Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Watashinda bila kudhaminiwa na chama kwa mujibu wa katiba?
 
Mohamed Said,

Mkuu Maalim Mohammed Said, kwanza asante kuchangia uzi wangu huu na asante ya pili ni kwa wewe kuwa mchangiaji wa kwanza, umelifanyia jambo kubwa sana bandiko hili bila wewe kujijua.

Baada ya kubandika tuu uzi huu nilikimbilia Kanisani kwenye ibada. Baada ya ibada nimekuja kufungua if baada ya masaa 4, nikakuta bandiko liko page 7!. Kuna mabandiko huwa nachangia na yana hoja muhimu sana ila sio tuu linaishia page 1 tuu, bali inakuta limeishia post hiyo hiyo moja ya the thread starter na halikuchangiwa na mtu hata mmoja, mfano ni bandiko hili


Hivyo kitendo cha wewe Mkuu Maalim kutia mguu humu kama mchangiaji wa kwanza kumelifungulia njia bandiko hili na amini usiamini ujumbe huu utawafikia walengwa, japo jf haitatajwa.

Hii ni kufuatia zile powers ulizonazo, nakuomba tena na tena katika mabandiko ya maslahi ya taifa, tuweke tofauti zetu pembeni tutangulize mbele maswali ya taifa kwa watu kama nyinyi kutumia vipawa vya powers mlizojaaliwa ku push forward ajenda za kitaifa kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Katika hili la serikali za mitaa, ni Chama kimoja tuu CCM ndicho kina ofisi kila kata, wana tawi lila mtaa na wana ujumbe wa shine kila nyumba 10 hivyo wagombea wa CCM wamejaziwa hizo fumu na kuhakikiwa. Vyama vingine havina hata ofisi ya wilaya achilia kata na mitaa hivyo wagombea wao ni kama watoto yatima. Ndio maana hapa nimemuomba rais Magufuli aingilie kati kwa kuruhusu wagombea wote wa vyama vyote bila kujali hizo kanuni ili tuu kuruhusu ushindani wa haki.

Tanzania hatuna utaratibu wa kufanya utafiti wa kisiasa ndio maana ile 2005 tuliandikisha wapigakura milioni 22, waliojitokeza kupiga kura ni milioni 12, JK alishinda kwa kura 9,123,952 ambayo ni zaidi ya asilimia 80%. Watu milioni 8 walijiandikisha lakini hawakujitokeza na nobody cares kujiuliza why!.

Uchaguzi wa 2010 walijiandikisha watu milioni 21
Waliojitokeza kupiga kura ni 8,626,283 – 42.84%
Watu milioni 12 hawakujitokeza, nobody asked anything!.

JK alishinda kwa kura 5,276,827 sawa na asilimia 61%. Kutoka asilimia 80% hadi 61% and nobody asked anything. Hakuna research yoyote iliyofanyika.

Kwa vile wewe ni reacher tufanyie research na utufundishe hiyo law of probability.

Swali moja linabaki, hili nililopendekeza humu lisipo tekelezwa na hao waliosusa wakiendelea kususa, what will happen next?.
P
 
Watashinda bila kudhaminiwa na chama kwa mujibu wa katiba?
Kama waliishakabidhi fomu za kugombea kabla ya tamko maana yake waliishadhaminiwa na vyama vyao. Ndio maana nikasema, inabidi wasifanye kampeni ili kuheshimu maamuzi ya vyama vyao. Na ikitokea wakshinda ili wasichonganishwe na vyama vyao, busara ni kujiuzulu tu.
 
Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.
Jamani huyu binadamu kwa miaka hii minne aliyokaa madarakani hamjamjua tu? Bwana yule hataki kitu kinachoitwa upinzani, hataki kabisa kusikia. Hilo la kusema atawasamehe haitatokea kamwe. Hataki upinzani na ameonesha kwa vitendo.
 
Hata mwenyekiti wa ccm taifa ukiachilia mbali rais Magufuli, hawezi kukubali kushindana kwa usawa, anafahamu hiyo itakuwa kuiondoa ccm madarakani.
 
!
!
Watu Hawachagui Raisi Kwenye Uchaguzi Huu. Unapotaja Reli Sijui Ndege Elimu Bure Na Ushuzi Mwingine Kama Huo Ni Mwenyekiti Gani Wa Mtaa Ataweza Kununua Kwa Ajili Ya Mtaa Wake?
Kuna Wasomi Wengine Hovyo Sana Aisee
Wasomi karibu wote wanafanana,kwa hapa kwetu huwa wanatoka Mlimani,wakiongozwa na Profesa wao yule Kabundi.
 
