Mkuu, nimekukera? Sipendi siasa za tyoe ya kina Nape kuingia nyumbani kwa wenye dhiki na kujidai kula nao mlo mmoja ili tuamini wako pamoja nao. Huo ni ulaghai wa kisiasa, lazima tujifunze kuukataa ulaghai huu. Viongozi hawa tunazvijua vipato vyao na maisha yao kwa ujumla, hivyo muunganiko wao na jamii usihesabiwe kwa sababu tu wanazuga kula pamoja na wenye dhiki kwa siku moja, bali tuwapime kwa juhudi zao kujaribu kuwanyanyua wenye dhiki toka chini na kuwapandisha juu.
Tupime matokeo ya uwajibikaji wao kwenye mambo ya msingi kwa ujumla wake. Kama mtu akijidai kula nami eti kwa sababu tu uchaguzi umekaribia, wakati mwenyewe najua nimenunua nyanya moja shilingi 600 na mchele kilo shilingi 3,000 nitamtimua bila masikhara!! Siasa za usanii sanii ndizo zinazoua uchumi wa nchi hii na kuwaweka wanyonge kuwa wafungwa wa wenye nafasi. Sipendi na nachukia mno wapinzani wanapoiga aina hii ya siasa wakati wao wanatakiwa kujipambanua kwa kujenga misingi bora ya siasa. Mambo ya kusifiwa kwa kunengua na wanavijiji wawaachie kina Kangi Lugola, tunataka matokeo chanya katika kumkwamua mwananchi wa kipato cha chini.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk