Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika wastawi

Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika wastawi

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
mmexport1750299556052.jpg

Maonesho ya Nne ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yamefanyika hivi karibuni huko Changsha mkoani Hunan, China, na kushirikisha zaidi ya watu elfu 30 kutoka nchi 53 za Afrika, mashirika 11 ya kimataifa, na zaidi ya kampuni 4,700 kutoka China na nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, ushirikiano wao wa uchumi na biashara umepata mafanikio mazuri.

Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika ni hatua halisi ya kwanza ya utekelezaji wa “Hatua Nane” za kuhimiza ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika zilizotangazwa na Rais Xi Jinping wa China katika Mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing mwaka 2018, ili kujenga jukwaa jipya la ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili.

Ingawa China na Afrika zina umbali wa zaidi ya kilomita elfu 10, ushirikiano wao wa uchumi na biashara una historia ndefu. tangu miaka elfu moja iliyopita, wakati hariri na kauri za China zilianza kusafirishwa kwenda Afrika kupitia meli za wafanyabiashara. Majumba ya kumbukumbu yaliyoko pwani ya Kenya bado yanahifadhi vipande vingi vya kauri vya China. Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China imedumisha ushirikiano mazuri wa uchumi na biashara na nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, majukwaa ya FOCAC na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” yameendelea kuchangia maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili pia umepanuliwa na kukuzwa siku hadi siku.

Ushirikiano wa uchumi na biashara ni moja ya sehemu muhimu zaidi ya uhusiano kati ya China na Afrika. Ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea, China ina mfumo kamili zaidi wa uzalishaji wa viwanda na soko kubwa zaidi la bidhaa na huduma duniani. Kwa upande mwingine, likiwa bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, Afrika ina maliasili nyingi na soko linaloendelea kukua kwa haraka. Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili una nafasi pana ya ukuaji.

Katika miaka ya hivi karibuni, China na nchi za Afrika zimenufaishana katika ushirikiano wao wa uchumi na biashara. Bidhaa za China za bei rahisi na ubora wa juu zimeingia kila mahali barani Afrika. Wakati huohuo, kampuni za China pia zimeanza kuzalisha bidhaa katika nchi za Afrika, na licha ya kukidhi mahitaji ya wenyeji, bidhaa hizo pia zinauzwa kwa nchi za nje, na hali hii imeongeza pato la taifa la nchi hizo za Afrika. Kwa upande mwingine, licha ya kutoa bidhaa kubwa zikiwemo mafuta na madini kwa China, katika miaka ya hivi karibuni, bidhaa nyingine bora za Afrika pia zimeingia kwenye soko la China. kwa mfano maua ya Kenya, kahawa ya Rwanda, na matunda ya Afrika Kusini, na vinapendwa sana na wateja wa China.

Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola bilioni 295.6 za Kimarekani, na kuvunja tena rekodi ya historia. China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika. Maonesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yamekuwa njia muhimu ya kukuza ushirikiano wa biashara kati ya pande hizo mbili. Habari zinasema, katika maonesho hayo ya mwaka huu, China na Afrika zilisaini miradi 176 ya ushirikiano, ambayo ina thamani ya dola bilioni 11.39 za Kimarekani.

China na Afrika ni marafiki, wenzi na ndugu wakubwa. Kutokana na juhudi za pamoja za pande hizo mbili, ushirikiano wao wa uchumi na biashara utakuwa na mustakabali mzuri zaidi, na kuendelea kuchangia juhudi za kutimiza ndoto ya Wachina ya ustawishaji wa taifa la China na ndoto ya Waafrika ya mshikamano na maendeleo.
 
Huwa nashangaa sana nchi za Afrika kuikumbatia China! Kwamba huwa hawafuatilii mienendo yake?.
 
Back
Top Bottom