Pascal Mayalla,

Anayofanya Meko sio mapya kwa watz bro! Kipya ni kwamba anajichimbia kaburi lake mwenyewe. Hata mkoloni alijenga reli, barabara, shule na vingone vingi hadi leo tuvitumia ila akina Nyerere walimng'oa mkoloni!! Watz wanataka hayo yote ila linda sana mshikamno wao na umoja wao uliojengwa miaka nenda rudi, kwa jasho la damu na maji! Leo hii anatokea mtu anajifanya ni kiongozi wa malaika mbinguni yupo duniani na anatawala anavyotaka! Time will judge us coz inapandwa mbegu ambayo sio kasumba yetu kabisa na madhara yale ni mabaya sana.

Mungu atusaidie, ila kiukweli Meko ni tatizo kwa Taifa na Africa kwa ujumla! Kikwete aliyeleta hii kitu ipo siku atajibu. Maraisi wa wastaafu wote wanaangalia na kukenua meno, unyama watz wanaofanyiwa hata Idd Amini hakufanya!

Mungu ibariki Arusha!
 
Nguruvi3,
Mkuu Nguruvi3, kwanza asante kuwa mchangiaji wa pili wa uzi huu, michango ya nyingi manguli inabeba a very heavy weight.
Kwanza ni kweli kwenye kila chaguzi duniani kote figisu ni kitu cha kawaida kama sehemu ya political propaganda machinery ila figusu za wenzetu sio za kwenye rules, regulations na procedures ambapo kwa kwetu tuna double standards.

Naunga mkono hoja, kama lengo ni kunusuru rasilimali za nchi, then washindi watangazwe tuu na tusiishie hapa hata uchaguzi wa 2020, lets save time, money and resources.
P
 
Naunga mkono hoja.
P
 
MENGELENI KWETU, Mkuu MENGELENI KWETU, sio kila kinachofanyika ni Magufuli, vitu vingine tunamsingizia bure huyu baba wa watu, hili kuwa JPM hakubaliki ni mtazamo tuu, hakuna research yoyote ku substience that, unaweza kudhani hivyo lakini matokeo ukakuta anakubalika kwa 99%.
Hili la wagombea urais kupimwa afya ya akili, naliunga mkono.
Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo!. Je, Tanzania tuna vichaa ...
P
 
Mkuu Mystery, Pasco ni yule yule juzi, jana na leo, kwenye mazuri napongeza, kwenye babaya nakosoa na kwenye mapungufu nashauri. Mimi sio member wa praise team ila kwenye mazuri kuna mengi namkubali sana Magufuli na kumpongeza, lakini kwenye makosa namkosoa. Praise team wao kazi yao ni moja tuu, kusifu, shangwe na mapambio.
Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri ...
Magufuli is Doing Good For This Nation, Tumuassess kwa Positive ...
Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya ...
Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The ...

P
 
Mohamed Said,
Mimi nilichotarajia ni kwamba taarifa za mtu ndiyo zitumike kumuengua mgombea na siyo kujaza form vibaya, kwani gharama ya kuchapisha form ni shilingi ngapi? Na msimamizi ni nani? Ni serikali ama ni CCM? Kama msimamizi ni serikali, mgombea akikosea kujaza form si huwa anaitwa na kupewa form ningine na kuelekezwa makosa katika form ya awali, kwani tunapoenda kujaza form za maombi ya aina yoyote serikalini.

Kawaida si tunaelekezwa kwanza namna ya kujaza form husika na pengine kuwekewa alama kabisa mahala pa sahihi ama dole gumba? Sasa usimamizi huu wa ki CCM CCM unatoka wapi serikalini? Tuipende Tanzania ndugu zangu, Nasisitiza, kwa mtandao wa CCM, Ushindi wa kati ya 60% na 70% ulikuwa wazi kabisa na unatosha sana, acheni tamaa ya ushindi wa 100%.
 
Waziri Jaffo yupo katika wakati mgumu, linalokuja kinywani analitamka halafu anafikiri baadaye.

Waziri kasema waliokosea kujaza fomu wameenguliwa kwa mujibu wa sheria.
Habari njema zimeanza, Waziri katangaza wagombea wote walioenguliwa kwa kujaza fomu vibaya warudishwe.
Huu sio mwanzo mbaya, sasa tunawasubiri Mbowe na Zitto kutangaza kuruhusu timu zao kuingia dimbani.
P
 
Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.
No sio kila kitu ni Magufuli, kujaza fomu wakosee wengine, lakini lawama ziende kwa rais Magufuli!.
Hata hivyo hoja yako imepita, Waziri Jafo katangaza msamaha kwa wote waliojaza fomu kimakosa, warudishwe.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…