Ushirikiano kati ya Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) na China wahimiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika

Ushirikiano kati ya Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) na China wahimiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Fadhili Mpunji

VCG111383868682.jpg

Mwishoni mwa mwezi Mei, Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) iliitisha mkutano wake wa mwaka mjini Accra, Ghana kujadili maswala yanayohusu maendeleo ya benki hiyo, na mchango wake katika kuisaidia Afrika kukabiliana na changamoto mbalimbali. Kauli mbiu ya mkutano wa safari hii ilikuwa “Kufikia uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi, na mpito wa haki barani Afrika”, lengo kuu ni kuangalia jinsi Afrika inavyoweza kufanikisha mpito wa muundo wa nishati katika mazingira ya sasa ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika wiki za karibuni matukio kadhaa yanayotokana na hali mbaya ya hewa yameripotiwa barani Afrika. Kwanza ni mafuriko yaliyotokea katika jimbo la Kwazul-Natal nchini Afrika Kusini, na pili ni ukame mkali unaendelea nchini Ethiopia, Kenya na Somalia na kusababisha vifo vya mifugo mingi na hata kuhatarisha maisha ya watu kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula. Changamoto kama hivi zimetokea kwenye nchi mbalimbali za Afrika kwa viwango tofauti.

Wakati nchi nyingi za magharibi zikiwa zimeelekeza ufuatiliaji wake kwenye mgogoro wa Ukraine, misaada ya kibinadamu kwa nchi za Afrika inayotolewa na nchi hizo sasa imepungua sana au kutoweka kabisa. Katika hali hii Afrika inalazimika kujitegemea, au kuangalia wadau wengine wenye utayari wa kusaidia kukabiliana na changamoto hizo. Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) imekuwa ni chaguo la muhimu kwa nchi za Afrika

Madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuwa wazi, na uingiliaji wa kifedha ni moja ya njia bora ya kutatua changamoto hizo. Kutokana na mahitaji haya Benki ya Maendeleo ya Afrika imekuwa inashirikiana na China tangu mwaka 1985 kuimarisha uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo. Mfano mzuri ni mfuko wa pamoja wa dola bilioni 2 za kimarekani (Africa Growing Together Fund) ulioanzishwa kwa pamoja kati ya Benki Kuu ya China na AfDB. Mfuko huu umefadhili miradi muhimu kama ule wa mwaka 2018 wenye thamani ya dola milioni 50 za kimarekani wa kusambaza umeme vijijini nchini Nigeria, na mradi wa mwaka jana wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 20 wa kuzalisha megawati 50 za umeme kwenye mto Malagarasi nchini Tanzania.

Mbali na Benki Kuu ya China kushirikiana na AfDB, China kupitia benki zake nyingine imekuwa mchangiaji mkubwa wa mfuko wa maendeleo wa Afrika, ambao kwa sasa unajikita kwenye miradi ya nishati endelevu. Kwa mujibu wa takwimu za uwekezaji wa China kwenye mambo ya nishati duniani (China Global Energy Finance Database) kati ya mwaka 2008 na mwaka 2020, nchi za Afrika zilipokea asilimia 20 ya uwekezaji wa China wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 46, sehemu kubwa ya uwekezaji huo ulienda kwenye sekta za umeme wa nishati ya maji, umeme wa joto la ardhini, umeme wa nishati ya jua, umeme wa nishati ya upepo, na teknolojia nyingine zinazosaidia kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.

Ushirikiano kati ya China na Benki ya maendeleo ya Afrika, ni sehemu ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya China na Afrika, ambao haubadiliki bila kujali hali ya dunia inakuwaje. Kwa sasa hali ya kimataifa ina mabadiliko matatu makubwa. Mgogoro wa Ukraine ambao umefanya nchi za magharibi zihamishie ufuatiliaji wake kwa nchi hiyo, janga la COVID-19 ambalo limeonyesha kuwa nchi za magharibi hazina ufuatiliaji mkubwa kwa Afrika, na janga la ukame ambalo pia halijafuatiliwa vilivyo nchi za magharibi. China imekuwa pamoja na nchi za Afrika katika kipindi chote cha changamoto hizi, na hilo pia limeonekana kwenye mchango wake kwa Benki ya maendeleo ya Afrika, wakati ikitafuta njia ya kuzisaidia nchi za Afrika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
 
Back
Top Bottom