Ushindi wa kishindo wa CCM Mbarali, ni fursa kwa upinzani kuwa mguu sawa

Chadema mbona mlipata mpemba Duni haji mtu mwenye nguvu kubwa siasa za Zanzibar mbona mlishindwa ku mu.handle hadi akakimbilia ACT wazalendo ambako alifanikisha ACT wazalendo kupata makamu wa Raisi ,na wabunge wengi bungeni

Hamjui siasa ,siasa inatumia mbinu zote kufanikisha jambo

Chadema mko sifuri kelele tu za unaharakati siasa mko zero
 
Unashindana na kipofu kucheza mpira wa kikapu alafu unajisifia umeshinda kwa kishindo, na kwa kishindo unajimwambafai, hii nikujitapeli mwenyewe fikra zako bila sababu yoyote.

Tulia mkuu ccm hamna kitu, ombeni uchaguzi halisi usije fanyika mtatema ndoano kabla ya saa sita mchana
 
Mbinu zote... sasa wenzako hawataki haramu🤣😂
 
Huna ujualo Zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Cdm haimbelezi mtu yoyote, na isitoshe hicho kipindi huyo Duni yuko CDM, ndio cdm ilishinda huko Zanzibar na uchaguzi ukafutwa, Sasa sijui ni nguvu gani unaongelea. Na hakukimbilia ACT, Bali alirudi CUF, baadae wote wakamfuata maalim seif ACT.

Aliyekuwa na nguvu kubwa huko Zanzibar ni Maalim Seif na sio Duni Hadji. Na Hadi Maalim Seif anafariki alikuwa na mahusiano mazuri na cdm. Kumbuka uchaguzi wa 2020 Maalim Seif alimuunga mkono Tundu Lisu na sio Tapeli Membe RIP aliyekuwa mgombea wa Zito kupitia ACT. Kura za ACT huko Znz zilitolewa na wapemba kutokana na Imani yao waliyokuwanayo kwa Maalim Seif, huyo Duni Hadji ni mfaidika wa nguvu za Seif na sio kinyume chake. ACT haina wabunge wengi huko Zanzibar maana dhalimu Magufuli alinajisi uchaguzi na kupora haki ya wapemba. Wapemba wana mambo mawili kwenye siasa na wala hawajali sera. 1. Hawaitaki ccm kwa namna yoyote ile, na walikuwa na Imani na Maalim Seif, ama popote atakapowapeleka.
 
Watz tukisema ni wajinga wanatutukana yaani wao wanapenda kuambiwa kua wameibiwa tuh
Jitu limesusia uchaguzi wengine wameenda kupiga kura afu analalamika kura za wizi
Mara cjui sio halali yaani tumelogwa
Tengenezen mazingira ya tume huru ya uchaguzi ndo mjisifie.tofauti na hapo mnajisifia ujinga.
 
Wenzako kwa akili zao wanaona ilo ni sawa na hakuna shida yoyote.Alafu wanajisifia kabisa.
 
Watz tukisema ni wajinga wanatutukana yaani wao wanapenda kuambiwa kua wameibiwa tuh
Jitu limesusia uchaguzi wengine wameenda kupiga kura afu analalamika kura za wizi
Mara cjui sio halali yaani tumelogwa
Huo wizi wa kura sio kwamba Kuna mtu anatuambia, huwa tunaona kwa macho yetu. Ukiona hakuna wizi ujue ccm wana uhakika wa kushinda. Na hakuna mtu anayejitambua atakwenda kushiriki uchaguzi ambao una maelekezo nani atangazwe mshindi, bila kujali Kura halali zinasema Nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…