Ushirikiano Kati ya China na Afrika waweka mwelekeo sahihi wa kuboresha kilimo barani Afrika

Ushirikiano Kati ya China na Afrika waweka mwelekeo sahihi wa kuboresha kilimo barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1766556581679.png


Moja kati ya maeneo yanayotajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuliondoa bara la Afrika kwenye changamoto za umaskini na usalama wa chakula ni kuboresha sekta ya kilimo. Kutokana na bara la Afrika kuwa na ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo, idadi kubwa ya watu wanaojishughulisha na sekta ya kilimo, na mazingira ya asili yanayofaa kwa sekta ya kilimo, ni wazi kuwa ukiweka mkazo wa kutosha katika sekta hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mabadiliko chanya.



Pamoja na ukweli huo, sekta ya kilimo barani Afrika bado iko nyuma sana, takwimu zilizotolewa hivi karibuni na shirika la misaada la Uingereza Oxfam, zinasema kwa sasa watu milioni 57 barani Afrika wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, yanayosababisha upungufu wa maji na chakula. Hali hii inatokea wakati katika maeneo mengine ya Afrika uzalishaji wa chakula umeongezeka na chakula kinaharibika kutokana na kutokuwepo kwa mbinu za kisasa za utunzaji, na kukosekana kwa miundo mbinu ya kufikisha chakula hicho kwenye maeneo yanayohitajika.



Kutokana na kuimarika kwa Ushirikiano kati ya China na Afrika, hasa kupitia mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, (FOCAC) baadhi ya maeneo yenye changamoto kubwa kwenye sekta ya kilimo barani Afrika yamekuwa yakifanyiwa kazi.



Eneo la kwanza ni kupeleka teknolojia za kisasa za uzalishaji wa mazao ya kilimo. Hadi sasa kumekuwa na idadi kubwa ya maofisa ugani kutoka nchi za Afrika wanaopata mafunzo ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo mashambani. Kupitia ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, maofisa ugani wa nchi za Afrika wanakuja kupata mafunzo ya nadharia katika madarasa ya chuo hicho mjini Beijing, na baadaye kupelekwa mashambani mkoani Hebei ambako hupewa mafunzo ya moja kwa moja ya kivitendo, tangu hatua ya kuandaa shamba, kupanda, kuweka mbolea, kumwagilia shamba, kuvuna, na kuhifadhi mazao. Mchakato wote wa mafunzo huambatana na upimaji wa maendeleo ya mimea kupitia maabara za kisasa. Kupitia utaratibu huo vijana kadhaa kutoka Tanzania, Malawi, Kenya, Zimbabwe na sehemu nyingine za Afrika wameweza kupata mafunzo na kurudi nyumbani kusaidia kuongeza uzalishaji wa kilimo.



Eneo la pili ni kuanzishwa kwa vituo vya mfano katika maeneo mbalimbali ya Afrika. Watalaam kutoka China na wale wa nchi za waliopata mafunzo nchini China, wanashirikiana kufanya yale waliyojifunza nchini China kwenye ardhi ya nchi za Afrika na kuwa na matokeo ya kuridhisha. Katika vituo hivyo, na kwenye mashamba yenye ushirikiano na vituo hivyo uzalishaji wa mazao ya chakula na mazao ya biashara umeongezeka kwa viwango tofauti.



Eneo la tatu, ni ujenzi wa miundombinu hasa kwenye maeneo yenye mazingira mazuri zaidi kijiografia kwenye uzalishaji wa kilimo. Miundo mbinu hii imekuwa na msaada mkubwa kwanza kwenye kusafirisha chakula kutoka kwenye maeneo yenye chakula cha ziada na kukifikisha sokoni na kwenye maeneo yenye mahitaji makubwa, na pili kusafirisha pembejeo za kilimo kutoka kwenye maeneo zinakopatikana hadi kwenye maeneo ya kilimo.



Hata hivyo pamoja na hatua hizo, uzalishaji bado haitoshi, kwa kuwa hatua hizo zinatekelezwa katika maeneo madogo. Kupitia uwekezaji zaidi na kupanua mafanikio hayo kwenye maeneo makubwa, changamoto ya usalama wa chakula itaondolewa, na hata uzalishaji wa chakula na mazao mengine ya kilimo unaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye uchumi wa nchi mbalimbali za Afrika.
 
Back
Top Bottom