama Freeman Mbowe bado anahaki ya kugombea hata kama amekuwa mwenyekiti kwa muda mrefu sana ila wanachama wa CHADEMA ndio wanatakiwa kutambua kwamba labda kigezo hiki kina mnyima Mbowe sifa ya kuwa mwenyekiti.
Je kuna uwezo upi wa ziada wa kutekeleza majukumu ya chama ambao mwenyekiti wa CHADEMA anapata ambao wajumbe wa kamati kuu wengine wana pungukiwa?