Ushindi wa kishindo wa CCM Mbarali, ni fursa kwa upinzani kuwa mguu sawa

Ushindi wa kishindo wa CCM Mbarali, ni fursa kwa upinzani kuwa mguu sawa

Narudia tena, Tanzania hakuna uchaguzi Bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Ingekuwa wananchi ndio wanaamua nani awe madarakani kupitia box la kura, Leo hii ccm isingekuwa madarakani.

Hao ACT hawako madakani huko Zanzibar kwa sababu ya sera Bali ni mpasuko wa CUF ulipelekea Maalim Seif kuondoka na wafuasi wake na kuwabwaga ACT. Na kwa huko Zanzibar ushindani sio wa sera, Bali ni tofauti kati ya waunguja na wapemba. Fahamu ACT haikuanzia Zanzibar hivyo acha upotosha, Bali ACT walikutana na embe chini ya mnazi, baada kutokana na ugomvi wa CUF. Ukitaka kujua wananchi wanataka Nini kifanyike uchaguzi wa haki kisha uje utoe mrejesho hapa.
Chadema mbona mlipata mpemba Duni haji mtu mwenye nguvu kubwa siasa za Zanzibar mbona mlishindwa ku mu.handle hadi akakimbilia ACT wazalendo ambako alifanikisha ACT wazalendo kupata makamu wa Raisi ,na wabunge wengi bungeni

Hamjui siasa ,siasa inatumia mbinu zote kufanikisha jambo

Chadema mko sifuri kelele tu za unaharakati siasa mko zero
 
Ushindi mkubwa wa kishindo walioupata ccm katika jimbo la mabara-Jijini Mbeya, ni ishara njema ya kukubalika, kuimarika na kuaminika kwa chama cha mapinduzi kwa wananchi na uhakika wa kushinda chaguzi zijazo.

Lakini pia uchaguzi huo ni fursa muhimu zaidi kwa upinzani kujipima, kujitathimini, kujipanga na kubuni na kuibua mbinu na mikakati kabambe dhidi ya ccm inayoimarika kila uchwao na kuikabili vilivyo tena kisayansi na kwa sera madhubuti za kuwavutia na kuwashawishi wanachama wengi zaidi hususani vijana ili hatimae kuibuka na kura nyingi zaidi na kushinda mitaa mingi zaidi, Kata nyingi zaidi, majimbo mengi zaidi na Inshaalah Urais katika chaguzi zijazo.

Niwapongeze sana wote walioshiriki uchaguzi huo muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya jimbo la mbarali.
Niwapongeze mno waliopata ushindi, na ambao hawakupata ushindi kwa ungwana na ustaarabu wa kiwango kukubali matokeo. Hakika asie kubali kushindwa huyo si mshindani.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Bariki Demokrasia Tanzania.
Unashindana na kipofu kucheza mpira wa kikapu alafu unajisifia umeshinda kwa kishindo, na kwa kishindo unajimwambafai, hii nikujitapeli mwenyewe fikra zako bila sababu yoyote.

Tulia mkuu ccm hamna kitu, ombeni uchaguzi halisi usije fanyika mtatema ndoano kabla ya saa sita mchana
 
Chadema mbona mlipata mpemba Duni haji mtu mwenye nguvu kubwa siasa za Zanzibar mbona mlishindwa ku mu.handle hadi akakimbilia ACT wazalendo ambako alifanikisha ACT wazalendo kupata makamu wa Raisi ,na wabunge wengi bungeni

Hamjui siasa ,siasa inatumia mbinu zote kufanikisha jambo

Chadema mko sifuri kelele tu za unaharakati siasa mko zero
Mbinu zote... sasa wenzako hawataki haramu🤣😂
 
Chadema mbona mlipata mpemba Duni haji mtu mwenye nguvu kubwa siasa za Zanzibar mbona mlishindwa ku mu.handle hadi akakimbilia ACT wazalendo ambako alifanikisha ACT wazalendo kupata makamu wa Raisi ,na wabunge wengi bungeni

Hamjui siasa ,siasa inatumia mbinu zote kufanikisha jambo

Chadema mko sifuri kelele tu za unaharakati siasa mko zero
Huna ujualo Zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Cdm haimbelezi mtu yoyote, na isitoshe hicho kipindi huyo Duni yuko CDM, ndio cdm ilishinda huko Zanzibar na uchaguzi ukafutwa, Sasa sijui ni nguvu gani unaongelea. Na hakukimbilia ACT, Bali alirudi CUF, baadae wote wakamfuata maalim seif ACT.

Aliyekuwa na nguvu kubwa huko Zanzibar ni Maalim Seif na sio Duni Hadji. Na Hadi Maalim Seif anafariki alikuwa na mahusiano mazuri na cdm. Kumbuka uchaguzi wa 2020 Maalim Seif alimuunga mkono Tundu Lisu na sio Tapeli Membe RIP aliyekuwa mgombea wa Zito kupitia ACT. Kura za ACT huko Znz zilitolewa na wapemba kutokana na Imani yao waliyokuwanayo kwa Maalim Seif, huyo Duni Hadji ni mfaidika wa nguvu za Seif na sio kinyume chake. ACT haina wabunge wengi huko Zanzibar maana dhalimu Magufuli alinajisi uchaguzi na kupora haki ya wapemba. Wapemba wana mambo mawili kwenye siasa na wala hawajali sera. 1. Hawaitaki ccm kwa namna yoyote ile, na walikuwa na Imani na Maalim Seif, ama popote atakapowapeleka.
 
Watz tukisema ni wajinga wanatutukana yaani wao wanapenda kuambiwa kua wameibiwa tuh
Jitu limesusia uchaguzi wengine wameenda kupiga kura afu analalamika kura za wizi
Mara cjui sio halali yaani tumelogwa
Tengenezen mazingira ya tume huru ya uchaguzi ndo mjisifie.tofauti na hapo mnajisifia ujinga.
 
Uchaguzi hatakuwa wa HURU na HAKI iwapo CCM itaendelea kusimamia chaguzi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ambae ni KADA wa CCM hawezi kuaminika hata kidogo

Ni sawa sawa na SIMBA icheze na YANGA halafu REFARII awe ni mmoja wa wachezaji walio kwenye benchi la ufundi la YANGA.
Wenzako kwa akili zao wanaona ilo ni sawa na hakuna shida yoyote.Alafu wanajisifia kabisa.
 
Watz tukisema ni wajinga wanatutukana yaani wao wanapenda kuambiwa kua wameibiwa tuh
Jitu limesusia uchaguzi wengine wameenda kupiga kura afu analalamika kura za wizi
Mara cjui sio halali yaani tumelogwa
Huo wizi wa kura sio kwamba Kuna mtu anatuambia, huwa tunaona kwa macho yetu. Ukiona hakuna wizi ujue ccm wana uhakika wa kushinda. Na hakuna mtu anayejitambua atakwenda kushiriki uchaguzi ambao una maelekezo nani atangazwe mshindi, bila kujali Kura halali zinasema Nini.
 
Back
Top Bottom