Owk
Kwanza kabisa style walizotumia zimechangia kufanya haya matokeo.
Pac alicheza Othodox, yaan unamshambulia adui bila kumpa nafasi.
Na style hii mara nyingi kama umekusudia kumtoa knock out adui.
Alicheza vema kama angekutana na mtu wa style yake angeza shinda.
Combinations saba ila hazikumpatia matokeo. Ngumi nyingi zilipotea, hapa nielewe kuwa zilitua mahali ambako hakumpatii point.
Round ya tano speed ikaisha.
Money man yeye alitumia Rope a dope.
Unamchokoza adui na kumkimbia, huku ukimkejeli ili kumharibia malengo.
Ulishuhudia jamaa alivyokuwa akimsogezea uso adui. Alimdanganya. Alikuwa anajaa kwenye kona na hapa mpinzani (pac man alikuwa anakuja kwa nguvu maana kwa style yake eneo kama hili ni rahisi kummaliza adui) Myweather alikuwa anajua hilo na ndo maana akawa anachepuka kwa haraka kukimbia au kumfumbata.
Alikuwa anatupa ngumi za mbali pia.
Hakuwa anatupa ngumi nzito ila zilikuwa zinafika.
Kujihami pia ilikuwa balaa. Na laiti kama Pac man angekuwa hajatulia yan angepanic angepigwa, maana mchezo huu jazba au kukamia kukizidi ni tatizo.
Hivyo ndivyo alivyoshinda.